Prosper Tv

Directions Website

Prosper Tv Sports & Entertainment Politics, Lifestyle and Comedy Channel, House of sports news and Interviews.

Call/WhatsApp: +25576741223
E-mail: [email protected]

KUMBUKA KUSUBSCRIBE YOUTUBE CHANELI YETU - Prosper Tv

Wachezaji wa timu ya Taifa ya Uganda, Uganda Cranes, walioshiriki kampeni ya kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrik...
25/09/2026

Wachezaji wa timu ya Taifa ya Uganda, Uganda Cranes, walioshiriki kampeni ya kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025, wameahidiwa bonasi ya hadi Dola 10,000 za Marekani, sawa na takribani Shilingi milioni 26, kwa kila mchezaji.

Bonasi hiyo itatolewa kwa kuzingatia uwiano wa idadi ya mechi ambazo kila mchezaji alishiriki katika kampeni hiyo ya kufuzu AFCON 2025.

Rais wa Shirikisho la Soka Uganda (FUFA), Moses Magogo, amethibitisha kuwa mpango huo ni sehemu ya hatua za kuboresha maslahi ya wachezaji wa timu ya Taifa, huku akieleza kuwa FUFA imeweka mkazo katika kuboresha mazingira ya maandalizi na ustawi wa Uganda Cranes.

Mbali na bonasi hiyo, FUFA imeweka utaratibu wa kuhakikisha Uganda Cranes inatumia hoteli za nyota tano wakati wa kambi nchini Uganda au nje ya nchi, pale ambapo mazingira yanaruhusu.

Aidha, wachezaji wanaocheza soka nje ya Uganda watanufaika na usafiri wa ndege wa daraja la biashara wanapoitwa kujiunga na timu ya Taifa.

Kwa ratiba zinazohusisha mechi mbili za ugenini au safari zinazofanyika ndani ya muda mfupi, FUFA imesema itatumia ndege za kukodi pale itakapohitajika, hatua inayolenga kupunguza muda wa safari na kuwawezesha wachezaji kujiandaa vizuri kwa michezo.

Shirikisho hilo pia limeahidi kuipatia Uganda Cranes basi jipya la timu, sambamba na kuboresha mfumo wa posho na bonasi mbalimbali kwa wachezaji.

Hatua hizo zinaelezwa kuwa sehemu ya mpango mpana wa FUFA wa kuboresha mazingira ya timu ya Taifa na kuongeza ustawi wa wachezaji wanaoiwakilisha Uganda katika mashindano ya kimataifa.

Follow Prosper Tv

Msemaji wa Simba SC, Ahmed Ally, amesema hadi sasa Uwanja wa Meja Jenerali Isamuyo ndio uliopangwa kuwa mwenyeji wa mche...
24/09/2026

Msemaji wa Simba SC, Ahmed Ally, amesema hadi sasa Uwanja wa Meja Jenerali Isamuyo ndio uliopangwa kuwa mwenyeji wa mchezo wa Derby, huku akisisitiza kuwa klabu hiyo bado haijafikia uamuzi wa kubadilisha uwanja huo.

Ahmed Ally amesema uwezekano wa kufanyika kwa mabadiliko bado upo endapo uamuzi mwingine utaibuka, lakini kwa sasa mpango uliopo ni kutumia Uwanja wa Meja Jenerali Isamuyo.

“Mpaka muda huu, uwanja wa Derby ni Meja Jenerali Isamuyo. Huenda maamuzi tofauti yakatokea, lakini bado hatujaafiki kufanya hivyo,” amesema Ahmed Ally.

Akizungumzia suala la wapinzani wao kutumia Uwanja wa Uhuru, Ahmed Ally amesema jambo hilo halileti hofu kwa Simba, akitoa mfano wa mchezo uliopita dhidi ya Azam FC uliochezwa katika Uwanja wa Azam Complex, ambapo Simba ilipata ushindi wa mabao 2-0.

“Kuhusu wao kuchezea Uwanja wa Uhuru, hiyo haina madhara hata kidogo kwetu, kwa sababu hata Uwanja wa Azam Complex waliutumia na bado tukashinda dhidi ya Azam chuma 2-0,” amesema.

