07/01/2026
Njama ya kumuua kiongozi wa kijeshi wa Burkina Faso, Kapteni Ibrahim Traoré, imeshindwa kufanikiwa, kwa mujibu taarifa iliyotolewa msemaji wa wa taifa hilo la Afrika Magharibi.
Taarifa imeadai kwamba mpango huo ulipangwa kitaalamu na Luteni Kanali Paul Henri Damiba, afisa wa kijeshi aliyeondolewa madarakani na Traore mnamo Septemba 2022.
Katika taarifa yake kwa umma, Waziri wa Usalama amesema, “Mipango yetu ya ulinzi na kijasusi iliingilia kati mpango huo haramu katika saa za mwisho za utekelezaji. Walikuwa wamepanga kumuua kiongozi wa taifa kisha kushambulia taasisi nyingine muhimu, wakiwemo baadhi ya viongozi wa kiraia,” amesema Mahamadou Sana na kuongeza kwamba njama hiyo imefadhiliwa na nchi jirani.
Hakuna maoni yoyote yaliyotolewa na Kanali Damiba au nchi iliyolalamikiwa kufadhili tukio hilo.
Tangu alipochukua madaraka, Kapteni Traore amekabiliana na jaribio la mapinduzi takribani mara mbili, hii ikiwa ya tatu na pia amekuwa akikabiliana na waasi, hatua ambayo imesababisha mamilioni ya watu kuondoka kwenye makazi yao.
Licha ya changamoto hizi na sifa yake ya kuwa kiongozi mkali, kiongozi huyo wa kijeshi mwenye umri wa miaka 37 anaendelea kupata umaarufu mkubwa miongoni mwa wananchi na amejipatia mashabiki kote barani Afrika kutokana na maono yake kuhusu umajumui wa Afrika na ukosoaji wake wa siasa za Magharibi kuhusu Afrika.
Tufuatilie kupitia ndani ya kisimbuzi cha CH 161 (antena) CH 401 (Dish) pamoja na kwenye YouTube channel yetu ya Kwa Taarifa zaidi.