Funguka LIVE

Funguka LIVE Hii ndiyo fursa ya Funguka kuhusu mambo mbali mbali yanayokugusa
TUKI SHARE HABARI na BURUDANI

K**A WEWE NI KIJANA, HILI LINAKUHUSUWengi itakuwa bado miaka miwili, mitatu au minne kabla ya kutimiza miaka 30. Natambu...
24/02/2026

K**A WEWE NI KIJANA, HILI LINAKUHUSU

Wengi itakuwa bado miaka miwili, mitatu au minne kabla ya kutimiza miaka 30.

Natambua kuwa kuna waliokwisha fikisha na kuna uwezekano kuna walio nyuma kidogo.

K**a katika umri tulionao sasa kuna mtu anakuambia wewe bado ni mdogo/mtoto, basi huyo mtu hakupendi na anakulemaza kiakili.
Kua! Acha utoto! Mambo yafuatayo kwa vigezo vya kibinadamu mwenye akili timamu, mtu mwerevu lazima uwe ushayatimiza.

1) Kuweka misingi ya kifamilia:

Katika umri huo unatakiwa uwe umeoa, umechumbia au uko katika uhusiano wenye kueleweka unaelekea kwenye kujenga familia. K**a katika umri huu bado unabadilisha wanawake na kudandia vicheche, basi sahau kuwa na familia imara. Mambo yafuatayo yatakuwa yanakunyemelea;
– Kuoa/kuolewa msichana/mvulana mdogo sana ambaye atakuona unamzeesha
– Kuoa /kuolewa chapchap bila kuwaza
-Kuokoteza magonjwa ya hatari
– Kunogewa na usela na kusahau kuoa/kuolewa

2)Kujitegemea kiuchumi:
Hapa simaanishi kufanya kazi na kupata mshahara pekee, la hasha! Hapa nalenga wale watoto wa mama ambao pamoja na kuwa wana kazi na mishahara, bado wanalalama mishahara haitoshi na kukimbilia kuomba hela nyumbani wanapoishiwa mara kwa mara. Wale ambao bado wanakaa nyumbani hii inawahusu pia. Pia wale wanaotumia 100% ya mishahara kununua vitu vinavyoisha (consumption) wakingoja wapate hela nyingi au wazazi, ndugu na jamaa wawasaidie kwenye uwekezaji. Africa tunachelewa sana kwenye hii sector.
3) Kuwa na kitega uchumi:
K**a unadhani mshahara wako wa milioni kadhaa ni mwingi sana, ngoja augue mtu wa karibu au wewe mwenyewe halafu daktari akuambie mgonjwa wako/wewe ana/unatakiwa ape/upelekwe nje ya nchi kwa matibabu zaidi wakati huna bima ya afya inayolipia hilo ndo utajijua k**a mshahara wako heshima yake inaishia samaki samaki au inavuka border. Kitega uchumi si lazima uwe na mkampuni mkubwa, la hasha! Ila uwe na kitu cha kueleweka na chenye malengo ya kukua kuwa kitu cha maana. Kwa wale wagumu kuelewa, UNATAKIWA UWE NA PATO LA PEMBENI NJE YA MSHAHARA.

4) Makazi:
Uwe hata na kiwanja hapo Bunju Arif! Huezi kunywa bia kila weekend halafu wenzio wakiongelea issues za nyumba/viwanja/mashamba yao unakimbilia kubadilisha mada (Eti Huyu LVG wamuondoe kabisa anaharibu timu). Kumbe unazuga kupotezea story za viwanja/nyumba.

5)Uwe na professional qualification

: ACCA,CPA,CFA,CSIA,CPB, LAW SCHOOL ETC wale wa procurement wana ya kwao n.k. Ikifika huu umri k**a CPA imekataa, tafuta hata mitihani za marketing upige, CPA sio issue zako. Lazima uwe na defined career (K**a hukubahatika kwenda kidato kingi, uwe na namna ya halali na ya kudumu ya kukupatia kipato). Umri huu k**a huna utaalam katika fani yako, jiandae kuwa frustrated ofisini. Madogo wanasoma jamaa angu! Halafu wako tayari kupewa salary ndogo wapige kazi kuliko wewe.. So take care!

