AWR Tanzania

AWR Tanzania Sikiliza Sauti ya Matumaini AWR Tanzania (Morning Star Radio zamani). ujumbe wa matumaini kwa watu wote.

Njozi za kuanzishwa kwa Radio hii, zilianza mnamo miaka ya tisini, ambapo mwaka 2000 viongozi wa makanisa ya Dar es salaam walikutana na kuweka mkakati madhubuti ya kuanzisha radio,kwa wakati huo ikijulikana k**a TAWR (Tanzania Adventist World Radio). Mwaka 2001, uchunguzi yakinifu wa kuanzishwa kwa Kituo hiki ulianza chini ya kitengo cha mawasiliano cha Makao makuu ya Kanisa Tanzania kijulikanach

o k**a TAMC (Tanzania Adventist Media Center). Baada ya mikakati madhubuti kukamilika, ujenzi wa kituo cha radio ulianza rasmi mnamo mwaka 2002, katika eneo la Mikocheni B, jijini Dar es salaam, ujenzi ambao uliendelea na kukamilika kwa sehemu kubwa mnamo mwaka 2003. Mnamo tarehe moja mwezi wa kumi mwaka 2003, kituo kilirusha matangazo yake kwa mara ya kwanza k**a
majaribio, kwa kutumia mtambo wa kurushia matangazo wenye uwezo wa watt 500, na tangu hapo safari ya
matangazo kusikika hewani iliendelea! Mwezi wa kumi na moja mwaka wa 2003, kituo kilifunguliwa rasmi na Mgeni aliyehudhuria
shughuli hiyo, Mchungaji Jan Paulsen, akija k**a Rais wa kanisa la Waadventista wasabato
Duniani, akitoea Nchini Marekani ambako ndiko makao makuu ya Kanisa Duniani, yalipo. Majuma mawili baada ya kufunguliwa rasmi kwa kituo, Mtambo wa kurushia matangazo
uliokuwa umefungwa mikocheni B mahali zilipo studio, ulishindwa kufanya kazi
kutokana na hitilafu iliyosababishwa na umeme, tatizo lililojitokeza baada ya mvua kali kunyesha. Jitihada za kujaribu kuirejesha katika hali ya kuendelea kufanya kazi zilishindikana,
jambo lililopelekea muingiliano na vyombo vingine vya habari, na kituo kufungwa kwa muda
na tume ya mawasilianona, ili kutoa nafasi ya kufanyika kwa marekebisho. Kituo kilirejea
tena katika hali yake na kuendelea na matangazo baada ya miaka miwili baadae. Mwaka 2005 mwezi wa tano,vifaa vipya vya kurushia matangazo viliagizwa ili kurejesha matangazo tena. Uagizaji huo
ulichukua muda wa miezi mitatu, na mwezi wa nane vifaa viliwasili na ufungaji ukaanza mara moja, wakati huu mtambo
ukiwa umehamishiwa eneo la kisarawe, mkoa wa Pwani. Baada ya ufungaji mtambo kukamilika, mnamo mwezi wa nane mwaka 2005, urushaji wa matangazo ya majaribio
ulianza mara moja, ambapo majaribio hayo yalichukua takribani mwezi mmoja, hadi mnamo mwezi wa tisa! Ilipofika tarehe 26, mwezi wa tano mwaka 2006, saa 11:00 jioni, kituo kilirusha
matangazo moja kwa moja kwa mara ya kwanza, baada ya matangazo ya majaribio
kukamilika! Tangu hapo, Morning Star Radio imeendelea kurusha matangazo yake hadi hivi sasa,
ambapo watu mbali mbali wamekuwa wakibarikiwa sana na matangazo haya, na kwa
hakika kituo hiki kimekuwa ni mbaraka sana kwa ma elfu ya wakaazi wa Tanzania
na dunia kwa ujumla ambapo matangazo
ya Redio hii yanasikika!

Ukimweka Mungu mbele ya maisha yako, hakuna kitu kitakachokutikisa. Uwepo wake ni uthibitisho wa amani, nguvu na uthabit...
02/10/2025

Ukimweka Mungu mbele ya maisha yako, hakuna kitu kitakachokutikisa. Uwepo wake ni uthibitisho wa amani, nguvu na uthabiti wako kila siku. 🙏💪

🙏🏽 Mungu yupo karibu sana na wale wanaomwita kwa uaminifu.Leo usisite kumwita, kwa maana Yeye husikia!
01/10/2025

🙏🏽 Mungu yupo karibu sana na wale wanaomwita kwa uaminifu.
Leo usisite kumwita, kwa maana Yeye husikia!

