UMGOnline

UMGOnline UHURU MEDIA GROUP
P.O.Box 9221, Dar es Salaam, Tanzania
[Fax] 2183780
[Telephone] +255 (22) 218163

03/11/2023

Mkoa wa Morogoro umeendelea kutekeleza miradi ya maendeleo ya sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu, afya, kilimo pamo...
03/11/2023

Mkoa wa Morogoro umeendelea kutekeleza miradi ya maendeleo ya sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu, afya, kilimo pamoja na usafirishaji na uchukuzi kwa kujenga na kufanya maboresho ya miundombinu ya barabara.

Utekelezaji huu unatajwa kuimarika zaidi katika kipindi hiki cha uongozi wa awamu ya sita ambapo kwa sekta ya usafirishaji na uchukuzi pekee, TARURA ilipokea shilingi bilioni 61.45 katika utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya barabara vijijini.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Morogoro katika kampeni ya TUMEWASIKIA TUMEWAFIKIA inayoendeshwa na Ofisi ya Habari Maelezo, mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Kighoma Malima pamoja na kueleza namna Mkoa unavyojidhatiti katika kukuza uzalishaji wa zao la mpunga na mazao mengine ya biashara amesema kwasasa Mkoa utajielekeza katika uzalishaji wa zao la karafuu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Mobhare Matinyi, amesema serikali imejipambanua zaidi katika kuwasikia na kuwafikia wananchi katika utatuzi wa changamoto.

"Mchezo wa Jumapili umebeba taswira ya mpira wa Tanzania na hivyo tukaona kudumisha utamaduni wetu tukutane hapa tule bi...
03/11/2023

"Mchezo wa Jumapili umebeba taswira ya mpira wa Tanzania na hivyo tukaona kudumisha utamaduni wetu tukutane hapa tule biryan, tununue tiketi na Jumapili twende Uwanja wa Mkapa. Hii ni ishara kwamba tuko tayari."

"Simba Sports Club tumekuwa na matukio mbalimbali ya kudumisha Utanzania. Jumapili tuna kazi moja tu, kwenda kumnyoa Yanga na k**a kuna Mwanayanga amekula biryan letu basi Jumapili atalitapika."

"Kila mtu akate tiketi yake na aandae jezi yake nyekundu au nyeupe. Simba tumejiandaa vizuri kwenda kuendelea pale pale tulipoishia kwa Kibu Deni mgeni rasmi."- Ahmed Ally.

Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Sengerema (SEUWASA)  pamoja na Menejimenti ya SEUWASA w...
03/11/2023

Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Sengerema (SEUWASA) pamoja na Menejimenti ya SEUWASA wakiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ambapo walitembelea mradi wa. Nyasigu-Lubungo-Ngoma.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema amani ndiyo nguzo kuu ya mamb...
03/11/2023

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema amani ndiyo nguzo kuu ya mambo mengine yote bila amani huwezi kuzungumza maendeleo.

Nchi ina amani wananchi wana umoja , mshik**ano na utulivu kuweza kufanya shughuli za ibada bila hofu yoyote na yatupasa kuendelea kumshukuru Mwenyezi Mungu aendelee kutudumishia amani yetu.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo baada ya kujumuika na waumini wa Dini ya Kiislamu katika ibada ya sala ya Ijumaa Masjid Noor Kombeni, Mkoa wa Mjini Magharibi leo tarehe

Vilevile Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa ni wajibu kuilinda na kuitunza amani ya nchi kwa kila mwananchi na si jukumu la Serikali peke yake kwa kuanzia ngazi ya jamii, pamoja na familia kupitia malezi .

Naibu Katibu Mkuu Bw. Amon Mpanju leo tarehe 03 Novemba, 2023 amewaasa wasanii kuzingatia maadili katika shughuli zao kw...
03/11/2023

Naibu Katibu Mkuu Bw. Amon Mpanju leo tarehe 03 Novemba, 2023 amewaasa wasanii kuzingatia maadili katika shughuli zao kwakuwa zina nguvu na umuhimu wa kuimarisha misingi ya utamaduni wa jamii yoyote duniani.

Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa tatu kubwa za basata ambapo amekiri kufurahishwa na uzinduzi wa Muongozo wa uzingatiaji wa maadili katika kazi za sanaa ambao utaimarisha maudhui ya kazi za sanaa nchini.

