Mzawaonline

Mzawaonline Ukurasa Rasmi wa Mzawa Online

19/09/2025

Mgombea ubunge wa Jimbo la Kisarawe kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Seleman Jafo, ameahidi kuwa endapo ataendelea kupewa ridhaa ya kuwatumikia wananchi katika kipindi cha miaka mitano ijayo, atahakikisha kunakuwepo na mikopo yenye tija kwa wanawake na vijana, pamoja na kuanzisha viwanda vidogo vidogo vitakavyoongeza ajira na thamani ya mazao.

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Chakenge, Kata ya Mzenga, Dkt. Jafo alisema katika kipindi kilichopita kulikuwa na changamoto katika utoaji wa mikopo, kwani baadhi ya maeneo walitumia vibaya fedha hizo, hali iliyosababisha serikali kusitisha na kuweka utaratibu mpya unaolenga kuhakikisha mikopo inaleta manufaa yaliyokusudiwa.

Aidha, Dkt. Jafo alieleza kuwa tayari wamefanikiwa kujenga kiwanda cha korosho, ambacho kinatarajiwa kutoa ajira kwa vijana na kuongeza thamani ya zao hilo muhimu katika wilaya ya Kisarawe.

17/09/2025

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan amewatoa wasiwasi Watanzania akiwahakikishia kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga kikamilifu katika kuilinda Tanzania na kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na salama.

Dkt. Samia akirejea ahadi yake wakati anajitambulisha kwa Watanzania mara baada ya Chama chake kumpa ridhaa ya kuwania nafasi ya Urais, akiwa mwanamke wa kwanza kupewa nafasi hiyo katika Historia ya Chama hicho, amesema amelazimika kuyasema hayo mara baada ya Wazee wa Pemba kumuomba kusimamia amani na utulivu katika uchaguzi huo Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

"Tunakwenda kwenye uchaguzi Mkuu, ninaowaomba sana twende tudumishe amani na utulivu. Uchaguzi si vita, uchaguzi ni tendo la kidemokrasia ni watu kwenda kwenye utaratibu uliowekwa, kuweka kura zetu, rudi nyumbani katulie ili nchi ibaki salama. Si muda wote kushika silaha kunaleta suluhu ya maana, niwaombe sana ndugu zangu amani na utulivu wa nchi yetu ni jambo muhimu kuliko jambo lolote. Hutaki kishindo kapige kura rudi nyumbani tulia." Amesema Dkt. Samia.

Dkt. Samia yupo Visiwani Zanzibar kwenye ziara zake za Kampeni, ambapo awali pia amesisitiza kuwa ikiwa Watanzania watampa ridhaa ya kuongoza serikali atahakikisha pia analinda kwa bidii zake zote tunu za Taifa ambazo ni amani, umoja na mshik**ano k**a sehemu ya kuenzi jitihada zilizofanywa na waasisi wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Amani Abeid Karume.

04/09/2025

Wakazi wa Kigoma waaswa kuunga mkono jitihada za Serikali katika utunzaji wa mazingira kwa kutumia nishati safi na salama ya kupikia

Wito huo umetolewa leo Septemba 04, 2025 na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Simon Nyakoro Sirro wakati akipokea mradi wa uuzaji na usambazaji wa majiko banifu unaosimamiwa na kuratibiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) .

"Kinachofanyika leo ni kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za matumizi ya nishati safi na salama katika kutunza mazingira na kuboresha Afya za wananchi" amesema Mkuu wa mkoa Mhe. Sirro, alipokuwa akipokea mradi huo.

Akiwasilisha taarifa ya mradi kwa mkuu wa mkoa, Mhandisi wa Miradi kutoka wakala wa Nishati Vijijini (REA), Raya Majallah amesema,

“Mradi huu unalenga kusambaza majiko banifu ili kukuza upatikanaji wa Nishati safi na endelevu, kupanua usambazaji wa Nishati mbadala katika maeneo ya vijijini na hivyo kuhamasisha matumizi ya teknolojia safi kupitia teknolojia za kisasa na bora za kupikia.

Katika kufanikisha hilo, Wakala wa Nishati Vijijini umekuja na mpango wa usambazaji na uuzaji wa majiko banifu 200,000 kwa bei ya ruzuku.

Mradi huu unagharimu kiasi cha zaidi ya TZS 429.5 ambapo serikali itatoa ruzuku ya TZS 365.1 na kufanikisha usambazaji na uuzaji wa majiko 8,424.

Uuzaji na usambazaji wa majiko banifu utafanyika katika wilaya Sita (6) za mkoa wa Kigoma ambazo ni wilaya ya Buhingwe, Kakonko, Kasulu, Kibondo, Kigoma Vijijini na wilaya ya Uvinza na kila wilaya kupata majiko 1,404.

Mikataba ya mradi huu ilisainiwa tarehe 09 Mei, 2025 kati ya REA na mtoa huduma kampuni ya Envotec Services Limited. Mtoa huduma atazambaza na kuuza majiko banifu kwa bei ya ruzuku katika wilaya zote Sita.

