24/11/2025
Na Serengeti Media Centre.
Ukimshangaa mbuni asiyepaa utamstaajabu ngwini, samaki asiyepaa mwenye uwezo wa kuogelea.
Kawaida ukimkuta mbuni ndani ya hifadhini anavyovimba akiwa amejichanganya na pundamilia na nyumbu wakitafuta malisho unaweza kujisahaulisha kuwa huyu ni ndege.
Watu wengi wamekuwa wakimuona mbuni k**a ndege wa kipekee na wa tofauti basi k**a unaisoma hii makala utaweza kuujua utofauti.
1. Muonekano
Mbuni ndiyo ndege mrefu, mkubwa na mzito zaidi duniani, anaweza kuwa na wastani wa kilo 50 k**a mbuzi lakini pia ana uzito sawa na kuku 20 na ndiyo sababu kuu kwanini mbuni hana uwezo wa kupaa.
Sasa utajiuliza, kwanini kuku ni mwepesi lakini hapai juu angani k**a kunguru? Naomba huo uwe mjadala wa siku nyingine.
2. Mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
Mbuni ana matumbo matatu na ni ndege pekee ambaye haja zake ndogo na kubwa hutoka tofauti, yani hazijichanganyi.
Mbuni ni mnyama mrefu kuliko wanyama wengine duniani. Ana vidole viwili tu vya miguuni.
3. Mbio na kasi
Mbuni ana uwezo wa kukimbia kwa kasi ya kilomita 70 kwa saa, kasi kubwa kuliko ndege yoyote yule. Hivyo safari yake ya Dar kwenda Bagamoyo inaweza kumchukua saa moja tu. Hatua yake moja ni sawa na hatua tano za binadamu.
4. Vidole
Tofauti na ndege wengine wenye vidole vinne ambapo vitatu huangalia mbele na kimoja nyuma, mbuni ana vidole viwili kwenye mguu wake mmoja, vyote vinaangalia mbele.
5. Kujihami
Kwenye hatari, silaha kubwa ya mbuni huwa ni mateke yake, hurusha mateke ya mbele yenye uwezo wa kuua wanyama wakali k**a fisi, chui hadi simba.
6. Tabia za misimu
Katika msimu wa masika mbuni hukaa peke yake au na mpenzi wake na katika msimu wa kiangazi, mbuni hukaa katika makundi ya mbuni wengi hadi 50 na hupenda kujichanganya na makundi ya swala na pundamilia.
Wakati mwingine ndege hao hujichanganya na wanyama wengine k**a pundamilia na swala.
7. Mapenzi yao ni ya kipekee
Katika hichi kitengo, mbuni ana utaratibu wa kipekee sana. Kwanza jogoo la mbuni hupiga mabawa yake k**a anataka kupaa ikiwa ni ishara kwamba anatafuta mwenza.
Akishapata mwenza, wanaanza kutafuta malisho na anahakikisha anampeleka sehemu ambapo hakuna wanyama wengine na wanaendelea kutafuta malisho hapo huku wakizoeana tabia.
Baadaye jogoo la mbuni huanza tena kupiga mabawa kwa nguvu zaidi na kuzunguka akiwa ameyashusha na akiwa anadonoa udongo, ambapo jike la mbuni likishaona hizo ishara basi huchuchumaa na kurusu kupandwa.
8. Yai la mbuni ni bonge la yai
Mbuni zaidi ya mmoja huweza kutaga mayai yao kwenye tundu moja na kila mbuni ana uwezo wa kutofautisha mayai yake na ya mbuni wengine.
Yai la mbuni lina uzito wa zaidi ya kilo 1 na ukubwa sawa na n**i. Yai la mbuni bwana, unaweza kulikaangia chipsi sahani k**a tano hivi.
9. Jike na dume wote huatamia mayai
Jike la mbuni ana rangi ya kijivu na huatamia mayai mchana kwa sababu rangi yake hufanana na mchanga hivyo ni ngumu kuonekana, huku jogoo la mbuni lenye rangi nyeusi hutamia mayai usiku kwa sababu ni ngumu kuonekana gizani. Mayai ya mbuni huchukua siku 35 mpaka 45 kutotolewa.
10. Jicho kubwa sana
Jicho la mbuni linalingana na yai la kuku. Jicho la mbuni ni kubwa kuliko ubungo wake. Hivyo ana uwezo mkubwa sana wa kuona mbali na kwenye giza.
Mbuni ni mnyama asiyeonekana kirahisi kwa sababu idadi yao imepungua sana hivyo kuwaona ni mpaka mbugani, kwenye hifadhi.
Ukitaka kumuona mbuni basi tufunge safari moja kwa moja mpaka kwenye hifadhi za taifa za Serengeti, Mikumi, Ruaha au Katavi. Pia ukitembelea maeneo ya uhifadhi k**a Selous na Ngorongoro utaweza pia kujionea mbuni.