30/11/2025
: Waziri Mkuu wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameliagiza Jeshi la Polisi liache kumtafuta Askofu Dkt. Josephat Gwajima k**a walivyokuwa wametangaza awali ili aweze kuendelea shughuli zake.
Amesema baada ya kutoa msamaha kwa Kanisa la Ufufuo na Uzima, waumini wanahitaji wamuone kiongozi wao, hivyo anatakiwa ajitokeze hadharani aendelee na kazi yake. “Mwacheni ajitokekeze tujenge umoja wa kitaifa, tushik**ane kurudisha umoja wa kitaifa. Tumekutana na TEC, viongozi wa dini, wa mila na viongozi mbalimbali; twendeni sote kwenye jambo hili, tujitokeze tuhamasishe Tanzania yenye amani, huu ndio wito wa kiongozi wetu wa nchi”
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumapili, Novemba 30, 2025) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa Arumeru katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Magufuli Leganga, kata ya Usa River, wilayani Arumeru mkoani Arusha.
Waziri Mkuu amewataka Watanzania wakatae kushawishiwa na wanaharakati wanaochochea vurugu kwani zinarudisha nyuma maendeleo ya nchi. "Nimekuja kuwapa pole wananchi wenzangu, kwa niaba ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Anatambua mambo yanayoendelea. Anatambua kazi kubwa ya kujenga Taifa mnayoifanya," amesema.
Kabla ya mkutano huo, Waziri Mkuu alikagua uharibifu uliofanywa wakati wa vurugu za Oktoba 29, mwaka huu kwenye kituo cha polisi cha Kikatiti (mita 500 kutoka barabara kuu ya Arusha - Moshi); Mahak**a ya Mwanzo ya Maji ya Chai (km. 3 kutoka barabara hiyo kuu); kituo cha mafuta Total Energies kilichopo Maji ya Chai (kipo barabarani) ambavyo vyote vilichomwa moto ikiwemo kuiba mali kwenye supermarket na kubomoa sefu ya kutunzia fedha.
Waziri Mkuu amesema masuala ya maendeleo ya wilaya ya hiyo k**a vile maji na barabara yamo kwenye Ilani ya CCM na kwenye ahadi za Mheshimiwa Rais lakini yatafanyika endapo tu nchi itakuwa na amani. “Tukichagua vurugu tutakuwa tumechagua kufukuza maendeleo, tukichagua vurugu tutakuwa tumechagua kuongeza umaskini kwa mtu mmoja mmoja," ameonya.
Credit