23/09/2025
Mwanariadha Alphonce Felix Simbu wa Tanzania amepewa mapokezi ya kishujaa katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Septemba 23, 2025 baada ya kuitoa kimasomaso nchi yake katika mashindano ya dunia yaliyofanyika Tokyo, Japan.
Shujaa huyo, alitwaa medali ya dhahabu baada ya kushika nafasi ya kwanza katika mbio za marathon za wanaume zilizofanyika usiku wa kuamkia Septemba 15, 2025 jijini Tokyo.
Simbu alishinda mbio hizo za kilomita 42 ndani ya muda wa 2:09.48, akimaliza mbele ya Amanal Petros wa Ujerumani.