Msasa Online

Msasa Online Matangazo Piga Simu +255758379300
(1)

MSASA ONLINE
Ni kiwanda cha habari kinacho tumia ubunifu na uvumbuzi wa teknolojia kwa kutoa habari, michezo, burudani, na elimu kidijitali kwa wafuasi wake na jamii inayozungumza kiswahili duniani kote karibu.

  KATIBU MKUU MRAMBA AKUTANA NA KAMPUNI YA NYUKLIA YA CHINA....Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mha. Felchesmi Mramba a...
21/09/2025


KATIBU MKUU MRAMBA AKUTANA NA KAMPUNI YA NYUKLIA YA CHINA....

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mha. Felchesmi Mramba ameongoza ujumbe wa Serikali ya Tanzania katika kikao na Shirika la Taifa la Nyuklia la China (China National Nuclear Corporation – CNNC), kujadili fursa za ushirikiano katika kuanzisha na kuendeleza mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia teknolojia ya nyuklia.

Katika kikao kilichofanyika jijini Vienna, Austria pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa 69 Wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomi (IAEA), Wawakilishi wa CNNC waliieleza Tanzania kuwa kampuni hiyo ina uzoefu mkubwa katika kujenga na kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme wa nyuklia, na wako tayari kushirikiana na Tanzania katika hatua mbalimbali za utekelezaji wa miradi ya aina hiyo.

“Tanzania imeanza maandalizi ya kuzalisha umeme kwa kutumia nyuklia ikiwa ni utekelezaji wa dhamira na nia njema ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuona nchi inakuwa na vyanzo endelevu, salama na vya uhakika vya nishati, hivyo tupo tayari kushirikiana na CNNC katika safari hii ya kuzalisha umeme wa nyuklia." Amesema Mramba

Ametoa shukrani kwa CNNC kwa kuonesha nia ya kushirikiana na Tanzania, akibainisha kuwa Serikali ya Tanzania imeamua kuwekeza katika mradi wa kuzalisha umeme wa nyuklia k**a sehemu ya mkakati wa kuongeza upatikanaji wa nishati endelevu na ya uhakika.

Katika kikao hicho, CNNC imeahidi kushirikiana na Tanzania katika kujenga uwezo wa kitaalamu kwa Watanzania kupitia mafunzo ya kiufundi, ziara za mafunzo, pamoja na kutoa ufadhili kwa masomo ya uzamili katika fani ya nyuklia. Hatua inayolenga kuhakikisha Tanzania inakuwa na wataalamu wa kutosha kusimamia na kuendeleza miradi ya nishati ya nyuklia nchini.

 Arsenal Na Manchester City EPL Leo…Jumapili nzuri kwa wapenda soka na wana uchumi, wakati Arsenal wakiwakaribisha Manch...
21/09/2025


Arsenal Na Manchester City EPL Leo…

Jumapili nzuri kwa wapenda soka na wana uchumi, wakati Arsenal wakiwakaribisha Manchester City katika viunga vya Emirates.

Siku ya pili baada ya jana wababe wa Dunia Chelsea kufungwa pale Old Trafford, leo ni kazi ya Arsenal kuitetea London.

Manchester City wanaenda kucheza mchezo wa tano hii leo wakati wamepoteza michezo miwili mpaka sasa, wakati Arsenal wakiwa wamepoteza mchezo mmoja pekee na kushinda mitatu na mpaka sasa wana alama 9.

Manchester City katika msimamo wapo nafasi ya 12 na alama zao 6 huku zikiwa ni takwimu mbovu zaidi tangu kikosi hicho kianze kunolewa na Pep Guardiola mwaka 2016.

 Maelfu Ya Raia Waandamana Ufilipino Kwa Kashfa Ya UfisadiMaelfu ya waandamanaji wameingia barabarani katika mji mkuu wa...
21/09/2025


Maelfu Ya Raia Waandamana Ufilipino Kwa Kashfa Ya Ufisadi

Maelfu ya waandamanaji wameingia barabarani katika mji mkuu wa Ufilipino Manila, leo Jumapili kuelezea ghadhabu yao juu ya kashfa ya ufisadi iliyohusisha wabunge, maafisa na wafanyabiashara ambao wanadaiwa kujipatia pesa nyingi kutoka kwa miradi ya kudhibiti mafuriko katika nchi hiyo iliyokumbwa na umaskini na kukumbwa na dhoruba ya Kusini Mashariki mwa Asia.

