15/09/2025
Rúben Amorim: "Sitobadilisha falsafa yangu. K**a INEOS wanataka kubadilisha falsafa hii, basi wanatakiwa kubadilisha na kocha pia. Tutacheza kwa njia ile ninayoiamini mpaka pale nitakapotaka kubadilisha.
"Project yetu ni ya muda mrefu, kwa hiyo tunatakiwa kurekebisha matatizo yaliyopo..kiukweli, tungefunga angalau magoli mawili leo na tungezuia magoli tuliyoruhusu kufungwa. Mechi iliamuliwa kwa makosa madogo madogo. Manchester City walikuwa na uwezo wa kutumia nafasi walizopata lakini sisi tulishindwa kutumia nafasi zetu.
"Tupo katika hatua ya kitu fulani ili kujaribu kushindana tena dhidi ya hizi timu. Siendi kujilinda mwenyewe, lakini tunatakiwa kufanya vitu bora. Tunatengeneza kitu fulani, lakini bila shaka, tunahitaji kushinda.
"Tunafanya vizuri lakini matokeo hayaonyeshi hili. Nakumbuka klabu yangu ya zamani (Sporting CP), tuliwafunga Manchester City 4-1 bila kuwa na muongozi ule ule au nafasi zile zile k**a tulizozipata leo. Tulikuwa na nafasi nzuri za kufunga magoli.
"K**a ukiangalia magoli, tulikuwa na uwezo wa kuzuia hayo magoli. Huu ndio ulikuwa utofauti mkubwa. Tunatakiwa kufanya vitu bora zaidi, hususani goli la pili. Tulifungwa magoli ambayo tungeweza kuyazuia.
'Sijamuona mchezaji kwenye timu yangu ambaye hajatoa kila kitu uwanjani. Walipambana lakini mengine yote ni juu yangu. Muda mwingine, nachukia pindi ninapoiangalia timu yangu na kuhisi kwamba tunatakiwa kukimbia zaidi, lakini sikuwa na hii hisia leo kwa sababu tulikimbia zaidi."