Maokoto News

Maokoto News Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Maokoto News, Digital creator, Dar es Salaam.

karibu katika official page ya MAOKOTO NEWS sehemu pekee utakayo pata fursa ya kujifunza , kuburudika na matukio tofauti ya wasanii,taifa,filam,mpira, music,pamoja na habari za ngumi za kulipwa na habari nyingine kede

Alipita JKT Tabora Msange 2014 baada ya form 6. Degree na Master akasoma UDSM tena akiwa chuoni akaanza kurekodi nyimbo ...
01/05/2025

Alipita JKT Tabora Msange 2014 baada ya form 6. Degree na Master akasoma UDSM tena akiwa chuoni akaanza kurekodi nyimbo zake za Hip Hop na bado akawa mshindi wa tafiti bora UDSM 2020/21. Msanii msomi Claudia Lubao “Chemical” amehitimu PhD yake Chuo Kikuu cha St Andrews Scotland.

26/04/2025

Afande kafika mbali sasa

Ulikuwa mzigo wa mke wake. Kwakuwa kampuni ya usafirishaji haikusema mzigo utafika lini na saa ngapi, mke hakuwepo mume ...
05/04/2025

Ulikuwa mzigo wa mke wake. Kwakuwa kampuni ya usafirishaji haikusema mzigo utafika lini na saa ngapi, mke hakuwepo mume akaupokea.

Kichwani kajiambia, "sisi ni mwili mmoja"
Akafungua kwa shauku na uchangamfu mkubwa. Akili ilimwambia, "mkeo itakuwa kakununulia zawadi nzuri baada ya wewe kumzawasia gari siku chache zilizopita"

Masikini macho yake!
Butwaa ikawa salamu ya kwanza ya ubongo wake. "Huyu mwanamke anataka nini hapa duniani? Ina maana simridhishi au hajaamua kuridhika na mimi?

Yuko njiapanda sasa, hajui aelekee kwenye "kujilaumu" au kwenye "kumlaumu mke!

Kwawewe ungefanya nini?

Habari kamili icheki YouTube Maokoto News
28/11/2024

Habari kamili icheki YouTube Maokoto News

Makamu wa Rais wa Equatorial Guinea, Teodoro Obiang Nguema Mangue amesema Serikali ya Nchi hiyo itawatimua kazini Maafis...
05/11/2024

Makamu wa Rais wa Equatorial Guinea, Teodoro Obiang Nguema Mangue amesema Serikali ya Nchi hiyo itawatimua kazini Maafisa na Watumishi wote wa Umma ambao ni miongoni mwa Wanawake zaidi ya 400 waliorekodiwa wakifanya mapenzi na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kitaifa la Upelelezi wa Fedha (ANIF) la Nchini humo, Baltasar Ebang Engonga (54) katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye Ofisi za Serikali na nyumbani kwa Ebang.

Ebang ambaye ni Baba wa Familia ya Watoto sita, tayari amek**atwa kwa kosa la kujirekodi akiwa anafanya mapenzi na Wanawake hao ambao wengine ni Wake za Watu akiwemo Mke wa Kaka yake, Binamu yake, Dada wa Rais wa Nchi hiyo, Mke wa Mkuu wa Ulinzi wa Rais wa Nchi hiyo, Mke wa Mwanasheria Mkuu wa Nchi hiyo na Mtoto wa Mkuu wa Jeshi la Polisi la Nchi hiyo.

Wengine walioonekana wakifanya mapenzi na Ebang kwenye video hizo ni Mke wa Mlinzi wake (Bodyguard), Mke wa Mchungaji wake, Wake wa Mawaziri kadhaa wa Nchi hiyo, Mke wa Mjomba wake ambaye ni Mjamzito, Marafiki 15 wa Mdogo wake wa k**e na Wanawake wengine mbalimbali ambapo imeelezwa wote hao walionekana kuridhia video hizo kurekodiwa

Ebang Engonga ni Mkurugenzi Mkuu Shirika la ANIF ambalo ni Shirika la Kitaifa la Upelelezi wa Fedha la Equtorial Guinea linalohusika na kusimamia uchunguzi wa kifedha na kusimamia shughuli zinazolenga kudhibiti ufisadi wa kifedha Nchini humo.

ALIYE JIREKODI AKIMKASHIFU NA KUCHOMA PICHA YA RAIS AHUKUMIWA MIAKA MIWILI JELAMahak**a ya wilaya ya Rungwe jana julai 4...
05/07/2024

ALIYE JIREKODI AKIMKASHIFU NA KUCHOMA PICHA YA RAIS AHUKUMIWA MIAKA MIWILI JELA

Mahak**a ya wilaya ya Rungwe jana julai 4. 2024 imemtia hatiani Bw. Shedrack Yusuph Chaula mwenye umri wa miaka 24 kutumikia kifungo cha miaka miwili (2) gerezani au kulipa faini ya shilingi millioni 5 kwa kosa la kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni kwa mujibu wa kifungu cha 16 cha sheria ya makosa ya mtandaoni 2015.

