TanzaMwanga

TanzaMwanga Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from TanzaMwanga, Media/News Company, Dar es Salaam.

Kwa maelezo ya Mitandaoni wanasema kuwa huyu ndio mtoto mzuri zaidi Duniani, K**a unaamini kuna mtoto anayemzidi uzuri w...
10/04/2025

Kwa maelezo ya Mitandaoni wanasema kuwa huyu ndio mtoto mzuri zaidi Duniani,

K**a unaamini kuna mtoto anayemzidi uzuri weka picha yake bila filter tulinganishe!

BARUA YA WAZI KWA MWENYEKITI WA CCM TAIFA MH. SAMIA SULUHU HASSANYAH. MAONI YA KUBADILISHA UTARATIBU WA KURUDISHA MAJINA...
23/03/2025

BARUA YA WAZI KWA MWENYEKITI WA CCM TAIFA
MH. SAMIA SULUHU HASSAN

YAH. MAONI YA KUBADILISHA UTARATIBU WA KURUDISHA MAJINA MATATU

Mheshimiwa Mwenyekiti,

Husika na kichwa cha barua hapo juu

Kutokana na Idadi ya wananchi kuongezeka, Chama chetu pia kimeongeza Idadi ya wanachama wengi wenye sifa na uwezo wa kushika nafasi mbalimbali za Uongozi,

Lakini pia idadi ya wasomi nayo imeongezeka hivyo sasa hivi tuna rasilimali watu kubwa,

Idadi hii kubwa inapelekea pia kuwa na wanachama wengi wanaowania nafasi za Uongozi,

Hapo awali wanachama waliokuwa wakiwania nafasi za Uongozi walikuwa wachache na hata wengine walikuwa wakishawishiwa kuombwa kugombea hivyo ilikuwa ni rahisi kuchuja na kupata majina matatu ya wanachama watakaokwenda kupigiwa kura,

Lakini sasa hivi hali imebadilika
Imefikia hatua mamia na huenda hata maelfu ya wanachama wakajitokeza kuomba ridhaa ya kuwania nafasi za Uongozi hivyo si rahisi kwa majina matatu tu kutosha kumpata mtu sahihi anayestahili kuongoza na zipo sababu,

1) Jina la kwanza ni muhimu kupitishwa Kiongozi aliyepo madarakani ili atetee nafasi yake

2) Jina la pili ni muhimu kupitisha jina la mgombea kwa kuzingatia usawa wa Kijinsia (Gender)

Hivyo inabaki nafasi moja tu ya mgombea kwa hawa wanachama wote wanaogombea,

Kimsingi nafasi moja hii ni finyu mno kwa wanachama hususani wanachama wale wasio na Viongozi wanaoweza kuwasemea kwenye Vikao,

Si hivyo tu,
Kipindi cha Uchaguzi ni kipindi kizuri sana kwa Chama kuona vipaji vipya vya Uongozi,

Kupitia Chaguzi tunaona vipaji vya mikakati, vipaji vya maono, vipaji vya kusema kwa wanachama wanaogombea n.k

Hivyo ikiwa tutatumia utaratibu huu wa kurudisha majina matatu vipaji vyote hivi hatutaweza kuviona na huenda wengine wakakata tamaa na kuachana kabisa na Siasa na wengine wakahamia vyama vya Upinzani kutafuta fursa ya kugombea na kuwatumikia wananchi,

Utaratibu huu wa majina matatu utakifanya Chama kionekane ni cha watu wachache, familia chache watakaosemeana wenyewe kwenye vikao na wengine wajione sio sehemu ya CCM kwasababu ya kukatwa majina yao na kupitishwa wachache wanaojulikana na wanaotokea familia zinazojulikana hivyo itapelekea Chama kupunguza Idadi kubwa ya wafuasi na wanachama ambao watatafuta fursa katika vyama vingine,

Utaratibu huu wa majina matatu unaondoa haki ya mwanachama ya Kuchagua na kuchaguliwa,

Kwasababu wajumbe wanaweza kuletewa majina matatu ya wanachama ambao si chaguo lao,
Hivyo haki yao ya kuchagua itakuwa imepokwa,

Vilevile pia wanachama watakaokatwa majina yao watakuwa wameondolewa haki yao ya Kikatiba ya kuchaguliwa,

Utaratibu huu wa majina matatu unakwenda kuminya Demokrasia ndani ya Chama kwasababu utazuia wanachama wengine kuonekana, kupata fursa ya kugombea na kupata fursa ya kumchagua Kiongozi wanayemtaka,

