Harakati Media

Harakati Media Kwa habari za kitaifa, kimataifa, biashara, afya, kijamii, michezo na brudani...

Mtatiro: Amani ni Chachu ya Uwekezaji na MaendeleoMkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Julius Mtatiro, amesema utulivu na amani ...
05/06/2026

Mtatiro: Amani ni Chachu ya Uwekezaji na Maendeleo

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Julius Mtatiro, amesema utulivu na amani iliyopo nchini Tanzania imeendelea kuwa kivutio kikubwa kwa wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali kuja kuwekeza katika miradi ya maendeleo yenye manufaa kwa wananchi.

Mtatiro ametoa kauli hiyo baada ya kutembelea mradi wa maji uliotekelezwa katika Kijiji cha Zumve, Kata ya Nyamalogo, Wilaya ya Shinyanga. Ametoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na serikali katika kulinda amani na kudumisha mazingira yanayowezesha maendeleo kupatikana.

Amesema wananchi wanapaswa kuwa raia wema kwa kutekeleza wajibu wao, kufanya kazi kwa bidii, kushirikiana na serikali pamoja na kuhoji kwa njia sahihi ili kuhakikisha serikali inatimiza wajibu wake kwa wananchi.

“Tunapoendelea kuwa wananchi wema, tukifanya kazi kwa bidii, kushirikiana na serikali yetu na kuihoji kwa njia sahihi ili itimize wajibu wake kwa wananchi, huku tukilinda amani yetu, tutaendelea kuvutia wawekezaji wengi zaidi,” amesema Mtatiro.

Aidha, amesisitiza kuwa wawekezaji hawawezi kupeleka mitaji yao katika nchi zenye migogoro na ukosefu wa utulivu, hivyo amani ni rasilimali muhimu inayopaswa kulindwa na kila Mtanzania wakati wote.

“Hawawezi kupeleka uwekezaji kwenye nchi zenye migogoro. Amani ni jambo la msingi sana kwa maendeleo ya taifa letu, hivyo tuilinde mchana na usiku,” amesisitiza.

Mtatiro ameongeza kuwa ulinzi wa amani utaendelea kuvutia miradi mingi ya maendeleo k**a mradi wa maji wa Zumve uliotekelezwa na shirika la Water for Good kwa kushirikiana na RUWASA, hatua itakayochochea ukuaji wa uchumi na kuboresha maisha ya wananchi.

05/06/2026

WASEMAVYO WATEJA WA TANESCO MKOA WA TABORA

Huduma bora za TANESCO zimekuwa chachu ya maendeleo kwa wananchi wa Tabora kupitia upatikanaji wa umeme wa uhakika.




FILAMU YA UCHUNGUZI YAIBUA MJADALA WA AMANI NA MAENDELEO AFRIKAFilamu ya uchunguzi ya mwanahabari David Hundeyin imechoc...
04/06/2026

FILAMU YA UCHUNGUZI YAIBUA MJADALA WA AMANI NA MAENDELEO AFRIKA

Filamu ya uchunguzi ya mwanahabari David Hundeyin imechochea mjadala kuhusu nafasi ya vijana, wajibu wa vyombo vya habari na umuhimu wa kulinda amani katika jamii za Afrika.

Akizungumza baada ya kuonyeshwa kwa filamu hiyo, mwanasiasa mkongwe Hamad Rashid amesema Waafrika wanapaswa kujenga uwezo wa kufanya tafiti na uchunguzi wa kina kuhusu masuala yanayowahusu huku wakitumia mafunzo yaliyopatikana kuimarisha umoja, amani na maendeleo.

Naye mchambuzi wa maendeleo kutoka Zimbabwe, Joshua Maponga, amesisitiza umuhimu wa vyombo vya habari vya ndani kuripoti kwa kina masuala ya jamii na kuwataka vijana kuelekeza nguvu zao katika ubunifu, uzalishaji na ujenzi wa uchumi.

Kwa upande wake, David Hundeyin amesema filamu hiyo inalenga kuhamasisha uelewa kuhusu namna ushawishi wa nje unavyoweza kuathiri jamii za Afrika kupitia njia mbalimbali.

DavidHundeyin Habari Tanzania

What made the *Karibu Nyumbani* Fun Run special was never just the distance, but the people who showed up, shared moment...
30/05/2026

What made the *Karibu Nyumbani* Fun Run special was never just the distance, but the people who showed up, shared moments, encouraged one another, and made *every step feel like home.* Thank you for being part of something truly unforgettable. Until we meet again next year, asante sana for the memories, the energy, and the spirit you brought with you.