Kwa sasa, Uwanja wa Meja Jenerali Isamuyo unaendelea kuwa sehemu iliyopangwa kutumika kwa mchezo huo, huku uamuzi wa mwisho kuhusu uwanja ukisubiriwa endapo kutakuwa na mabadiliko.

Follow Prosper Tv

Beki wa Simba SC, Rushine De Reuck, amesema mashabiki wa soka nchini Tanzania wana mapenzi makubwa na mchezo huo pamoja ...
23/09/2026

Beki wa Simba SC, Rushine De Reuck, amesema mashabiki wa soka nchini Tanzania wana mapenzi makubwa na mchezo huo pamoja na kuweka presha kubwa kwa wachezaji, tofauti na alichokizoea nchini Afrika Kusini.

Akizungumza katika kipindi cha lMicro Moments of Self-Love kinachoongozwa na Fatema Dewji, De Reuck amesema kiwango cha mapenzi na matarajio ya mashabiki wa Tanzania ni kikubwa zaidi, hali ambayo imekuwa tofauti na mazingira aliyoyazoea katika soka la Afrika Kusini.

Hata hivyo, beki huyo amesema ameamua kuichukulia presha hiyo kwa mtazamo chanya badala ya kuiruhusu kumuathiri kisaikolojia.

“Kwangu mimi presha ni fursa na bahati (privilege). Inapoanza kujisikia k**a mzigo, basi itachukua nguvu zako nyingi sana,” alisema De Reuck.

De Reuck amesema matarajio makubwa kutoka kwa mashabiki yanampa wajibu na hamasa ya kuhakikisha anatoa mchango mkubwa kila anapokuwa uwanjani.

Aidha, amesema kuona furaha ya mashabiki wa Simba baada ya timu kupata ushindi humpa nguvu zaidi na kumfanya atambue thamani ya kuitumikia klabu hiyo yenye mashabiki wenye shauku kubwa.

Follow Prosper Tv

Afisa Habari na Mawasiliano wa TRA United, Christina Mwagala, ameweka wazi azma ya klabu hiyo kuifunga Young Africans (Y...
21/09/2026

Afisa Habari na Mawasiliano wa TRA United, Christina Mwagala, ameweka wazi azma ya klabu hiyo kuifunga Young Africans (Yanga SC) na kuwa timu itakayohitimisha kibarua cha kocha mkuu wa Yanga, Manqoba Mngqithi.

Mwagala ametoa kauli hiyo kupitia Kipenga, akieleza kuwa TRA United inalenga kupata ushindi dhidi ya Yanga katika mchezo wao ujao, huku akisisitiza kuwa klabu hiyo inataka kuwa chanzo cha kuondoka kwa kocha huyo badala ya Simba SC.

“Ninawaomba Yanga wamfukuze kocha wao baada ya Dabi ya Kariakoo wakikutana na sisi. Tunamtaka kocha Manqoba. Tunataka tuwafunge Yanga, wafukuze kocha. Kwa hiyo, tunataka afukuzwe baada ya kucheza na sisi. Sisi ndio tuharibu kibarua chake na sio Simba SC,” amesema Mwagala.

Kauli hiyo imekuja wakati ambapo Manqoba Mngqithi akiendelea na majukumu yake ya kuiongoza Yanga, huku mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya Simba SC ukiwa miongoni mwa mechi zinazotajwa kuwa na umuhimu mkubwa katika msimu wa Ligi Kuu ya NBC.

Follow Prosper Tv

Klabu ya Simba SC imevunjwa kambi na kuwapa wachezaji mapumziko kufuatia kusimama kwa shughuli za ligi kutokana na kalen...
19/09/2026

Klabu ya Simba SC imevunjwa kambi na kuwapa wachezaji mapumziko kufuatia kusimama kwa shughuli za ligi kutokana na kalenda ya FIFA, ikiwa imeacha alama ya kuvutia katika michezo yake ya mwanzo ya msimu wa Ligi Kuu ya NBC.

