
20/09/2025
DONE DEAL: Ramadhani Masempele ajiunga na East African University VC ya Rwanda!
Ni hatua kubwa kwa Ramadhani Masempele, middle blocker hatari wa Tanzania, aliyekuwa mhimili wa muda mrefu ndani ya Jeshi Stars. Baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa uhodari na nidhamu ya hali ya juu, sasa anavuka mipaka kuanza ukurasa mpya katika ligi ya Rwanda.
Masempele, anayejulikana kwa nguvu, uthabiti na ukuta imara kwenye neti, ameacha alama isiyofutika kwenye volleyball ya Tanzania. Safari yake mpya itamkutanisha na Mtanzania mwenzake, Omary Bure, ambaye tayari anang’ara ndani ya klabu hiyo.
Uhamisho huu ni zaidi ya deal la kawaida ni ishara kuwa wachezaji wa Tanzania wanatambulika kimataifa, na vipaji vyao vina nafasi ya kung’aa katika anga kubwa zaidi.
Mashabiki wa volleyball Tanzania, hii ni historia nyingine inayoandikwa. Ramadhani anapanda ngazi, na sote tupo kushuhudia safari hii.
What a deal. What a journey.
🔥