Utaratibu huu wa kurudisha majina matatu unapunguza nguvu ya maamuzi ya wanachama na kuvipa vikao nguvu ya kuwaamulia na kuwachagulia wanachama Viongozi wao,

Utaratibu huu wa majina matatu unaua Vijana na vizazi vijavyo vya kisiasa kwasababu kwa kiasi kikubwa hivi havijulikani na vikao vya maamuzi bali vinapambana kutafuta kuonesha vipawa vyao,

Kipindi cha Uchaguzi ndicho kinakuwa kipindi kizuri sana kwa kizazi hiki kipya kuonekana hivyo utaratibu wa majina matatu unakwenda kukizika rasmi kizazi hiki kisionekane,

Siasa ni mchezo wa fitna
Viongozi waliopo madarakani pia nao wanaweza wakafanya fitna ili wanachama wenye nguvu wasipitishwe kugombea nao,

Hili tumelishuhudia maeneo mengi ambapo inafikia hatua wanachama wanaamua kumchagua mtu dhaifu ilimradi tu wamuondoe Kiongozi aliyepo madarakani,

Siasa ni uwekezaji wa muda mrefu wa hali na mali hivyo ikiwa hawa wanachama waliowekeza kwa wananchi wao kisha wakaja kukatwa majina yao lazima itakwenda kuhatarisha mno Uhai wa chama na kupelekea mipasuko mikubwa kwenye Chama,

Tuutumie Uchaguzi wa mwaka 2015 k**a rejea lilipokatwa jina la Mh. Edward Lowassa ilipelekea kuwepo na mpasuko mkubwa ndani ya Chama,

Tumeona huko nyuma,
Wanachama wanapoletewa majina ambayo sio machaguo yao waliamua kushirikiana na vyama pinzani kukihujumu chama,

Tumeona kuna wanachama ambao walikuwa Viongozi wazuri lakini walipokatwa walikwenda Upinzani na hatimaye tukapoteza Chaguzi mbalimbali,

Ili yasitokee haya ni vema chama kikatafakari upya kuhusu mfumo huu wa majina matatu,

Naomba ikikipendeza Chama kiongeze majina walau yawe kumi (10) kutokana na wingi wa wanachama wanaoomba kuwania nafasi za Uongozi,

Ama chama kikiona inafaa kipitishe wanachama wote kugombea kisha vikao viamue kuhusu majina matatu miongoni mwa wanachama watakaoongoza kwa kura,

Uchaguzi wa mwaka 2020 binafsi niliwania Ubunge kura hazikutosha nilikuwa mtu wa tatu kwa kura,

Lakini k**a ungekuwa utaratibu wa chama kuleta majina matatu naamini kwa asilimia zaidi ya mia moja jina langu lisingepitishwa na wala lisingedhaniwa k**a ni jina ambalo linaweza kuleta ushindani na kuwa watatu kwa kura,

Utaratibu huu wa majina matatu umetukatisha tamaa na kuturudisha nyuma wanachama wengi tulio na nia ya kuwania nafasi mbalimbali za Uongozi,

Kwa kuwa chama chetu ni sikivu na kinajali mno wanachama wake na kinafanya Siasa kulingana na wakati,

Ni matumaini yangu makubwa kuwa maoni haya yatazingatiwa na marekebisho yenye tija yatafanywa kwa ajili ya kuboresha na kukiimarisha chama chetu!

Wako katika ujenzi wa Chama cha Mapinduzi na Taifa la Tanzania

IBRAHIM JEREMIAH

SARE ZA CHAMAJipatie sare za Chama kwa bei rahisi ■Bendera za kushika mkononi Jumla 400■Bendera za Mashina/Mabalozi 2,50...
12/02/2025

SARE ZA CHAMA

Jipatie sare za Chama kwa bei rahisi

■Bendera za kushika mkononi Jumla 400
■Bendera za Mashina/Mabalozi 2,500
■Bendera za Matawi 6,000
■Kofia Jumla 5,000 tu
■Skafu Jumla 8000 tu
■Tshirts Jumla 12,000 tu
■Mashati Jumla 20,000 tu

Tupo Mtaa wa Kariakoo
Tunatazamana na Ofisi ya CCM Mkoa wa Dar es salaam,

Mikoani tunatuma

Kwa mawasiliano piga
0767 896789
0769896751

Zamu ya MwanzaKilele cha mbio za mwenge 14/10/2024
12/10/2024

Zamu ya Mwanza
Kilele cha mbio za mwenge 14/10/2024

Nautafakari uzee!Umeishi miaka mingi Umeona mengi, umepitia mengi,Yapo uliyofaulu na yapo ambayo hukuweza kuyafanikisha,...
03/03/2024

Nautafakari uzee!

