26/11/2023
MWANYEKITI WA CHAMA PROF. LIPUMBA ALAANI KITENDO CHA POLISI KUVAMIA NA KUZUIA MKUTANO JIJINI DARA ES SALAAM.
Mwenyekiti wa chama cha CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akifafanua katika mkutano wake na waandshi wa habari kuhusu kitendo cha jeshi la polisi buguruni kuvamia na kusitisha mkutano wao wa hadhara siku ya tarehe 24 November 2023 makao makuu ya chama hicho Buguruni jijini Dar es salaam.
Alisema jeshi la polisi lisiturudishe kwenye siasa ya mapambano basi sisi tunataka siasa za kujenga hoja na maridhiano ambazo hata Rais Samia mwenyewe anatangaza siasa za maridhiano, kufatia tumio hili inaonyesha kuwa bado falsafa ya mhe rais juu ya maridhiano bado aijaeleweka kwa baadhi hivyo nishauri serikali iandae utaratibu wa kutoa mafunzo kuelezea siasa za maridhiano ni nini.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha CUF ilala, bwana Hamis Chambuso amemtaka waziri wa mambo ya ndani kuomba rai mara moja kufatia kitendo kilichofanywa na OCD wa Buguruni licha ya chama kufuata taratibu zote wakati maandalizi siku ya mkutano Polisi wakavamia na kuvunja mkutano huo.
“Kitendo hiki ni cha kukemewa kwa Tunajipanga kwenda kwenye uchaguzi hivyo vitendo k**a hivi havikubaliki ukizingatia tupo Dar es Salaam palipofanyika maridhiano sasa sijui huko mikoani kutakuwaje?”Alisema Chambuso.