04/07/2017
TETESI KUTOKA BARANI ULAYA TAR. 04/06/2017
Mshambuliaji wa Spain na Chelsea Diego Costa, 28, anataka kuondoka Stamford Bridge kwa wakati anaotaka yeye, na jambo hilo linachelewesha hatua ya Chelsea kumsajili Romelu Lukaku, 24, kutoka Everton (Chanzo Daily Mirror).
Antonio Conte anataka Chelsea watoe hata paundi milioni 100 kumsajili Romelu Lukaku, k**a Everton wanataka kiasi hicho ili kumuuza (Chanzo The Telegraph).
Mshambuliaji kutoka Argentina Lionel Messi, 30, atasaini mkataba mpya Barcelona mara tu atakaporejea kutoka kwenye fungate yake baadaye mwezi huu (Chanzo Goal).
Paris Saint-Germain wanajiandaa kupanda dau jipya la kumtaka mshambuliaji wa Monaco Kylian Mbappe, 18, na wamewasiliana na wawakilishi wa mchezaji huyo (Chanzo L’Equipe).
Arsenal wanapanga kutoa paundi milioni 70 kuwasajili viungo wawili kutoka Sporting Lisbon ya Ureno, William Carvahlo, 25, na Gelson Martins, 22 (Chanzo A Bola).
Arsene Wenger atakutana na Alexis Sanchez, 28, na Hector Bellerin, 22, wiki hii kujaribu kuwashawishi wasiondoke Emirates (Chanzo The Sun).
Everton wana uhakika wa kumrejesha Goodison Park Wayne Rooney, 31, kutoka Manchester United msimu huu (Chanzo TalkSport).
West Ham United wanataka kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Javier Hernandez “Chicharito” , 29, kutoka Bayer Leverkusen (Chanzo Telegraph).
Liverpool wanapanga kutoa euro milioni 12 kumsajili kipa wa Sevilla Sergio Rico (Chanzo ABC Sevilla).
Chelsea wameonesha dalili kuwa wapo tayari kutoa paundi milioni 60 kumsajili beki wa kushoto Alex Sandro kutoka Juventus (Chanzo Telegraph).
Barcelona wanaongoza katika mbio za kumsajili beki wa Juventus Leonardo Bonucci. Chelsea wanataka kumsajili beki huyo, lakini yeye angependa kwenda Barcelona (Chanzo Daily Mirror).
Inter Milan wanataka kupanda dau la kumtaka mshambuliaji wa PSG Angel di Maria (Tuttosport).
Kipa wa zamani wa Arsenal Jens Lehmann anatarajia kurejea Emirates k**a mmoja wa makocha wa kikosi cha kwanza (Chanzo Guardian).
Gianluigi Donnarumma amekataa kuhamia Paris-Saint-Germain na amekubali kusaini mkataba mpya kusalia AC Milan (Chanzo Sky Sport Italia).
Kiungo wa zamani wa Manchester United Ravel Morrison, 24, amefanya mazoezi na Birmingham City, akitaka kuhamia klabu hiyo kutoka Lazio (Chanzo Daily Mirror).
Southampton wanataka kukamilisha usajili wa paundi milioni 8.75 wa mshambuliaji Yann Karamoh, 18, ambaye ana mzozo na klabu yake ya Caen ya Ufaransa (Chanzo Sun).
Meneja wa Atletico Madrid Diego Simeone ameanza mazungumzo na klabu hiyo kuhusu mkataba mpya utakaompeleka hadi mwaka 2020 (Chanzo AS).
Meneja wa Manchester United Jose Mpurinho anakasirishwa na hatua ya klabu hiyo kutosajili wachezaji zaidi ya Victor Lindelof, 22, peke yake mpaka sasa (Chanzo Daily Mirror).
Jose Mourinho anataka mshambuliaji Alvaro Morata, 24, kutoka Real Madrid na kiungo Nemanja Matic, 28, kutoka Chelsea wajiunge na kikosi chake kabla ya Jumapili watakapoanza safari ya Marekani ya mechi za maandalizi (Chanzo Daily Star).
Real Madrid ‘wamekomaa’ na Alvaro Morata hadi Manchester United watakapotoa paundi milioni 79 (Chanzo Marca).
Kiungo kutoka Guinea Naby Keita, 22, anataka kuhamia Liverpool, lakini klabu yake RB Leipzig inataka paundi milioni 70 (Chanzo Daily Mirror).
Crystal Palace wameshindwa kulipa paundi milioni 30 wanazotaka Liverpool kwa ajili ya beki wa kati Mamadou Sakho, 27 (Chanzo Guardian).
Manchester United wanajiandaa kupanda dau kumsajili beki Marc Bartra, 26, kutoka Borussia Dortmund (Chanzo Manchester Evening News).
Newcastle bado hawajafanikiwa kumsajili kipa Pepe Reina, 34, kwa kuwa Napoli hawajapata mtu wa kuziba nafasi yake (Chanzo Newcastle Chronicle).
Leicester City wamefanya mazungumzo ya awali na Sevilla kuhusu usajili wa kiungo Vicente Iborra (Chanzo Sky Sports).
Kipa Wojciech Szczesny amerejea Arsenal kutoka Roma alipokuwa kwa mkopo kwa miaka mwili (Chanzo Instagram)
Tafadhari Gonga “SHARE” ili habari hizi ziwafikie na wadau wengine wapenda soka.
Tetesi nyingine kesho panapo majaaliwa, "LIKE" page yetu ya Spotibez ili habari hizi ziwe zinakufikia moja kwa moja kila zinapotoka, One Love!
https://www.facebook.com/Spotibez