16/09/2025
Kwanini jersey hii? unapaswa kujua mambo haya machache na muhimu kuhusu toleo hili la jersey.
Ni toleo la zamani lakini maarufu na nzuri kimuonekano hata sasa. Aina hii ya jersey ni maarufu sana nje ya Tanzania.
Yenye rangi ya blue, ndio jersey inayoongoza kwa kununuliwa na watalii na wageni wengi kutoka nje ya Tanzania
Zipo zenye rangi nyeupe, nyeusi na blue, zote zikiwa zinafanana muundo wake.
Aina hii ya jersey hasa ile ya blue ndio jezi za Tanzania zinazopendwa zaidi na watalii, wageni kutoka nje ya Tanzania wanavutiwa zaidi na jersey hizi.
Nyeusi na nyeupe ni adimu kidogo. Na k**a utatembelea maduka na sehemu zinazouzwa bidhaa za kitanzania kwaajiri ya watalii, utagundua ukuu na thamani ya toleo hili la jersey.
Sio kwa watanzania, lakini kwa kila mgeni anayetembelea Tanzania anauwezekano mkubwa sana wa kununua aina hii ya jersey kati aina zote tulizonazo, na sio k**a jersey tu, hii ni nembo yenye thamani.
Lakini kumbuka jambo hili, kule Zanzibar zipo pia ijapokuwa kule kuna mbabe wake huyo nina uhakika, kati ya watalii 10, 6 au zaidi kati yao lazima wanunue jezi hiyo, umeitambua??
Unakubaliana na maelezo haya??