
26/02/2025
Kituo cha Vijana cha Don Bosco Upanga Dar Es Salaam kwa namna ya kipekee kinapenda kukuhalika Ewe Kijana Mkristo Mkatoliki kutoka maeneo mbalimbali Kushiriki Safari Ya Hija Ya Kipekee kabisa iliyopewa jina la *"PILGRIM OF HOPE, GRATEFUL TO MOTHER MARY (MAHUJAJI WA MATUMAINI, SHUKRANI KWA MAMA MARIA)"*
IKiwa umewai kwenda Kibeho, Ikiwa umekuwa ukisali Rozari Takatifu, Ikiwa ni mfuasi mzuri wa Mama Maria huu ndo wakati wako wa Kwenda Kumshukuru Mama Maria wa Kibeho kwa kusema Asante kwa yale mema ambayo amekutendea kupitia maombi ambayo umekuwa ukimuomba yeye atufikishie kwa Mwanawe Yesu Kristo, Usipange kukosa ni Safari ya Kipekee mno na yenye baraka mno na ukizingatia tuko katika Mwaka wa Jubilei ya Miaka 2025 ya Kanisa Tukimsheherekea Bwana wetu Yesu Kristo
Ni kuanzia Septemba 01-10, 2025 na Safari itaanzia Kituo cha Vijana Donbosco Upanga Dar Es Salaam
Tutakuwa na Vituo vya kuchukua watu katika Maeneo yafuatayo
1.Morogoro Mjini
02. Dodoma
3. Kanisa Kuu Katoliki Jimbo la Singida
4. Kanisa Kuu Jimbo Katoliki la Kahama
5. Njia Panda ya Bukoba na Ngara
Wahujaji watapata Fursa pia ya Kutembelea
01. Ubalozi wa Tanzania Kigali
02. Genocide Memorial Center
03. Kituo cha Watoto Yatima cha Mother Theresa Kigali
(Wahujaji mnahimizwa kubeba majitoleo kwa ajili ya watoto wahitaji, Hii ni Sehemu ya Hija yetu TAKATIFU)
Gharama za Safari kwa Ujumla ni Tsh.570,000/= zikijumuisha mambo yafuatayo
01. Usafiri wa Kwenda na Kurudi
02.Chakula na malazi tuwapo Kigali na Kibeho
03. Tisheti, Kofia(wanaume), Kikoi wanawake pamoja na Chupa ya Kisasa inayoweza kutunza vitu vya moto au baridi kwa muda mrefu
*Tuwapo njiani Kila Mhujaji atalazimika kutumia mfuko wake binafsi*
Aidha unaweza kufanya malipo haya kupitia MKOMBOZI BANK ACC NO. 00124319664901(SAVIO PILGRIMAGE SERVICE)
UNAWEZA KUWASILIANA NASI KUPITIA NAMBA ZIFUATAZO
01.Pd. Valerian Kway SDB
+255769938662
02. Stadius Alistides
+255768972212
Vijana wote Mnakaribishwa sana, Twendeni Tukamshukuru Mama Maria
*Urubyir