Simba imeingia kwenye mapumziko hayo ikiwa imeshinda michezo yake sita ya mwanzo ya ligi, ikiwemo ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Azam FC katika mchezo uliochezwa Septemba 16, 2026, kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Ushindi huo umeendeleza mwenendo mzuri wa kikosi hicho katika hatua za mwanzo za msimu, huku Simba pia ikiwa imefanikiwa kusonga mbele katika Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuifunga Mighty Wanderers ya Malawi kwa jumla ya mabao 7-1 katika michezo miwili ya raundi ya awali.

Mapumziko hayo yanatarajiwa kuwapa wachezaji nafasi ya kupumzika na kurejea wakiwa tayari kuendelea na majukumu ya klabu baada ya dirisha la FIFA kufungwa.

Simba sasa inaelekeza nguvu zake kwenye maandalizi ya ratiba inayofuata, huku mchezo unaosubiriwa kwa hamu ukiwa ni Dar es Salaam Derby dhidi ya Yanga SC, unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 10, 2026, katika Uwanja wa Uhuru.

Kwa sasa, Simba inaingia kwenye kipindi hicho cha mapumziko ikiwa na rekodi ya ushindi wa asilimia 100 katika michezo yake sita ya mwanzo ya ligi, jambo linaloweka msingi wa kuvutia kuelekea mwendelezo wa msimu.

Follow Prosper Tv

Msemaji wa Young Africans (Yanga), Ally Kamwe, amesema klabu hiyo haijawasilisha rufaa kupinga kadi nyekundu aliyoonyesh...
18/09/2026

Msemaji wa Young Africans (Yanga), Ally Kamwe, amesema klabu hiyo haijawasilisha rufaa kupinga kadi nyekundu aliyoonyeshwa kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Geita Gold FC.

Kamwe amesema licha ya kukosekana kwa Aziz Ki katika mchezo huo, Yanga ina imani na uwezo wa Erick Mwijage kuziba nafasi yake, huku akimzungumzia kwa namna ya kipekee mchezaji huyo kabla ya Kariakoo Derby dhidi ya Simba.

Kwa mujibu wa Kamwe, Aziz Ki amekuwa na mchango mkubwa katika michezo ya Kariakoo Derby katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, akimtaja k**a “King wa Kariakoo Derby” kutokana na uwezo wake wa kuamua matokeo katika baadhi ya michezo dhidi ya Simba.

Akizungumza kuhusu Mwijage, Kamwe amedai kuwa mchezaji huyo ana uwezo mkubwa na amemfananisha na kiungo wa Barcelona na timu ya Taifa ya Hispania, Pedri, huku akiihoji Simba kuhusu uwezo wake wa kumdhibiti katika mchezo huo.

Follow Prosper Tv

Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Burkina Faso, Amir Abdou, amemwacha kiungo mshambuliaji Stéphane Aziz Ki kwenye kikosi ch...
17/09/2026

Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Burkina Faso, Amir Abdou, amemwacha kiungo mshambuliaji Stéphane Aziz Ki kwenye kikosi cha wachezaji 25 kitakachotumika katika michezo ijayo ya kufuzu AFCON 2027 dhidi ya Benin na Jamhuri ya Afrika ya Kati, pamoja na mchezo wa kirafiki dhidi ya Argentina.

Abdou ametangaza kikosi hicho Alhamisi, Septemba 17, 2026, huku Aziz Ki akiwa miongoni mwa majina yaliyokosekana kwenye orodha hiyo. Taarifa kutoka vyombo vya habari vya Burkina Faso, ikiwemo Burkina24 na Quotidien Sidwaya, zimethibitisha kutokuwemo kwa nyota huyo, lakini hazijaeleza sababu maalumu iliyotolewa na kocha kuhusu kutomjumuisha.

Uamuzi huo unakuja katika kipindi ambacho Abdou anaonekana kufanya mabadiliko kadhaa kwenye kikosi chake, akiwemo kuwaingiza baadhi ya wachezaji wapya k**a Ismaël Maïga, Rachid Kouda na Axel Taonsa, huku jumla ya mabadiliko 11 yakifanyika ikilinganishwa na kikosi chake kilichotumika kwenye michezo ya kirafiki dhidi ya Belarus na Russia.