Kila siku inaanza salama tunapomkabidhi Bwana maisha yetu. Neema yake hutubeba, mkono wake hututia nguvu, na wokovu wake...
01/10/2025

Kila siku inaanza salama tunapomkabidhi Bwana maisha yetu. Neema yake hutubeba, mkono wake hututia nguvu, na wokovu wake hutulinda hata katikati ya taabu. 🙏✨

Wakati dhoruba za maisha zinapokuzunguka, Mungu hubaki kuwa ngome thabiti ya usalama na faraja. Kimbilia kwake, na utapa...
30/09/2025

Wakati dhoruba za maisha zinapokuzunguka, Mungu hubaki kuwa ngome thabiti ya usalama na faraja. Kimbilia kwake, na utapata amani isiyoondoshwa. 🙏✨

Hakuna jaribu lililo kubwa kupita uwezo wako kwa sababu Mungu anakuweka salama. Yeye hushika neno lake, na kila changamo...
29/09/2025

Hakuna jaribu lililo kubwa kupita uwezo wako kwa sababu Mungu anakuweka salama. Yeye hushika neno lake, na kila changamoto huambatana na njia ya ushindi. Usiogope, wewe si peke yako. ✨💪

Nguvu za dunia hupita, lakini jina la Bwana ndilo ngome imara na ushindi wa kweli. Mtegemee Yeye, na hutayumbishwa kamwe...
28/09/2025

Nguvu za dunia hupita, lakini jina la Bwana ndilo ngome imara na ushindi wa kweli. Mtegemee Yeye, na hutayumbishwa kamwe. 🙏🔥

Katika udhaifu wako, nguvu ya Mungu huonekana kwa ukuu. Usijione dhaifu, maana neema yake inakufunika na kukupa uwezo wa...
27/09/2025

Katika udhaifu wako, nguvu ya Mungu huonekana kwa ukuu. Usijione dhaifu, maana neema yake inakufunika na kukupa uwezo wa kushinda kila jaribu. 🙏✨

Wewe si peke yako katika safari ya maisha. Mungu mwenye nguvu anakushika mkono, anakutia moyo na kukuahidi msaada. Simam...
26/09/2025

Wewe si peke yako katika safari ya maisha. Mungu mwenye nguvu anakushika mkono, anakutia moyo na kukuahidi msaada. Simama imara, msaada wake haushindwi. 🙏✨

25/09/2025

NENO LA LEO - (OCTOBER 2025)

Kanisa la Waadventista wa Sabato Kimanga Dar es salaam,Tunakukaribisha kwenye Mkutano wa injili kwa njia ya redio,Naam tunakuletea ujumbe wa Neno la Mungu Mada kuu ni Kwa neno lako Mahubiri haya yanakujia kupitia Awr Tanzania,Tarehe 01-31Mwezi wa kumi 2025 Jumatatu hadi ijumaa saa tano na robo asubuhi hadi Sita mchana.Hakika ni Dakika 45 za Baraka.Hapa utakutana na Yesu kupitia kwa Muhubiri Mchungaji Nashon Lameck kutoka mtaa wa Kimanga Dar es salaam.Kwa mawasiliano zaidi kuhusu ubatizo,maombi,ushauri na Maswali wasiliana na mhubiri wetu kwa namba hii 0715338600.
Usipange kukosa na Nyote Mnakaribishwa.

Neno la Mungu ni mwanga unaoondoa giza la mashaka na hofu. Ukilifuata, hautapotea njiani, bali utaongozwa kwenye ukweli ...
25/09/2025

Neno la Mungu ni mwanga unaoondoa giza la mashaka na hofu. Ukilifuata, hautapotea njiani, bali utaongozwa kwenye ukweli na uzima wa milele. 🙏📖

10/08/2025

Hodi hodi Mtwara!(AWR TZ)
Mtwara kuchere.
Hivi karibuni tutaanza uzalishaji na matangazo live kutoka studio zetu mpya za kisasa za Mtwara (AWR TANZANIA).Ewe mdau na msikilizaji na wakazi wote wa Mtwara karibuni tufanye kazi pamoja.
AWR TAANZANIA - SAUTI YA MATUMAINI

"Ushindi hauji kwa nguvu zako, bali kwa Roho wa Mungu. Jipe moyo — si wewe unayetenda, ni Mungu aliye ndani yako!"      ...
06/08/2025

"Ushindi hauji kwa nguvu zako, bali kwa Roho wa Mungu. Jipe moyo — si wewe unayetenda, ni Mungu aliye ndani yako!"

Address

P. O. BOX 77170
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when AWR Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share