The Afya Post

The Afya Post Elimu, Taarifa na Habari za afya kwa Kiswahili

Kutumia dawa za antibayotiki mara kwa mara kwa muda mrefu husababisha fangasi kwani dawa hizo huua wadudu wote wanaolind...
02/12/2023

Kutumia dawa za antibayotiki mara kwa mara kwa muda mrefu husababisha fangasi kwani dawa hizo huua wadudu wote wanaolinda mwili na kuacha uke ukiwa hauna kinga. Dawa za antibayotiki ni pamoja na Ciprofloxacin, Doxycycline, Erythromycin, Gentamicin, Ampicillin na Amoxicillin

Ripoti ya utafiti ya baraza la utafiti wa kimatibabu la India (IACMR) imeonesha kupunguza kiwango cha wanga hasa wali na...
02/12/2023

Ripoti ya utafiti ya baraza la utafiti wa kimatibabu la India (IACMR) imeonesha kupunguza kiwango cha wanga hasa wali na chapati katika lishe husaidia kupunguza hatari ya ugonjwa wa kisukari cha aina ya 2. Aina hii ya kisukari hutokana na mtindo wa maisha au umri.

Neno AMBULANCE kwenye gari la wagonjwa huandikwa kinyume ili kumuwezesha dereva anaekua mbele kusoma kwa ufasaha kwa kut...
13/11/2023

Neno AMBULANCE kwenye gari la wagonjwa huandikwa kinyume ili kumuwezesha dereva anaekua mbele kusoma kwa ufasaha kwa kutumia Side Mirror/kioo cha pembeni.

Nimonia ni ugonjwa unaoathiri mfumo wa kupumua.   Dalili zake ni pamoja na  • Kupata shida ya kupumua  • Kuongozeka kwa ...
12/11/2023

Nimonia ni ugonjwa unaoathiri mfumo wa kupumua.

Dalili zake ni pamoja na
• Kupata shida ya kupumua
• Kuongozeka kwa mapigo ya moyo
• Joto mwilini
• Kutetemeka, kutokwa na jasho
• Kukohoa
• Maumivu ya kifua
• Kichwa kuumwa, kuhisi kutapika na kuharisha

Baada ya miaka saba ya utafiti na majaribio matatu, sindano ya uzazi wa mpango kwa wanaume ipo tayari. Sindano hiyo inai...
12/11/2023

Baada ya miaka saba ya utafiti na majaribio matatu, sindano ya uzazi wa mpango kwa wanaume ipo tayari. Sindano hiyo inaitwa Reversible Inhibition of S***m Under Guide (RISUG) ambayo imeonesha ufanisi kwa asilimia 99.02% katika kuzuia mimba.

Ripoti ya utafiti wa afya ya uzazi na mtoto na viashiria vya Malaria (TDHS) ya mwaka 2022 inaonyesha zaidi ya nusu ya wa...
12/11/2023

Ripoti ya utafiti wa afya ya uzazi na mtoto na viashiria vya Malaria (TDHS) ya mwaka 2022 inaonyesha zaidi ya nusu ya wanawake kwenye maeneo mbalimbali nchini wana kiriba tumbo, huku mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya na Kusini Unguja ilkiongoza.

Naibu waziri wa afya Dk Godwin Mollel ameipa miezi mitatu menejimenti ya Mfuko wa Bima ya Afya NHIF ihakikishe imeboresh...
10/11/2023

Naibu waziri wa afya Dk Godwin Mollel ameipa miezi mitatu menejimenti ya Mfuko wa Bima ya Afya NHIF ihakikishe imeboresha mifumo itakayoweza kuondoa usumbufu na pia kudhibiti udanganyifu pasipo kuwa kero kwa wanufaika wa mfuko.

Mamlaka ya chakula na dawa nchini Marekani (FDA) imepitisha chanjo ya kwanza duniani ya ugonjwa wa chikungunya, chanjo h...
10/11/2023

Mamlaka ya chakula na dawa nchini Marekani (FDA) imepitisha chanjo ya kwanza duniani ya ugonjwa wa chikungunya, chanjo hiyo inayojulikana k**a Ixchiq imeidhinishwa kwa wale walio na umri wa miaka 18 na zaidi na wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa ugonjwa huo.

Kushindwa kusimama kwa mguu mmoja kwa angalau sekunde 20 inaweza kuwa ishara ya uwepo wa tatizo kwenye ubongo wako huku ...
10/11/2023

Kushindwa kusimama kwa mguu mmoja kwa angalau sekunde 20 inaweza kuwa ishara ya uwepo wa tatizo kwenye ubongo wako huku tafiti zikitaja shida hiyo kuwepo kwenye mishipa ya damu ya ubongo au mfumo wa neva kwa ujumla.

Awali huduma ya uwekaji p**o ili kupunguza unene ilikuwa ikipatikana Hospitali ya Mloganzila pekee kwa gharama ya Sh mil...
10/11/2023

Awali huduma ya uwekaji p**o ili kupunguza unene ilikuwa ikipatikana Hospitali ya Mloganzila pekee kwa gharama ya Sh milioni 4.

Tangu kuanza kwa huduma ya upasuaji wa kupunguza uzito Hospitali ya Taifa ya Muhimbili – Mlonganzila imeweza kufanya upa...
10/11/2023

Tangu kuanza kwa huduma ya upasuaji wa kupunguza uzito Hospitali ya Taifa ya Muhimbili – Mlonganzila imeweza kufanya upasuaji kwa watanzania wasiopungua 150 ambao wameweza kufaidika na huduma hiyo.

Mkuu wa Idara ya Upasuaji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili - Mlonganzila Dk Erick Muhumba amesema huduma ya upasua...
10/11/2023

Mkuu wa Idara ya Upasuaji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili - Mlonganzila Dk Erick Muhumba amesema huduma ya upasuaji wa kurekebisha miili inaanza Disemba mwaka huu. Mloganzila wamechelewa kuanza huduma hii kutokana na mtaalamu kutoka Afrika Kusini kuchelewa kufika nchini.

Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when The Afya Post posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share