Vikosi vya polisi vimewekwa katika hali ya tahadhari ili kuzuia kutokea kwa vurugu zozote, wengine wametumwa ili kupata udhibiti wa maandamano tofauti katika bustani ya kihistoria ya Manila na karibu na mnara wa demokrasia kando ya barabara kuu, pia katika eneo la mji mkuu, ambapo waandaaji walitarajia kuwa na idadi wakipinga ufisadi katika miaka ya hivi karibuni.

Kundi la waandamanaji lilipeperusha bendera za Ufilipino na kuonyesha bango lililosomeka kwa jumbe za kupinga ufisadi na kutaka hatua za kisheria zichukuliwe kwa wahusika.

Wahamasishajii wamesema waandamanaji watajikita katika kuwashutumu waliohusika na ufisadi wa kazi za umma, wabunge na wamiliki wa makampuni ya ujenzi, pamoja na mfumo unaoruhusu ufisadi mkubwa, lakini hawatamtaka Rais Ferdinand Marcos Junior kuachia ngazi.

Kashfa hiyo iliibuliwa na rais Marcos alipotoa hotuba iliyoangazia mapungufu katika miradi mingi ya udhibiti mafuriko.

Baadaye alianzisha tume huru ya kuchunguza kile alichosema kuwa hitilafu katika miradi hiyo yenye thamani ya dola bilioni 9.5 za Marekani ambazo zilipaswa kutekelezwa tangu aingie madarakani katikati ya mwaka 2022.

Hasira ya umma ilizuka zaidi wakati wanandoa matajiri ambao waliendesha makampuni kadhaa ya ujenzi ambayo yalishinda kandarasi za mradi wa kudhibiti mafuriko walionyesha makumi ya magari ya kifahari ya Ulaya na Marekani na meli wanazomiliki wakati wa mahojiano na vyombo vya habari.

 Karibu mdau wetu. Hizi ni kurasa za mbele na nyuma za magazeti ya hapa Tanzania.
21/09/2025


Karibu mdau wetu. Hizi ni kurasa za mbele na nyuma za magazeti ya hapa Tanzania.

 Manchester United Na Chelsea Leo Pale Old Trafford....Wiki hii wapenzi wa ligi kuu soka Uingereza(EPL) tutabahatika kus...
20/09/2025


Manchester United Na Chelsea Leo Pale Old Trafford....

Wiki hii wapenzi wa ligi kuu soka Uingereza(EPL) tutabahatika kushuhudia timu kubwa za London na za kutoka jiji Maarufu la Manchester zikikutana, kitu ambacho ni nadra sana kutokea, mara ya mwisho ilikua ni februari 2018 wakati Manchester United walipoifunga Chelsea 2-1 katika ligi kuu halafu Manchester City wakainyuka Arsenal 3-0 pale Wembley katika fainali ya kombe la ligi lijulikanalo k**a Carabao.

Katika ligi kuu hii ni mara ya kwanza kwa timu kubwa za Manchester Kukutana na timu kubwa za London ndani ya wiki moja.
Kabla ya kesho kushuhudia Arsenal watakapoialika Manchester City, Leo zinakutana timu zenye mashabiki wenye kelele zaidi Duniani pale Old Trafford Manchester United wanawaalika Chelsea.

Chelsea wanaenda Old Trafford huku wakikumbuka kuwa mara ya mwisho kuvuna alama 3 pale ilikua ni miaka 12 iliyopita ambapo waliamua kumuaga vizuri kocha mwenye heshima zaidi Old Trafford Sir Alex Ferguson walipomfunga goli 1-0 kupitia kwa Juan Mata mnamo Mei 5, 2013 na ndio mwaka aliostaafu Ferguson.

Leo tunazishuhudia timu hizi ambazo bado hazijajengeka huku Manchester United ikiwa katika hali mbaya zaidi mwanzoni tu mwa ligi kuu,huku katika ligi mpaka sasa imeshinda mchezo mmoja pekee ikifungwa mechi 2 na sare 1 kwenye mechi 5 zilizopita.

Chelsea haijafungwa mpaka sasa katika mechi 4 za mwanzo ikitoa sare 2 na kushinda 2, ikiwa na safu imara ya ushambuliaji chini ya Joao Pedro, Pedro Neto na Liam Delap.

Mechi ni muda mchache Ujao, je Chelsea wataendelea kupaona pagumu Old Trafford au ndio United watawaruhusu Chelsea kushinda?

Address

Mbezi Louis
Ubungo
0000

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Msasa Online posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share