KARIBU NYUMBANI YABAMBA OLDUVAI.Washiriki zaidi ya 300 wameshiriki mbio fupi za kilomita 5 katika  bonde la Olduvai Ngor...
25/05/2026

KARIBU NYUMBANI YABAMBA OLDUVAI.

Washiriki zaidi ya 300 wameshiriki mbio fupi za kilomita 5 katika bonde la Olduvai Ngorongoro kwa lengo la kutangaza vivutio vya asili vya Olduvai na Laetoli ambapo historia ya Binadamu wa Kale ilianzia.

Akizungumza kwa Niaba ya Kamishna wa Uhifadhi kwenye tukio hilo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi anayesimamia Huduma za Utalii na Masoko Mariam Kobelo ameeleza kuwa
Ngorongoro kwa kushirikiana na Cape to Cairo Marathon imefanya mbio hizo ili kuonesha utajiri wa utalii wa asili, historia, urithi wa utamaduni na mambo kale uliopo Olduvai na Laetoli k**a Nyumbani kwa asili ya Binadamu. Ameongeza kuwa Ngorongoro ni Nyumbani kwa Nyumbu wanaohama kwa kuwa pumzi ya kwanza ya ndama kupigwa mhuri kabla ya kuhamia maeneo mengine safari yao huanzia Ndutu Ngorongoro.

"Ngorongoro ni Nyumbani kwa asili ya binadamu kisayansi, Ni nyumbani kwa Nyumbu wanaohama kila mwaka, ni nyumbani kwa Spinshi ya Ndege zaidi ya 500, ni nyumbani kwa Wanyama wakubwa watano, kiufupi eneo la Ngorongoro ni Nyumbani kwa mkusanyiko wa Vitu vingi ndio maana tunawaambia wadau wote ndani na nje ya Nchi kuwa Wonders Are Calling" ameongeza Kamishna Kobelo.

Mkurugenzi wa Cape to Cairo Arusha International Marathon, Timothy Mdinka ameeleza kuwa lengo la mbio hizo ni kutangaza mazao mapya ya Utalii yaliyopo Tanzania na Bara la Africa kwa Ujumla kupitia shughuli mbalimbali ikiwemo Michezo k**a mbio ambayo imefanyika leo Olduvai pamoja na marathon ya Cape to Cairo itakayofanyika tarehe 31 Mei, 2026.

Mbio hizo zimejumuisha wadau mbalimbali wakiwepo Ngorongoro, Cape to Cairo international Marathon, Karatu Runners, Amani Collection, CRDB, UNDP, NHIF, Diplomatic and Tourism Police Arusha

SIFA YA WADATOGA KUOA WAKE WENGI.Katika bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii, makabila ya Wadatoga na Wahadzabe ambay...
17/05/2026

SIFA YA WADATOGA KUOA WAKE WENGI.

Katika bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii, makabila ya Wadatoga na Wahadzabe ambayo ni sehemu ya Jiopaki ya Ngorongoro Lengai walitia nakshi na uturi bajeti hiyo kwa kumsindikiza waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Ashatu Kijaji (Mb) kuingia katika ukumbi wa bunge jijini Dodoma.

Wadatoga ni waumini wa kuoa mke zaidi ya mmoja wanaotokana na jamii yao, wana uwezo wa kuoa hadi wake kumi na kila mke akafurahia utamu wa ndoa kutoka kwa mume wake.

Kwa Jamii hii kuwa na wake wengi si heshima tu bali unachukuliwa k**a uchumi kwa kuwa utapata watoto wengi watakaokusaidia shughuli za kuchunga mifugo, kulima chakula cha familia, kufanya kazi za uhunzi, kujenga maboma ya familia na kutanua ukubwa wa jina la ukoo.

Wadatoga hawaishiwi "Power" kwasababu hawali chipsi mayai, soseji wala Baga, hawatafuti energy wala dawa za Congo,hawana mawazo ya vikoba,ni mwendo wa vyakula vya asili tu k**a Ugali, mtama, ulezi, Maharage, mbaazi, viazi vitamu na Maziwa ambapo mafuta ya kupikia hawanunui dukani bali yanatokana na samli kutoka kwenye maziwa ya Ng'ombe yaliyogandishwa kisha kuchekechwa kwenye kibuyu maalum na kuzalisha mafuta ambayo husafishwa kiasili na kukaa muda mrefu bila kuharibika.

