26/09/2025
“Tunafahamu ya kwamba tuna mechi ya Ligi ya Mabingwa siku ya Jumapili kwenye dimba la Mkapa kuanzia saa 10 jioni na tayari wageni wetu Gaborone United wamewasili alfajiri ya leo. Mambo yote yamekwenda vizuri na watafanya mazoezi leo na kesho.”
“Mchezo wetu wa Jumapili utachezeshwa na waamuzi kutoka nchini Niger na sasa wapo njiani. Kikosi kiliingia kambini jana baada ya mchezo dhidi ya Fountain Gate walirudi kambini na wapo timamu, hakuna mtu yeyote ambaye alipata majeraha. Watakaokosa mchezo ni Mohammed Bajaber na Abdulrazak Hamza.”
“Nipo hapa kuwathibitishia kwamba mechi yetu ya Jumapili haitakuwa na mashabiki kutumikia adhabu ya CAF. Kilichosababisha ni mchezo ni dhidi ya Al Masry, kuna shabiki aliingia uwanjani na kuna mashabiki waliwasha moto. Adhabu hiyo inakwenda pamoja na faini ya Dola 50,000 k**a Tsh. 120 milioni hivi.”
“Niwaase mashabiki wenzangu wa Simba, uache vitendo vya vurugu uwanjani. Kwanza tuanze ulinzi wa wenyewe kwa wenyewe ukiona mtu anataka kuwasha zile fire works mzuie, ukiona mtu anataka kuingia uwanjani tushirikiane kumzuia ikiwezekana kumtoa uwanjani. Angalia mechi k**a hii tunakwenda uwanjani bila mashabiki. Hatupo hapa kulaumiana ila kukumbushana.”
“Hasara ya kwanza tunakosa mashabiki, hasara ya pili tunakosa mapato na hasara ya tatu tunalipa faini ya USD 50,000. Vilevile tumepewa adhabu kutokana na mechi ya fainaili dhidi ya RS Berkane, huku vilevile tuliwasha fireworks. Kwenye mechi ya fainali tumetozwa faini ya USD 35,000. Jumla Tumetoshwa USD 85,000 sawa na Tsh. 200 milioni.”
“Tunacheza bila mashabiki kwenye mechi dhidi ya Gaborone United pekee lakini sbaabu tumefanya makosa mfululizo CAF watakuwa makini na sisi kwelikweli sababu wanaona tunafanya vitendo ambavyo sio vya kiungwana hivyo watakuwa wanaangalia k**a Simba Sports Club tumebadilika. Ni lazima tuwe makini kwelikweli ili kuwaonyesha kwamba tumejifunza na tumebadilika. Kuanzia hivi sasa tuchukue taswira mpya kwenye eneo la ushabiki.”
“Wapo mashabiki ambao wametaka kuwa sehemu ya maumivu ambayo tunapitia Klabu ya Simba na maumivu yenyewe ni faini ya Tsh. 212,500,000 sawa na USD 85,000. Kwa mapenzi yao mashabiki wameomba kuchangia faini ili kuipunguzia klabu mzigo na sisi tumepokea na tumeridhia mashabiki wachangie hususani kwenye eneo la faini.”- Semaji Ahmed Ally.