
25/07/2025
Kabila Ashtakiwa Kwa Makosa Ambayo Adhabu Yake Ni Kifo…..
Mahak**a Kuu ya Kijeshi mjini Kinshasa, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, leo inaanza kusikiliza kesi ya mashtaka ya kijeshi dhidi ya Joseph Kabila, rais wa zamani wa nchi hiyo, kwa tuhuma zinazohusiana na madai yake ya uanachama wa AFC/M23.
Haijabainika iwapo Kabila, ambaye amerejea nchini mwake katika eneo linalodhibitiwa na waasi wa M23, atafikishwa mahak**ani. Inatarajiwa kwamba anaweza kuhukumiwa bila kuwepo kwake.
Hii ilikuwa ni baada ya Bunge kumuondolea kinga, na bado hakuweza kujieleza kuhusu tuhuma zinazomkabili.
Katika kesi hiyo inayoanza saa 9:00 alasiri kwa saa za Kinshasa, Kabila anatuhumiwa kwa makosa ya jinai yakiwemo kushirikiana na kundi la waasi, Usaliti, Kuhalalisha uasi, Mateso, Kuua kwa risasi, Ubakaji jijini Goma, na Kuvuruga amani.
Baadhi ya makosa haya yanaadhibiwa na kifo chini ya sheria za DRC.