11/12/2024
Watanzania waishio Nchini China (DITAG) kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania Nchini China, pamoja na ofisi ya Konseli kuu ya Tanzania, jijini Guangzhou, China siku ya tar 8 kuamkia 9 Disemba 2024 wamesherehekea sikukuu ya Uhuru wa Tanzania bara kipekee kwa kualika mataifa mengine kuungana nao.
Sherehe hizo zilihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Mataifa mengine wanaoziwakilisha nchi zao Nchini China k**a Mabalozi kutoka nchi za Russia, Marekani, Iran, Iraq, Nepal, India, Turkey, n.k huku nchi za Afrika zikiwakilishwa na Mabalozi kutoka Zambia, Uganda, Mali, Nigeria, Congo, n.k
Aiza mgeni rasmi kwenye sherehe hizo Alkuwa ni MH. Balozi wa Tanzania Nchini China Balozi Khamis Musa Omary na kuhudhuriwa na makampuni mbalimbali ya Watanzania nchini China pamoja na Wanafunzi, Wafanyakazi na Wafanyabiashara kutoka majimbo yote 31 nchini China.
Katika Sherehe hizo Muwakilishi kutoka Shirika la Ndege la Air Tanzania Nchini China Ndg. Josephat Kagirwa nae alkuwepo, sambamba na Watu maarufu kutokea Tanzania k**a Irene Uwoya, Juma Lokole, DJ Romy Jones, Salma Jabu Nisha, Leonard Kachebonaho Wa UVCCM, nk
Hashtag ya Sherehe hizo ilkuwa na ujumbe wa ikiunga mkono kauli mbiu ya mwaka huu ya uhuru inayosema “Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania bara, uongozi madhubuti, na ushirikishwaji wa Wananchi, ni msingi wa maendeleo yetu” •