Aziz Ki si mgeni kwenye kikosi cha Burkina Faso. Kiungo huyo amekuwa sehemu ya timu hiyo katika vipindi mbalimbali na aliitwa pia kwenye kikosi cha Taifa mwaka 2025, huku rekodi za mashindano zikionyesha kuwa amekuwa akitumika katika kikosi cha taifa katika miaka ya karibuni.

Kinachofanya kutokuwepo kwake kuibua maswali ni kwamba kocha huyo katika mkutano wake wa waandishi wa habari leo alieleza kwa uwazi sababu za kuwaacha baadhi ya wachezaji wengine.

Kwa mfano, Abdou alieleza kwamba Bertrand Traoré hajaingizwa kwa sababu bado hajapata muda wa kutosha wa kucheza tangu kujiunga na Wolverhampton, huku akisisitiza kuwa anahitaji kwanza kurejesha kiwango na mfululizo wa michezo.

Pia, kuhusu Mohamed Zongo, kocha huyo alisema ukosefu wa muda wa kucheza katika klabu ndiyo sababu kuu inayomfanya asimuite kwenye kikosi cha wakubwa.

Kwa upande mwingine, katika suala la Cyriaque Irié, Abdou alitoa maelezo ya kina zaidi kuhusu uamuzi wake, akisisitiza nidhamu na umuhimu wa wachezaji kuhudhuria kambi ya Taifa kwa muda wote waliopangiwa.

Hakuna kauli ya Amir Abdou inayosema Aziz Ki ameondolewa kutokana na utovu wa nidhamu, majeraha, kiwango duni, mgogoro na kocha au sababu nyingine maalumu.

Kwa hiyo, kwa taarifa iliyo sahihi kwa sasa, kinachoweza kusemwa ni kwamba Aziz Ki ameachwa nje kutokana na uchaguzi wa kocha katika kikosi kipya, huku sababu mahsusi ya kutomjumuisha ikiwa haijawekwa wazi hadharani.

Burkina Faso itaanza kampeni yake ya kufuzu AFCON 2027 kwa kuikabili Benin Septemba 25 mjini Ouagadougou, kabla ya kucheza na Jamhuri ya Afrika ya Kati Septemba 28, huku mchezo wa kirafiki dhidi ya Argentina ukipangwa Oktoba 3 mjini Buenos Aires.

Follow Prosper Tv

Klabu ya Young Africans (Yanga SC) imeandaa utaratibu wa kuwasilisha rufaa rasmi kupinga kadi nyekundu ya moja kwa moja ...
17/09/2026

Klabu ya Young Africans (Yanga SC) imeandaa utaratibu wa kuwasilisha rufaa rasmi kupinga kadi nyekundu ya moja kwa moja aliyoonyeshwa kiungo mshambuliaji wake, Stephane Aziz Ki, katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Geita Gold FC.

Uongozi wa Yanga unaamini kuwa tukio lililosababisha Aziz Ki kupewa kadi hiyo halikustahili adhabu ya kadi nyekundu ya moja kwa moja, huku ukieleza kuwa maamuzi ya mwamuzi hayakuakisi mazingira halisi ya tukio lililotokea uwanjani.

Rufaa hiyo inatarajiwa kuwasilishwa kwa Kamati husika ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa ajili ya kupitia upya tukio hilo na adhabu iliyotolewa.

Iwapo rufaa hiyo itakubaliwa na adhabu hiyo ikaondolewa au kupunguzwa, Aziz Ki ataweza kuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kitakachokutana na Simba SC katika mchezo wa Kariakoo Derby baada ya mapumziko ya michezo ya kimataifa.

Follow Prosper Tv

Clatous Chama anaendelea kuonyesha sababu ya kuwa miongoni mwa wachezaji wanaotegemewa katika kikosi cha Simba SC, akian...
16/09/2026

Clatous Chama anaendelea kuonyesha sababu ya kuwa miongoni mwa wachezaji wanaotegemewa katika kikosi cha Simba SC, akianza msimu mpya kwa kiwango kinachomfanya kuwa sehemu muhimu ya mipango ya timu hiyo katika mashindano ya ndani na kimataifa.

