27/12/2025
Mtu mmoja amefariki dunia na wengine 26 kujeruhiwa kufuatia ajali kubwa iliyohusisha magari 56 kwenye Barabara ya Kan-etsu Expressway mkoani Gunma, kaskazini magharibi mwa Tokyo, mapema leo Disemba 27.
Polisi walisema ajali ilianza baada ya kugongana kwa malori mawili mjini Minakami, hali iliyosababisha foleni ndefu. Moto ulizuka mwishoni mwa foleni na kuteketeza zaidi ya magari kumi, na ulizimwa baada ya saa saba.
Ajali hiyo ilitokea huku kukiwa na onyo la theluji nzito wakati wa likizo za mwisho wa mwaka mpya.
Written by