TZ Trends

TZ Trends Official Page for TZ Trends Media
For Reliable News, this is the perfect place

02/12/2025

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu akizungumza na Wazee wa Dar es salaam siku ya leo

Rais Samia ameawauliza Watu walifanya vurugu Oktoba 29 kosa la Serikali ya awamu ya sita ni lipi kwani Serikali imehakikisha imefanya kila kitu ili kuhakikisha Watanzania wanapata huduma zote muhimu

Msanii na Mtangazaji kutoka clouds media group  ametangazwa na shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira  kuwa balozi wa ...
02/12/2025

Msanii na Mtangazaji kutoka clouds media group ametangazwa na shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira kuwa balozi wa hiari wa Kwanza kutetea urejeshwaji wa mifumo ya ikolojia (ecosystem restoration).

Hii ni nafasi ya kipekee sio tu kwa Frida Amani Bali pia k**a nchi katika kuendelea kuhamasisha uhifadhi na utunzaji wa mazingira.

Frida Amani kupitia page yake ameshukuru na kupokea rasmi uteuzi huo kwa kutoa Rai katika kuhamasisha vijana katika utunzaji wa mazingira

"Ninayo furaha kubwa kupata heshima hii, na ninakubali rasmi uteuzi huu k**a Balozi wa kwanza wa UNEP katika kusimamia Urejeshwaji wa Mifumo ya Ikolojia. Heshima hii ni kubwa kuliko ninavyoweza kueleza. Mazingira yamekuwa msingi wa ustawi wetu na kuyaona yakidhoofika kumezidi kuniaminisha kuwa kila mmoja wetu, mimi nikiwemo, tuna jukumu la kurejesha tunachopoteza.

Ninaishukuru UNEP kwa kuniamini na kunipa nafasi hii muhimu, na kwa kutambua nguvu ya sanaa, utamaduni na vijana katika kuleta mabadiliko ya kimazingira."

Askari wa Jeshi la Magereza mwenye umri wa miaka 31 (jina limehifadhiwa) anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Shinyang...
02/12/2025

Askari wa Jeshi la Magereza mwenye umri wa miaka 31 (jina limehifadhiwa) anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga akituhumiwa kumuua mpenzi wake, Bitie Chacha (25), mwalimu wa Shule ya Msingi, mkazi wa Bugweto A, Kata ya Ibadakuli, Manispaa ya Shinyanga.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi Bitie aliuawa Novemba 30 majira ya saa moja usiku kwa kuchomwa na kisu sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo mapajani, shingoni na kichwani.

Kabla ya kuhitilafiana Bitie alikuwa akiishi na ofisa magereza huyo k**a wapenzi lakini ilitokea kutokuelewana kati yao ndipo mtuhumiwa akamshambulia mwalimu huyo.

Kwa mujibu wa rafiki yake na marehemu, ugomvi wa wapenzi hao ulianzia baa baada ya askari huyo kuchukua simu ya mkononi ya marehemu na kusoma ujumbe mfupi.

Source; East Africa Tv

02/12/2025

Binti mwenye umri wa miaka (18) jina lake (limehifadhiwa) mkazi wa wilaya ya urambo huko mkoani Tabora ambaye aliripotiwa kuchomwa sindano ya usingizi na kisha kubakwa na daktari wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya Urambo ameeleza kile alichodai kufanyiwa pindi akiwa hospitalini hapo.

Hata hivyo licha ya maelezo ya binti huyo ambae ni mke wa mtu,mbele ya k**ati ya ulinzi na usalama mkoa wa Tabora afisa tabibu msaidizi wa hospitali ya wilaya ya Urambo Juma selemani ambaye anadaiwa kufanya tukio hilo alikana kuhusika kufanya kitendo hicho zaidi tu ya kumpatia huduma za matibabu kwa changamoto ya uzazi zilizokuwa zikimkabili binti huyo

Mkuu wa mkoa wa Tabora Paul Chacha baada ya kusikiliza pande zote mbili akatoa maagizo ya kumsimamisha kazi mganga mkuu wilaya ya urambo Dkt David Manyama ambaye inadaiwa alikua akilifumbia macho sakata hilo la ubakaji

🎥 E TV

Ameandika  unakubaliana naye??
02/12/2025

Ameandika unakubaliana naye??

01/12/2025

Mchekeshaji kupitia ukurasa wake wa Instagram ame-share video akiwa na Watoto wake wakiwa wanasoma Qurani

Video hiyo imewavutia wengi huku wakimsifia Gladness kwa kuwalea Watoto wake katika misingi ya Dini

Ameandika  "Mechi yetu ya 3 ya hatua ya Makundi tutacheza January 21 2026 dhidi ya Esperance ugeniniKutoka leo hadi Janu...
01/12/2025

Ameandika
"Mechi yetu ya 3 ya hatua ya Makundi tutacheza January 21 2026 dhidi ya Esperance ugenini

Kutoka leo hadi January 21 ni siku zaidi ya 50

Katika siku hizo kikosi chetu kitafanyiwa mabadiliko makubwa ya kiufundi na itakapobidi kuongeza nguvu kwenye dirisha dogo tutafanya hivyo, na tunaamini mabadiliko hayo yataturejesha kwenye makali yetu

Umefika ule wakati wa Simba yetu kuonesha maajabu yake na kuwashangaza watu kwa comeback yetu

Kwa sasa kikosi kinarejea na moja kwa moja tunaanza maandalizi ya michezo yetu ya Ligi kuu

Tukumbuke kuwa katika Ligi tuna mwenendo mzuri hivyo tunapaswa kuwekeza nguvu kubwa tusiteleze

Kila Mwana Simba aelekeze nguvu na akili katika mchezo wetu dhidi ya Mbeya City na Azam Fc"

Unakubalina na Afisa habari wa ?

01/12/2025

Wewe ungepewa nafasi ya kuwarudisha, ungemrudisha nani na kwanini??

01/12/2025

Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amekanusha taarifa zilizo chapishwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa amefiwa na Mama yake mzazi

Kupitia taarifa aliyoitoa kupitia ukurasa wake wa instagram, Msigwa amesema Mama aliyefariki sio mama yake mzazi bali ni mama wa Kazini hivyo amewaomba watu wote waliojiandaa kwenda msibani kijijini kwao ache pia wote walichapisha taarifa hizo potofu wazifute mara moja

"Kwa mara nyingine naomba kuwajulisha kuwa Mama yangu mzazi YUPO HAI, hajafariki dunia k**a ambavyo baadhi ya watu wamechapisha kwenye mitandao yao ya kijamii na kuzua taharuki. Mnasababisha watu waende kijijini msibani wakati msiba haupo. SIO SAWA.

Wote mliochapisha taarifa ya upotoshaji kuhusu Mama yangu mzazi futeni tafadhali. Mama yupo hai na mwenye afya njema" ameandika Msigwa

 kupitia ukurasa wake wa Instagram ame-share picha mpya na Watu wengi wamesifia muonekano wake Watu wengi wameonesha kus...
26/11/2025

kupitia ukurasa wake wa Instagram ame-share picha mpya na Watu wengi wamesifia muonekano wake

Watu wengi wameonesha kushangaa kwani siku zinavyozidi kwenda ndiyo anazidi kuwa mrembo

26/11/2025

Hali ya Watu walio Bet jana

22/11/2025

Baadhi ya Wasanii mbalimbali wakicheza na kwenye usiku wa Kibao kata ulioandlaiwa na Nandy mwenyewe

Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when TZ Trends posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to TZ Trends:

Share