Kiungo huyo wa Zambia amekuwa na mchango mkubwa katika mwanzo mzuri wa Simba, akionyesha uwezo wa kutengeneza nafasi, kuchezesha timu na pia kutafuta nafasi ya kufunga. Katika Ligi Kuu msimu huu, Chama tayari ana mabao matatu, huku Simba ikiwa imecheza mechi sita bila kupoteza.

Kiwango chake kimeonekana pia katika mashindano ya kimataifa, ambapo alifunga katika ushindi wa Simba wa mabao 6-1 dhidi ya Mighty Wanderers ya Malawi katika mchezo wa marudiano wa raundi ya kwanza ya kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika. Ushindi huo uliisaidia Simba kusonga mbele kwa jumla ya mabao 7-1.

Katika mchezo wa Mzizima Derby dhidi ya Azam FC uliochezwa leo, Chama aliongeza jina lake kwenye orodha ya wafungaji baada ya kufunga bao la pili la Simba dakika ya 68, likiwa bao lililosaidia kukamilisha ushindi wa 2-0 na kuipa timu yake pointi zote tatu.

Kinachomtofautisha Chama katika mwanzo huu wa msimu si mabao pekee, bali pia namna anavyohusika katika ujenzi wa mashambulizi na kutoa suluhisho katika maeneo ya mwisho ya uwanja. Uwezo wake wa kutumia uzoefu, utulivu na ubunifu unapokuwa na mpira umemfanya kuwa mmoja wa wachezaji wanaovuta macho katika kikosi cha Simba.

Kadiri msimu unavyoendelea, Chama anaonekana kurejea kwenye nafasi ambayo mashabiki wa Simba wameizoea—kuwa mchezaji anayeweza kubadilisha mwelekeo wa mchezo kwa ubunifu wake na uwezo wa kutumia nafasi.

Kwa mwanzo huu, jina la Chama linaendelea kuwa miongoni mwa majina yanayopewa uzito katika safari ya Simba kwenye msimu wa 2026/27.

Follow Prosper Tv

Simba SC imeanza vyema msimu mpya wa Ligi Kuu ya Tanzania baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Azam FC kati...
16/09/2026

Simba SC imeanza vyema msimu mpya wa Ligi Kuu ya Tanzania baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Mzizima Derby uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Mchezo huo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka ulianza kwa ushindani mkubwa, huku timu zote zikijaribu kutengeneza nafasi za kufunga. Hata hivyo, kipindi cha kwanza kilimalizika bila timu yoyote kupata bao.

Simba ilirejea kipindi cha pili ikiwa na kasi zaidi na juhudi zake zilizaa matunda dakika ya 59, ambapo Rushine De Reuck aliifungia timu hiyo bao la kwanza na kuifanya Simba kuanza kuongoza kwa bao 1-0.

Azam FC ilijaribu kurejea mchezoni na kusaka bao la kusawazisha, lakini Simba iliendelea kuwa imara na kuongeza presha kwenye eneo la hatari la wapinzani wake.

Dakika ya 68, Clatous Chama aliifungia Simba bao la pili na kuifanya timu hiyo kuongoza kwa mabao 2-0. Azam ilijaribu kupunguza pengo katika dakika zilizobaki, lakini haikuweza kupata bao.

Hadi mwamuzi alipuliza filimbi ya mwisho, Simba iliondoka na ushindi wa mabao 2-0 na pointi zote tatu, katika mchezo mwingine muhimu wa Ligi Kuu Tanzania.

Ushindi huo unaendeleza mwenendo mzuri wa Simba dhidi ya Azam baada ya timu hiyo pia kuifunga Azam katika fainali ya CRDB Bank Federation Cup iliyochezwa Julai mwaka huu.

Follow Prosper Tv

Address

Dar Es Salaam
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Prosper Tv posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share

Category