B24 Newz Tz

B24 Newz Tz B24 Newz ni ukurasa ambao unatumika kukupasha taarifa mbalimbali kuhusu matukio yanayojiri duniani bila upendeleo wowote

17/01/2026

šŸŽ„Hii ndiyo sehemu ndogo ya Bukoba Vijijini

16/01/2026

šŸŽ„Wamiliki wa Night Club kuna ujumbe wenu hapa

16/01/2026

šŸŽ„Kampuni ya mabasi ya Shabiby yanunua mabasi 70 ya Yutong,mkataba umesainiwa nchini morocco Tarehe 15/01/2026.

13/01/2026

šŸŽ„Diwani wa kata Kemondo Mhe,Khatwib M***a Kayoza ampigia salute Mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini Dkt Jasson Rweikiza

12/01/2026

šŸŽ„Hatimaye walichokihitaji wananchi wa Kijiji Nyakigando kata Kaibanja wamekipata




ZIARA YA SIKU SITA YA MBUNGE RWEIKIZA ILIVYOACHA NEEMA KWA WANANCHI JIMBONI MWAKE.Ziara ya Mbunge wa Jimbo la Bukoba Vij...
11/01/2026

ZIARA YA SIKU SITA YA MBUNGE RWEIKIZA ILIVYOACHA NEEMA KWA WANANCHI JIMBONI MWAKE.

Ziara ya Mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini Dkt Jasson Rweikiza iliyofanyika kwa muda wa siku sita katika vijiji 27 vilivyopo kata 23 imetamatika Januari 10,2025 huku ikiwa imeacha neema kwa wananchi.

Dkt Rweikiza akiwa katika ziara hiyo amewashukru wananchi wote kutoka vijiji 94 vya Jimbo la Bukoba Vijijini kwa kuwapigia kura za kihistoria wagombea wa Chama Cha Mapinduzi CCM katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika 2025.

Akiwa katika ziara hiyo pia Dkt Rweikiza alisisitiza kuwa miradi iliyotajwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi itatekelezwa hatua kwa hatua hivyo wananchi wawe wavumilivu na wawe tayari kutoa ushirikiano wa kutosha pindi watakavyoombwa kufanya hivyo.

Ziara hiyo ilikuwa maalumu kwa ajili ya kushukru na kutimiza ahadi yake binafsi kwenye vijiji 27 ambavyo vilipiga kura nyingi kwa wagombea wa CCM ambapo kijiji cha Bulinda kata Kanyangereko ndicho kilichoongoza na kujipatia shilingi milioni tano,kijiji cha pili ni Nyakigando kata Kaibanja ambacho kilipatiwa shilingi milioni nne, Kijiji cha tatu ni Buganguzi kata Bujugo ambacho kilipatiwa shilingi milioni tatu na cha nne ni kijiji Kyamulaile kilichopo kata Kyamulaile ambacho kilipatiwa shilingi milioni mbili.

Vijiji vyingine 23 vilipatiwa shilingi milioni 23 ambapo kila kijiji kimepatiwa shilingi milioni moja huku Dkt Rweikiza akiweka wazi kuwa wenye mamlaka ya fedha hizo zinatumika vipi ni wananchi wenyewe na wala sio viongozi.

Nao wananchi wamemshukru sana Dkt Rweikiza kwa kutimiza ahadi hiyo ndani ya muda mfupi huku wakimwelezea kuwa bado wana imani naye sana hata k**a akitaka kugombea tena 2030.




11/01/2026

šŸŽ„Piano la Kihaya

09/01/2026

šŸŽ„SEHEMU YA KWANZA

DIWANI LWAKOMEZI AMSHUKRU DKT RWEIKIZA KWA KUMWAMINI MIAKA 10 K**A KATIBU WAKE.

Diwani wa kata ya Kaibanja Mhe,Jasson Lwankomezi amemshukru mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini Dkt Jasson Rweikiza kwa kumwamini na kufanya nae kazi k**a katibu wake kwa kipindi cha miaka kumi.