Akisoma hati ya mashtaka mwendesha mashtaka wa serikali Rosemary Mgeniji mbele ya hakimu mkazi mkuu wa mahak**a ya wilaya ya Rungwe Mh. Ramla Shehagiro ameeleza kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo 22/6/2024 katika kijiji cha Ntokela wilayani Rungwe mkoani Mbeya.

Imeelezwa mahak**ani hapo na mwendesha mashtaka kuwa mshtakiwa huyo akiwa dukani kwake maeneo ya Ntokela alirekodi ujumbe wa video wenye maneno“Kwakua umeshindwa kutetea taifa lako lisiathirike na ushoga hii video inakuhusu wewe na si mtu mwingine” huku akijua kuwa taarifa hizo ni za uongo zenye kupotosha jamii.

Alipopewa nafasi ya kujitetea mahak**ani hapo mtuhumiwa huyo Bw. Shadrack Chaula mkazi wa Ntokela amesema yupo tayari kutumikia adhabu yoyote atakayopewa na mahak**a hiyo.

Upande wa jamhuri ukiongozwa na mawakili wa serikali Veronica Mtafya na Rosemary Mgeniji umeiomba mahak**a itoe adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine kwani kitendo hicho kimetafsiriwa k**a udhalilishaji kwa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akitoa hukumu hakimu mkazi mkuu wa mahak**a ya wilaya ya Rungwe Ramla Shehagiro amesema kwa mujibu wa sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015 kifungu cha 16 amemtia hatiani kwenda gerezani kutumikia kifungo cha miaka miwili au kulipa faini ya shilingi milioni tano (5).

Hata hivyo mtuhumiwa amepelekwa gerezani kwenda kutumikia kifungo baada ya kushindwa kulipa faini.

04/07/2024

KABLA YA KUWA CHAMPION ALIKUWA DANCER NA NDIO MWALIMU WA ANGEL NYIGU 😂😂😂 ILA MANDONGA MUNGU ANAKUONA.......... Angel Nyigu NJOO UMCHUKUE MWALIMU WAKO

23/05/2024

Kaoneka na mandonga wakutana live na kutaka kuzichapa #

Hapo ni Urambo Tabora na huyu ni Nyoka aina ya Koboko aliyeuliwa na wakulima. Koboko ndiyo nyoka hatari kuliko nyoka wot...
26/03/2024

Hapo ni Urambo Tabora na huyu ni Nyoka aina ya Koboko aliyeuliwa na wakulima. Koboko ndiyo nyoka hatari kuliko nyoka wote hapa duniani na hii ni kwa sababu ya mkusanyiko wa sumu kali alionao, nyoka huyu ana aina mbili za sumu ambazo hufanya kazi kwa pamoja na endapo mtu atang’wata basi ndani ya dakika 3 hadi 10 mtu huyu akikosa matibabu hupoteza maisha.

Nyoka hawa huwa na maeneo maalumu ya kung’ata ambayo ni kichwani, shingoni au kifuani kwani mara nyingi hukaa juu ya mti, na ukiwakuta chini urefu wao ni futi 16 na akiwa na hasira husimama nusu mwili wake ambapo ni sawa na futi 8.

Wataalamu wanashauri jinsi ya kumuua ni kuchemsha chungu cha maji ya moto au uji kisha kujitwika kichwani na kupita maeneo ambao wanapatikana nyoka hawa, wakitaka kung’ata katika maeneo yao huishia kudumbukia ndani ya chungu hiko chenye kimiminika cha moto, hufa.

Lakini pia nyoka huyu unaambiwa anauwezo wa kutembea mwendo kasi mkubwa sana ambapo anaweza kukimbia 23km hadi 25km ndani ya saa moja, huku binadamu wa kawaida ana uwezo wa kukimbia 12km ndani ya saa moja na endapo mnyama huyu ataamua kung’ata sehemu yenye kundi kubwa la watu basi anauwezo wa kung’ata kunzia watu/wanyama 70 nakuendelea bila kuchoka.

Hapa nchini kwetu nyoka aina hii hupatikana kwa wingi mkoani Tabora na sehemu zenye misitu mikubwa k**a vile, Iringa, Morogoro, Milima ya Udzungwa huko wapo wegi sana.

Pia nyoka aina hii hutajwa katika orodha ya wanyama wanaoongoza kuuwa watu wengi zaidi duniani.