K**a wewe ni kijana na unataka kuwa na uwezo wa kuwa na wake wengi karibu makumbusho ya Urithi Jiopaki ujue siri ya wadatoga na vyakula vyao vya miaka na mikaka.

08/05/2026

TANESCO YAANZA RASMI ZOEZI LA ULIPAJI FIDIA WANANCHI WA LINDI NA MTWARA

🛑 Lengo ni kupisha mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa 220kV Masasi, Mahumbika

Jemsi Mbowe atoa wito kwa Vijana,  tumieni Mitandao kwa HekimaMwanasiasa na aliyekuwa mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Hai,...
06/05/2026

Jemsi Mbowe atoa wito kwa Vijana, tumieni Mitandao kwa Hekima

Mwanasiasa na aliyekuwa mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Hai, James Mbowe, ametoa rai kwa vijana nchini kuacha kujihusisha na vitendo vya uvunjifu wa sheria kupitia mitandao ya kijamii.

Amesisitiza kuwa majukwaa ya kidijitali yanapaswa kutumika kwa staha, heshima na uwajibikaji, badala ya kuwa sehemu ya matusi, vitisho na lugha chafu dhidi ya viongozi na wananchi.

“Vijana wajikite katika shughuli za kuwaongezea kipato badala ya kushinda mitandaoni wakishambulia watu,” amesema Mbowe.

Aidha, amegusia hatua za Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kuwashikilia vijana 37 kwa tuhuma za makosa ya kimtandao, akisisitiza kuwa sheria zinafuatwa na hatua zinaendelea kuchukuliwa kwa wanaokiuka matumizi sahihi ya mitandao.

Ujumbe ni wazi: Mitandao ya kijamii si uwanja wa kuvunja sheria, bali ni fursa ya kujenga maisha, kukuza uchumi na kuleta maendeleo kwa jamii.

Tanzania

WAMASAI, WAHADZABE, WADATOGA NA WAIRAQW WANAPOKUTANISHWA NA URITHI WA DUNIAMaadhimisho ya siku ya Urithi wa Dunia Afrika...
05/05/2026

WAMASAI, WAHADZABE, WADATOGA NA WAIRAQW WANAPOKUTANISHWA NA URITHI WA DUNIA

Maadhimisho ya siku ya Urithi wa Dunia Afrika yaliyofanyika katika Makumbusho ya Urithi Jiopaki mjini Karatu tarehe 5 Mei, 2026 yameyakutanisha makabila makuu manne yanayounda Jiopaki ya Ngorongoro Lengai ambayo ni wamasai, wahadzabe, wairaqw na wadatoga na hivyo kuunganisha kutaniko kubwa la urithi wa dunia katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe. Dkt Lameck Karanga amesema uwepo wa makabila hayo, historia yao pamoja na kuenzi tamaduni zao ni utajiri mkubwa kwa Tanzania na kutoa wito kwa wadau na jamii kwa ujumla kuendelea kulinda maeneo ya urithi wa dunia na kuibua maeneo mapya yatakayoingizwa katika orodha ya Urithi wa Dunia ili kuongeza thamani ya ubora wa kipekee ulimwenguni (Outstanding Universal Value) na kuvutia wageni wengi zaidi.

Naibu Kamishna wa Uhifadhi, Utalii na Maendeleo ya Jamii Ngorongoro Joas Makwati ameeleza kuwa mamlaka itaendelea kuongeza juhudi za kulihifadhi eneo la Ngorongoro ambalo ni urithi wa dunia na kultangazia zaidi k**a eneo pekee lenye Ushahidi wa kisayansi kuhusu historia ya binadamu unaoeleza kuwa binadamu kwa kuthibitishwa na ugunduzi wa masalia ya binadamu wa kale na zana za mawe zilizopatikana katika bonde la Olduvai.

Kwa upande wake Naibu Katibu wa Tume ya Taifa ya UNESCO Tanzania Dkt. Khamis Said ameeleza kuwa tangu Tanzania ijiunge na UNESCO imepata mafanikio mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuridhia mikataba kumi (10) ya UNESCO,Kuwepo kwa Hifadhi Hai za Mwanadamu na Mazingira sita (6) na Kuwepo kwa maeneo saba (7) ya urithi wa Dunia.

Kauli mbiu ya siku ya urithi wa dunia kwa mwaka huu ni “Kusherekea siku ya Urithi wa Dunia na kukuza Viongozi wa baadaye”. (Celebrating Africa’s Heritage, Mentoring the Leaders of Tomorrow).

Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Harakati Media posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share