Mhe,Lwankomezi ametoa shukrani hizo katika Mkutano wa hadhara wa Dkt Rweikiza wa kuwashukru wananchi waliompigia kura za ushindi uliofanyika kijiji Nyakigando kata Kaibanja

Mbali na kushukru Mhe,Lwankomezi amebainisha kuwa yupo tayari kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Katibu mpya alieaminiwa kwa kipindi hiki.

09/01/2026

šŸŽ„Mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini Dkt Jasson Rweikiza akizungumza na wananchi wa kijiji Nyakigando kata Kaibanja amewashukru kwa kumpigia kura za kishindo huku akiwahakikishia kuwa miradi ya maendeleo iliyopo katika Ilani ya chama itatekelezeka hatua kwa hatua.

Kijiji cha Nyakigando kimekuwa cha pili kwenye vijiji vilivyopiga kura nyingi kwa wagombea wa Chama Cha Mapinduzi CCM katika uchaguzi mkuu wa 2025 na kujinyakulia shilingi milioni nne.

Tofauti na Nyakigando kijiji ambacho kimepata shilingi milioni nne, vijiji vingine vinne navyo vimetimiziwa ahadi ambavyo ni Kijiji Kiziru kata Karabagaine ambacho kimepata shilingi milioni moja,kijiji Kishogo kata Kishogo kimepata shilingi milioni moja,Kijiji Bundaza kimepata shilingi milioni moja na Kijiji Bwizanduru kata Maruku shilingi milioni moja.




08/01/2026

šŸŽ„SEHEMU YA KWANZA

IZIMBYA WAMSHUKRU DKT RWEIKIZA KWA KUTAMBUA MCHANGO WAO KWENYE USHINDI WAKE,YEYE AWAAHIDI MAKUBWA.

Wananchi wa kata ya Izimbya wamemshukru Mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini Dkt Jasson Rweikiza kwa kutambua mchango wao baada ya kalizika kwa uchaguzi mkuu 2025 uliompa kura za kishindo.

Diwani wa kata hiyo Venant Tryphone amesema kuwa,Dkt Rweikiza amefika kuwashukru hivyo watampa tena.

Dkt Rweikiza akizungumza na wananchi hao ,amewashukru kwa kumpigia kura za kishindo huku akiwaahadi kumalizia ujenzi wa kiliniki ya Butulage ndani ya mwaka huu.

Ameongeza kuwa atatoa mchango wa shilingi Milioni tano kwenye ujenzi wa Zahanati ya Izimbya ndani ya miezi michache ijayo.

Dkt Rweikiza akiwa katika ziara yake ya shukrani ametimiza ahadi yake kwa vijiji vinne ambapo ametoa shilingi milioni nne.

Vijiji ambavyo jana vimetimiziwa ahadi ni Kijiji Izimbya kata Izimbya ambacho kimepokea shilingi milioni moja,Kijiji Mishenye kata Butelankuzi shilingi milioni moja,Kijiji Kagondo kata Mikoni shilingi milioni moja na Kijiji Buguruka kata Kanyangereko




08/01/2026

šŸŽ„SEHEMU YA PILI

Ndg,Deocles Byabato amebainisha kuwa wakati wa uchaguzi chama kilizuia wagombea kutoa ahadi kwa hofu ya kushindwa kuzitimiza lakini Dkt Rweikiza aliwahakikishia kuwa ahadi ya kutoa zawadi kwa vijiji imo ndani ya uwezo wake na ataitimiza mara baada ya uchaguzi.

07/01/2026

šŸŽ„SEHEMU YA KWANZA

WANANCHI KIJIJI KAGARAMA WAMSHUKRU DKT RWEIKIZA KWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO.

Baadhi ya wananchi katika kijiji cha Kagarama wamemshukru Mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini Dkt Jasson Rweikiza kwa utekelezaji wa miradi ya Maendeleo

Hata hivyo wananchi hao wamemuomba kushughulikia suala changamoto ya uchakavu wa madarasa katika shule zilizopo katika kata hiyo pamoja na ufungaji wa pamu ya umeme katika kisima cha maji kinachohudumia kijiji Kagarama.

Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when B24 Newz Tz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to B24 Newz Tz:

Share