29/07/2025
Nukta Fakti imefanya uchunguzi kwenye chapisho linalosambaa kwenye mitandao ya kijamii hususan Facebok linalosambaza taarifa zinazodai kuwa Maria Sarungi amechapisha chapisho linalomshutumu Makamu Mwenyekiti wa Chadema kukivunja chama hicho kwa mikono yake mwenyewe na kubaini kuwa taarifa hiyo si ya kweli.
Uchunguzi umebaini kuwa chapisho hilo ni feki, halijachapishwa na Mwananchi Digital, halipo kwenye kurasa rasmi za chombo hicho cha habari. Aidha aina ya mwandiko (fonts) zilizotumika kwenye chapisho hilo sio unaotumika katika machapisho rasmi ya chombo hicho cha habari.
Pia chapisho la Mtandao wa X lililotumika k**a chanzo cha taarifa, halijachapishwa na halipo kwenye ukurasa rasmi wa Maria Sarungi. Aina ya mwandiko (fonts) na mpangilio (theme) unaoonekana kwenye chapisho sio rasmi unaotumiwa katika mtandao huo.
Na Nukta Fakti