Sekta ya Maji kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) imekabidhi majengo ya vyoo kwa shule 1...
03/11/2023

Sekta ya Maji kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) imekabidhi majengo ya vyoo kwa shule 11 pamoja na vituo vya afya vinne katika wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza kwa lengo la kuimarisha hali ya usafi wa mazingira katika taasisi hizo.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Bi. Neli Msuya amekabidhi kwa Diwani wa Kata ya Ilemela, Wakili Willbard Kilenzi aliyepokea kwa niaba ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela, Mhe. Renatus Malungu.
Bi. Neli amesema hatua hiyo itaimarisha hali ya usafi wa mazingira katika taasisi hizo.
"Katika mradi huu wa vyoo tumeweka pia matenki ya maji hii itasaidia watumiaji kunawa mikono kwa majisafi na sabuni ili kulinda afya zao k**a muongozo wa afya unavyoelekeza pia kujiepusha na magonjwa yasababishwayo na uchafu,” Bi. Nelly amesema
Diwani wa Kata ya Ilemela, Wakili Willbard Kilenzi ameipongeza MWAUWASA kwa mradi huo ambapo amesema utakuwa msaada katika kuimarisha hali ya usafi wa mazingira katika taasisi hizo.
"Kwa niaba ya Manispaa ya Ilemela tunasema asante sana MWAUWASA kwa mradi huu wa vyoo pamoja na miradi mingine mnayoendelea kuitekeleza katika wilaya yetu, mmejenga vyoo hivi kwa ubora na tuwaahidi tutavitunza ili vidumu na kuendelea kuwa msaada kwa watumiaji," Wakili Kilenzi amesema.
Mradi huo umetekelezwa na MWAUWASA chini ya Mkandarasi kampuni ya M/s. URSINO LIMITED kwa fedha iliyotolewa na Serikali pamoja na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) kwa gharama ya shilingi bilion 2.26.
Mradi umetekelezwa kwa muda wa miezi 15 ukitarajiwa kunufaisha walimu na wanafunzi wapatao 14,233 katika shule za msingi za Nyamwilolela, Mhonze, Umoja, Mihama, Bugongwa, Chabusi, Sangabuye, Bugungumuki, Tumaini, Kabangaja pamoja na shule ya msingi Igombe.
Vituo vya Afya vilivyonufaika na mradi huo ni pamoja na kituo cha afya Karume, Sangabuye, Nyamwilolela pamoja na Lumala.

Serikali imesema inaangalia uwezekano wa kufanya vikao vya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikal...
03/11/2023

Serikali imesema inaangalia uwezekano wa kufanya vikao vya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kuwa vya kisheria.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis wakati akijibu maswali bungeni jijini Dodoma leo Novemba 3, 2023.

Amesema kuwa changamoto zote za Muungano zimekuwa zikitatuliwa na kupatiwa ufumbuzi kwa njia ya majadiliano na maridhiano, utaratibu ambaoi umekuwa wa mafanikio makubwa.

Mhe. Khamis amesema kuwa katika utatuzi wa changamoto hizo umeandaliwa utaratibu wa vikao vya Kamati ya Pamoja ya SJMT na SMZ wa kushughulikia masuala ya Muungano wa Aprili 2019.

Akiendelea kujibu swali la Mbunge wa Jimbo la Mwera Mhe. Zahor Mohammed Haji, Naibu Waziri Khamis amesema kuwa utaratibu wa vikao hivi umetumika kwa mafanikio makubwa na kuhakikisha changamoto nyingi zinatatuliwa.

Ujumbe wa Marafiki waliosoma na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko (Mb) ukiongozwa na Mbunge ...
03/11/2023

Ujumbe wa Marafiki waliosoma na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko (Mb) ukiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Hai, Mhe. Saashisha Mafuwe umetoa pongezi kwa Dkt. Biteko kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati.

Wametoa pongezi hizo leo Novemba 3, 2023 katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma ikiwa ni pamoja na kumtakia heri katika majukumu yake mapya ambapo wamesisitiza kuunga mkono juhudi za Serikali.

Kwa upande wake, Dkt. Biteko amewashukuru kwa kumtakia heri na kuwataka kufanya kazi kwa bidii ili azma ya Mhe. Rais Samia itimie katika kujenga uchumi wa nchi na Watanzania wanufaike.

Ujumbe huo ni wanafunzi waliosoma Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine Mwanza (SAUT) na marafiki wengine waliosoma maeneo mbalimbali nchini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Ujumbe Maalum kutoka kwa Mfalme wa Saudi Arabi...
03/11/2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Ujumbe Maalum kutoka kwa Mfalme wa Saudi Arabia Salman bin Abdulazizi Al Saud uliowasilishwa na Balozi wa Saudi Arabia hapa nchini Yahya Ahmed Okesh mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 03 Novemba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Balozi wa Saudi Arabia nchin...
03/11/2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania Mhe. Yahya Ahmed Okesh baada ya kuwasilisha Ujumbe Maalum kutoka kwa Mfalme wa Saudi Arabia Salman bin Abdulazizi Al Saud Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 03 Novemba, 2023.

Address

Dar Es Salaam
POBOX9221

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when UMGOnline posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to UMGOnline:

Share