Umeishi miaka mingi
Umeona mengi, umepitia mengi,
Yapo uliyofaulu na yapo ambayo hukuweza kuyafanikisha,

Unatazama mazingira uliyoishi ukiwa mdogo huyaoni, mazingira yamebadilika kutokana na mabadiliko ya Kimaendeleo,

Pale palikuwa na miti mlikuwa mkichuma Matunda,
Pale mlikuwa mkicheza, pale mlikuwa mkikutana, pale mlikuwa mnasoma, pale palikuwa kwa baba, babu, bibi, mjomba, shangazi, jamaa na jirani lakini pale si kwao tena na wengi wa hawa watu hawapo tena, walikwishafariki Dunia,

Ulikuwa na ndugu, marafiki na jamaa lakini mkatawanyika kutafuta maisha sehemu mbalimbali katika Dunia,

Wengine walifanikiwa na Wengine hawakuweza kufanikiwa

Ulikuwa na uliosoma nao
Lakini Mkatawanyika kila mahali Duniani
Wengine mnakumbukana lakini mlishahauliana,

Ulikuwa mtoto, ukawa kijana
Na muonekano mzuri na mavazi mazuri ya kipindi hicho lakini sasa hivi ngozi ya mwili imesinyaa, nywele zimekuwa na Mvi,

Yale mavazi uliyokuwa unayaona ni ya kisasa kwa zama hizi yanaoonekana ni mavazi ya zamani, zile nyimbo ulizokuwa ukizipenda nazo zimekuwa za kizamani,

K**a ulibahatika kujenga basi hata Nyumba itaonekana ni ya kizamani Dunia inakuja na mabadiliko ya kimaendeleo kila wakati,

Watu wengi uliokuwa nao karibu wamekwisha aga Dunia, wamefariki,

Wengine una namba zao za simu lakini
Kila siku unaumia kuzifuta namba zao kwasababu wameshafariki na kila siku wanazidi kuendelea kufariki, ardhi haichoki kumeza watu, kila siku ni ni safari za kwenda kuzika,

Nguvu nazo zimepungua, akili nayo haifanyi kazi k**a ilivyokuwa ikifanya kazi zamani, homa za mara kwa mara (homa za uzee) nazo hazitaki kukuachia nafasi,

Unaishi kila siku ukimeza Dawa na kuhitajika Hospitali mara kwa mara na ukienda Hospitali haupokelewi k**a vile ulivyokuwa ukipokelewa ujanani, kwasababu unaenda Hospitali za kawaida ili kumudu gharama lakini pia unahitaji kupata huduma za bure za wazee,

Maisha yako sio yale tena,
Ulikuwa ukihudumia na kusaidia watu lakini sasa hivi umekuwa ni muhitaji, umekuwa mtu wa kuhitaji msaada wa kulelewa na kuuguzwa,

Huenda hata mwenzi wako wa maisha mke/mume mliyekuwa mkiishi na kufarijiana pamoja naye amekwishafariki,

Huenda hata baadhi ya watoto wako mwenyewe ambao hukutamani kuona wanakuacha Duniani lakini nao wamefariki,

Kuzika mtoto/watoto kunauma,
Na maumivu yake yanajirudia kila unapokumbuka,

Huenda uzee umekuja na ulemavu,
Huoni tena, hutembei, husikii vizuri, husemi vizuri ama umepata ugonjwa wa akili na magonjwa mengineyo,

Kila ukitazama mbele unaona ya kuwa siku zako za kuwepo hapa Duniani si nyingi, unaishi ukijua kuwa muda wowote unaweza kufa kwasababu wengi waliokuzunguka wamekufa,

Kila kitu ulichonacho unakiacha,

Watoto, mke, ndugu, marafiki, mali na vyote vizuri na vya thamani kwako unaviacha, unakwenda usikowahi kukujua wala kukuona, mwisho wa maisha yako,

Fikra hii inapokaa kichwani inaumiza sana!

Nimeutafakari uzee mara kadhaa lakini leo nikasukumwa kuandika ili ulimwengu ujue wazee wetu wanakuwa katika hali gani,

Iweni na Jumapili njema,
BWANA YESU awabariki na kuwalinda!

