25/10/2025                                                                            
                                    
                                                                            
                                            Ulimwengu wa mitandao ya kijamii uko katika simanzi baada ya kifo cha nyota chipukizi wa TikTok, Emman Atienza, raia wa Ufilipino, ambaye ameripotiwa kufariki dunia akiwa na umri wa miaka 19 tu.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyombo vya habari vya kimataifa k**a People na New York Post, Emman alifariki nyumbani kwake mjini Los Angeles, Marekani, kutokana na kujitoa uhai (su***de), tukio hilo limezua majonzi makubwa, hasa kwa mashabiki wake waliokuwa wakifuatilia video zake zenye ucheshi na ujumbe wa kuhamasisha vijana.
Emman, ambaye alikuwa pia mtoto wa mtangazaji maarufu wa televisheni Kim Atienza, alikuwa akipendwa kwa tabia yake ya unyenyekevu na ubunifu.
Familia yake imethibitisha taarifa za kifo chake na kuomba mashabiki kuheshimu faragha yao wakati huu mgumu wa maombolezo.
Mitandao ya kijamii imefurika jumbe za rambirambi, wengi wakimkumbuka Emman k**a kijana mwenye kipaji, aliyejua kuleta tabasamu kwa mamilioni ya watu duniani kupitia TikTok