Na unaambiwa nyoka huyu akiwa msituni hapendelei kusikia kelele au milio ya gari na mara nyingi endapo atasikia mlio wa gari hupendelea kuufuatilia mlio huo nakufanya shambulio hivyo inashauriwa kufunga vizuri vioo vya magari wakati wa kupita msituni.

Na wataalamu wanashauri kuwa endapo nyoka huyu atakuwa amejificha katika upenyo wa gari basi ni vyema dereva kukimbiza gari hilo kwa mwendo kasi usiopungua 80 na kuendelea kwa ndani ya dakika 10 hadi 15 ili kusaidia kummaliza nyoka huyo kutokana na joto kali au kumchosha nyoka huyo na kumpunguzia makali ya sumu yake ya kudhuru watu.

Maokoto News ....

Huyu sio mbu yule mdudu bali ni micro camera (spy camera), inayong'ata k**a mbu yule mdudu wa malaria. Dunia inazunguka ...
04/01/2024

Huyu sio mbu yule mdudu bali ni micro camera (spy camera), inayong'ata k**a mbu yule mdudu wa malaria. Dunia inazunguka kwa speed sana. Kifaa hiki kinakung'ata k**a mbu anavyong'ata na kazi yake kubwa ni kuchukua sampuli za damu kwaajili ya DNA na mengineyo, au kinaweza kutumika kuchoma sindano ya sumu nk. Kinaweza kutumwa kutoka bara moja hadi lingine, kimng'ate yeyote nyumbani kwake na kisha kikaondoka na damu mpaka USA tayari kwa sampuli za DNA kwa shughuli zao. Kifaa hiko kimetengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu na kinachajiwa kikiwa mbali bila kuhitaji kisimame ndio kiunganishwe na umeme, Kinatumia muundo unaoitwa Inductive charging (also known as wireless charging), it uses an electromagnetic field to transfer energy between two objects through electromagnetic induction. Energy is sent through an inductive coupling to an electrical device, which can then use that energy to charge batteries or run the device. Katika ulimwengu huu mpya, hiki ndio kifaa hatari zaidi kwa ujasusi leo.

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limemtaka Msanii Whozu kushusha mara moja video ya wimbo wake wa ‘Ameyatimba’ kwenye d...
05/11/2023

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limemtaka Msanii Whozu kushusha mara moja video ya wimbo wake wa ‘Ameyatimba’ kwenye digital platform zote, pia limemtoza faini ya Tsh. milioni 3 na limemfungia kujishughulisha na kazi za sanaa kwa muda wa miezi 6 kuanzia leo November 04, 2023 kutokana na wimbo huo kuwa na maudhui yanayokiuka kanuni za maadili.

BASATA imesema Whozu alichapisha video ya wimbo huo Nov 02, 2023 akiwashirikisha wasanii wenzake Mbosso na Bill Nass, na kwamba wimbo huo una maudhui yanayokiuka kanuni za maadili kutokana na kuwepo ishara ya vitendo vinavyoashiria matusi kinyume na Kanuni ya 25(6) (j) pamoja na vitendo ya unyanyasaji, ukatili na udhalilisha wa utu wa Mwanamke kinyume na Kanuni ya 25(6)-(f).

“Msanii huyu ameshaonywa mara mbili na kutozwa faini mara moja huko nyuma kwa kukiuka taratibu za kuzingatia maadili katika kazi za sanaa lakini bado ameendelea kupuuza”

“Baraza la Sanaa la Taifa kupitia Sheria Na. 23 ya Mwaka 1984 na Marekebisho yake ya Mwaka 2019 ambayo inatoa Mamlaka kwa Baraza kusimamia Maadili ya msingi kwenye Sekta ya Sanaa kwa Kanuni ya 25(1)-(8) ya Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa za Mwaka 2018.

Baada ya Harmonize kualikwa na Diamond Platnumz kwenye Wasafi Festival na kukataa, ameandika kwamba ameshalewa na amebad...
26/10/2023

Baada ya Harmonize kualikwa na Diamond Platnumz kwenye Wasafi Festival na kukataa, ameandika kwamba ameshalewa na amebadili mawazo.

Harmonize amesema uenda wakaimba wimbo wao na Diamond Platnumz "Kwangaru" pamoja siku hiyo ikifika.

OKKY!!! Nishalewa nimeamua kuwa nitakuwa Mtwara!! Hakikisha unanunua tickets tukaijaze Nangwanda✌️ umesha imagine kwangwaru litapigwa pale live after 5 years." - Harmonize ameandika.
Maokoto News

Address

Dar Es Salaam
2782

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Maokoto News posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share