6) Uwe ushaamua ka hicho kitambi unakiondoa au unakilea:

Hapa sichekeshi! Kitambi kina madhara mengi. Suruali haikai vizuri, UTAPIGIWA, Kisukari, pressure n.k. Ukikinyamazia muda huu jua kitakuwa kishakomaa na majukumu yatakuwa mlima. Ukikiachia kijiamulie, kitakuganda k**a “roba ya mbao” till death does you apart! K**a unakipenda endelea nacho, k**a hukipendi uwe ushaweka program ya kukiondoa.

7)Uwezo wa kusaidia wanaokutegemea:

K**a we ni wa kishua, hapa hapakuhusu. Wewe ambaye si wa kishua, wazazi walikuwa na mategemeo flani walipokuwa wanakusomesha. K**a umefika miaka 30 hujaanza kuyatimiza mategemeo yao bila sababu ya msingi, jua watakuwa washakata tamaa na wewe.

8) Uwe na busara.

Kuwa mtu wa kufikiri kabla ya kutenda. Tengeneza haiba nzuri na ya kuheshimika kwa wanaokuzunguka. K**a huna busara hadi umri huu basi we sahau suala la busara ukiwa hai.. Labda utakutana nayo akhera.!

9) Savings:

Hapa nimeweka kizungu kuonyesha msisitizo. Kila mtu ana kipato chake. Ila formula ni kwamba angalau uwe ushahifadhi fedha sawa na mishahara yako ya mwaka na nusu gross of Tax kwa kipindi hicho. Kwa wale wagumu kuelewa namaanisha Ukiacha kazi au kusimamishwa kazi, uwe na uwezo wa kukaa mwaka na nusu bila kuingiza kitu chochote lakini uendelee kuishi maisha yale yale.

10) Umjue Mungu:

Nimeliweka hili mwisho si kwamba ni la mwisho kwa umuhimu, La hasha! Ni ili ulikumbuke zaidi. Mjue Mungu, mpende na umuogope. Nenda ibadani, soma neno lake na umuombe. Uwe na desturi ya kusali nyumbani kwako angalau kila unapoamka na wakati wa kulala. K**a humuogopi Mungu katika umri huu, basi wewe kwenda Mbinguni ni ngumu kuliko ngamia kupenya tundu la sindani (hata k**a ni masikini).

A Powerful City Disappeared | History Barely Explains Why
20/01/2026

A Powerful City Disappeared | History Barely Explains Why

Before the world we know today, there were secrets.This is Part One of a mysterious story about a powerful city that once thrived with life, culture, and kno...

ZIJUE AINA ZA WANAWAKE WANAOPENDWA  SANA NA WANAUME  WAPENDA USAWA-Hii ni aina ya kipekee inayohitajika katika katika ul...
23/01/2022

ZIJUE AINA ZA WANAWAKE WANAOPENDWA SANA NA WANAUME
WAPENDA USAWA-
Hii ni aina ya kipekee inayohitajika katika katika ulimwengu wa kimapenzi ni wanawake wanaoheshimu usawa wa jinsia, walio tayari kubeba majukumu yakifamilia kwa ulinganifu sawa na wanaume, wenye uwezo wa kuongoza jamii kwa asilimia 50 kwa 50.

Wanawake wajuzi wa mambo ya faragha wanapendwa sana. Sifa yao kubwa niuwezo wa kuwatosheleza wenzi wao katika tendo la ndoa. Tafiti zinaonesha kuwa wanaume hupenda sana wanawake watundu katika mchezo wa sita kwa sita. Mara nyingi wanatajwa kuwa na uwezo wa kuteka akili za wanaume bila kujali sifa zao za nje au za ndani.

MARAFIKI -
Wanawake wenye sifa sawa na rafiki ni aina ya nne inayowavutia wanaume.Wao hutegemea zaidi nguvu ya kushawishi inayotokana na namna wanavyojali na kujitolea kuhakikisha wanakuwa marafiki wa kweli kwenye shida naraha kwa wapenzi wao. Si wakorofi, ni waungwana na wapenda amani.