Gharama ya jiko moja ni TZS 50,990 lakini serikali imetoa ruzuku ya asilimia 85 sawa na TZS 43,341.50 na hivyo mwananchi atanunua jiko kwa kiasi cha TZS 7,649 tu.

Kwa upande wake Afisa masoko wa Kampuni ya Envotec Services Limited, Bi Kisa Sefa Mwamwaja amesema, majiko haya banifu yametengenezwa kwa kutumia Teknolojia za kisasa ambazo hazihitaji matumizi makubwa ya kuni na mkaa wakati wa kupika na hivyo kusaidia katika utunzaji wa mazingira.

31/08/2025

Mgombea ubunge wa Jimbo la Kisarawe kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Seleman Jafo, ameahidi kuimarisha kilimo kwa kuanzisha vitalu vya mikorosho na minazi, pamoja na mazao mengine. Amesema hatua ya mwanzo itakuwa kuanzisha shamba la vitalu darasa la minazi na mikorosho, ili kuhakikisha wananchi wananufaika zaidi na fursa za kilimo.

Dkt. Jafo aliyasema hayo Agosti 30, 2025, wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi uliofanyika Kisarawe.

Mkuu wa  Mkoa  wa Manyara Mhe. Queen  Sendiga  leo Julai 11,2025 wilayani Hanang amezindua rasmi mradi wa usambazaji wa ...
11/07/2025

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga leo Julai 11,2025 wilayani Hanang amezindua rasmi mradi wa usambazaji wa mitungi ya gesi ya kilo sita kwa bei ya ruzuku mkoa wa Manyara. uzinduzi huo umeongozwa na mkuu wa mkoa pamoja na viongozi wengine wa mkoa, wilaya, kata pamoja na vijiji na vitongoji vyake.

Mhe. Sendiga amesema lengo la uzinduzi mradi ni kuutambulisha rasmi mradi kwa wananchi wa mkoa wa Manyara ambao ndio walengwa na wanufaika wa mradi.

Mhe. Sendiga, amepongeza juhudi za Serikali na REA katika kufanikisha utekelezaji wa mradi na kuongeza kuwa lengo la Mkakati wa Nishati Safi ya Kupikia ni kuwa ifikapo mwaka 2034, asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia, jambo ambalo litasaidia kutunza na kuhifadhi mazingira.

“Serikali, imeweka ruzuku ya asilimia 50, kwa hiyo wakina Baba na kina Mama wa mkoa wa Manyara, wajiandae kutumia gesi, tuwapunguzie wakina Mama kushika masizi, kutumia kuni na mikaa, kwetu sisi Mradi huu ni neema”. Alisema, Mhe. Sendiga.

Kwa upande wake, Msimamizi wa mradi kutoka REA, ndugu Abdulrazack Mkomi amesema kwa nchi nzima Mradi huo wa kusambaza mitungi ya gesi ya kilo 6 kwa Wananchi utagharimu shilingi bilioni 8 ambapo kwa mkoa wa Manyara zaidi ya shilingi milioni 284 zitatumika kugharamia mitungi 16,275 kwa mkoa mzima na kila wilaya mitungi 3,255 itasambazwa

“Kampuni ya MANJIS imeshinda, tenda ya kusambaza mitungi hiyo, ilitangaza ofa ya kusambaza mtungi mmoja kwa shilingi 35,000 kwa kutambua hilo, Serikali italipia asilimia 50 ya bei hiyo, ambayo itakuwa shilingi 17,500.” Alifafanua, Mkomi.

Mkomi, amesema ili kupata mtungi huo wenye ruzuku ya Serikali kila Mwananchi anapaswa kuwa na kitambulisho cha NIDA.

Aidha Mhe. Sendiga amewaomba wananchi kutoa ushirikiano wakutosha kwa mtoa huduma (MANJIS LOGISTICS LTD) ili kufanikisha utekelezaji wa mradi na kuwasihi wananchi kutumia fursa ya upatikanaji wa mitungi ya gesi kwa bei ya ruzuku kuweza kuachana na matumizi ya nishati zisizo salama za kupikia ili kuweza kutunza na kuboresha afya zao ,mazingira pamoja na kuimarisha usawa wa kijinsia.

Mkoa wa Manyara una jumla ya wilaya 5 ambazo Wananchi wake watanufaika na mitungi ya gesi ni pamoja na wilaya ya Babati, Hanang, Simanjiro, Mbulu na Kiteto.

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Dk. Selemani Jafo, amechukua fomu ya kuwania nafasi ya Ubunge kwa mara nyingine t...
29/06/2025

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Dk. Selemani Jafo, amechukua fomu ya kuwania nafasi ya Ubunge kwa mara nyingine tena kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Dk. Jafo amejaza fomu hiyo na kuirejesha kwa Katibu wa Chama hicho wa Wilaya ya Kisarawe, Ndugu Josephine Mwanga.

Address

Kimara S**a
Dar Es Salaam
1615

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mzawaonline posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share