12/01/2026
Kocha wa Klabu ya Azam Flotent Ibenge akizungumuza na waandishi wa habari kuelekea Mchezo wa kesho kati ya Azam FC dhidi ya Yanga Amesema kuwa
"Tunajua Yanga ndiyo timu bora zaidi Tanzania kwa sasa, lakini sisi tutakuwa bora zaidi yao"
Kocha wa Azam FC, Florent Ibenge amesema wako tayari kwa fainali na wamejiandaa kuwa bora zaidi uwanjani kuliko wapinzani wao.
Ibenge amesema wachezaji wote wako tayari kwa mechi na wote anawaamini.
Nawaamini wachezaji wangu wote, Napenda kila mchezaji acheze, Sipendi kuwa na timu inayomtegemea mchezaji mmoja, kwamba asipokuwepo yeye, basi timu nzima inakufa.
Fainali ni kesho Januari 13 saa 10:30 jioni, Azam FC vs Yanga,SC, Gombani Pemba.