Tuandikie Maoni yako.

  Hebu Niambie Nini Kinakuvutia Zaidi Na Unajivunia Katika Mila Za Kiafrika?
25/01/2021


Hebu Niambie Nini Kinakuvutia Zaidi Na Unajivunia Katika Mila Za Kiafrika?

Upendo Ni Miongoni Mwa Hisia Za Asili Anazozaliwa Nazo Kila Binadamu.Lakini Moyo,Utashi Pamoja Na Hisia Ndio Huamua Nini...
22/05/2018

Upendo Ni Miongoni Mwa Hisia Za Asili Anazozaliwa Nazo Kila Binadamu.
Lakini Moyo,Utashi Pamoja Na Hisia Ndio Huamua Nini,Nani Na Kivipi Upendo Udhihirishwe...

Nakutakia Wakati Mwema

HIVI, UNAZITAMBUA DALILI AMBAZO ZIKIKUTOKEA ZITAKUONYESHA K**A KAZI ULIYOPO NI SAHIHI KWAKO AU LA? SOMA UJIELIMISHEJiuli...
01/11/2017

HIVI, UNAZITAMBUA DALILI AMBAZO ZIKIKUTOKEA ZITAKUONYESHA K**A KAZI ULIYOPO NI SAHIHI KWAKO AU LA? SOMA UJIELIMISHE

Jiulize, ????????????????????
JE ...viatu ulivyovaa ni siazi yako na k**a ndio ni aina yako?
Miongoni mwetu tunatumia asilimia 75 ya muda wetu kwa siku katika kazi.
Kwahiyo kuwa katika kazi ambayo haikupi faraja inaweza ikakuletea matatizo katika maisha yako ya kila siku.

Umejaribu njia zote kujitahidi kuendana na hali lakini bado unaona wazi kabisa kwamba kuna kitu kinakosekana.
Ni ukweli usiopingika kuwa kazi yoyote ile kwa upande mwingine kuna kipindi inachosha.
Unachopaswa kujiuliza ni je,
hali hii unayojisikia ni ya muda au ni ya kudumu?
K**a ushawahi kukumbana na hali hiyo au kujiuliza hilo swali basi makala hii inakuhusu.
Sasa utajuaje k**a kazi uliyopo sasa ulifanya uamuzi sahihi kuifanya au ulikosea?

Kwa kifupi sana zifuatazo ni dalili ambazo unapaswa kuziangalia ili kufahamu na kutatua fumbo hili:
1.HUNA SHAUKU YA KUPANDA DARAJA

2.UNAJIONA UKO PEKE YAKO

3.KILA WAKATI HUISHI KULALAMIKA

4.KIPAUMBELE CHAKO NI PESA TU

5.HAKUNA JIPYA UNALOJIFUNZA

6.HUJIONI KUKUA KATIKA KAZI YAKO

7.HAUIONEI FAHARI KAZI YAKO

8.UNAJIHUSISHA NA VITU VYA OVYO UKIWA KAZINI

9.HAUTUMII UWEZO WAKO

RAHA YA MAISHA NI KUFURAHIA KITU UNACHOFANYA,
IWE INAKUINGIZIA KIDOGO AU KIKUBWA FURAHA NDIO HUWA KIPAUMBELE.

KUFANIKIWA NI ZAIDI YA KUWA KIPATO KIKUBWA
NA MALI.
ANZA LEO KUTAMBUA KAZI UNAYOIPENDA NA UANZE KUISHI MAISHA YA MAFANIKIO KWA KUUTUMIA UWEZO WAKO KAMILI.

18/10/2017

According to Dr. John M. Gottman of the Gottman Institute , fighting isn't a sign of a weak relationship, but a strong one… depending on h...

30/04/2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na viongozi wa dini wa mkoa wa Kilimanjaro baada ya kupata nao c...

09/04/2017

Bofya Hapa Kuona Ibada  

Address

Kinondoni
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Funguka LIVE posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share