Ndugu yenu
IBRAHIM JEREMIAH

*TAHADHARI*UBUNGO COMMERCIAL AND LOGISTICS CENTER NI BOMU LINALOKUJA KUUA WAFANYABIASHARA WAZAWAHuenda dhamira ilikuwa n...
29/02/2024

*TAHADHARI*

UBUNGO COMMERCIAL AND LOGISTICS CENTER NI BOMU LINALOKUJA KUUA WAFANYABIASHARA WAZAWA

Huenda dhamira ilikuwa ni njema, sina shaka na hili kwasababu tunatamani nchi yetu iwe kitovu cha Biashara Barani Afrika,

Ujenzi wa Kituo cha Biashara hususani Biashara kati ya China na Tanzania unaoendelea Ubungo huenda ukaja kuleta balaa nchini,

Waswahili wanasema wasiwasi ni akili,

Naam,
K**a wasiwasi ni akili na mimi nikaona wasiwasi wangu si mbaya kwasababu wahenga walisema

"Kunguru mwoga huishi miaka mingi"

Lakini pia tunajifunza kutokana na kufuatilia historia na kuangalia kwa wenzetu pia,

Endapo ujenzi huu ungewapa kipaumbele wafanyabiashara na wawekezaji wa ndani nadhani mashaka yangu yangepungua kwa kiasi kikubwa,

Lakini mashaka yangu yanaongezeka ninapoona kuwa mradi huu unaonesha kugusa zaidi watu wa nje hususani ndugu zetu Wachina,

Naomba mniwie radhi nikiandika hawa ndugu zetu ni wa kufanya nao Biashara lakini si watu wazuri wanaopaswa kujua siri zako k**a masoko yako n.k

Kwa Wafanyabiashara ambao wamewahi kufanya nao Biashara wananielewa kiundani na wataungana nami kuwa hawa watu wakiona unafanya Biashara sana huwa wanaanza kupeleleza kujua ulipo, wateja wako na masoko yako ili waje wawekeze na kuchukua ile ridhiki yako,

Huenda mkadhani ni masihara lakini wenzetu ukifanya nao Biashara wakiona unapata watatafuta kila namna ili wakuzunguke wafungue Tawi eneo ulilopo ili wachukue wateja wako,

Hata hawa Wawekezaji wengi wa Kichina waliopo hapa kabla walikuwa wasambazaji wa bidhaa kwa Wafanyabiashara wa hapa, walipoona mzunguko wao ndipo nao wakaamua waje na kuteka Biashara moja kwa moja,

Nina hofu sana kuwa Ubungo huenda yakatokea haya,

Ubungo itaua Masoko yote makubwa ya Tanzania ambayo kwa kiasi kikubwa ndio masoko ya Watanzania wazawa,

Hawa wazawa hawataweza kuhimili Ushindani wa Wachina wenye Viwanda na Uchumi mkubwa kitu ambacho kitapelekea Biashara za Watanzania kuanguka, mapato ya nchi kushuka na Uchumi wa nchi kumilikiwa na Wageni,

Mtanzania akinunua bidhaa kwenye nchi zao hawezi kuuziwa kwa bei sawa na wao wenyewe hivyo hawa watu hawataweza kushindana,

Hili ni la kweli na la hakika, unaweza ukalichukua na ukalihifadhi kwa kumbukumbu za baadae.

Mambo haya sio Mageni kwasababu yalitokea na yanaendelea kutokea,

Tunaona Raia wengi wa kigeni wakifanya shughuli ambazo zinatakiwa zifanywe na Watanzania,

Tuliona raia wa Kigeni wakipanga mpaka Maua Barabarani, tunaona wanachanganya Rangi za Magari Kariakoo na wanauza robo Lita elfu 10,

Hivi mnakumbuka maandamano na vurugu zilizotokea Kenya na kuwafukuza Wachina kwenye jengo la *China Square*?

Wachina walikuwa wanafanya Biashara ndogo na kuuza bidhaa kwa bei ya China,

Wateja wakakimbilia China Square wakaacha kununua bidhaa kwenye maduka ya Wakenya,

Jambo hili lililopelekea Biashara nyingi za Wakenya kudorora hivyo Wafanyabiashara Wakenya wakaanzisha Maandamano na vurugu na kutaka China Square ifungwe,

Na kweli China Square ilifungwa na Serikali ilibadilisha taratibu zilizosaidia kuwalinda Wafanyabiashara wazawa,

Kwa hali ninayoiona hivi sasa sidhani k**a tumejipanga vema kulipokea jambo hili,

Sidhani k**a tumeangalia athari zake kwa Wafanyabiashara wa ndani,

Sidhani k**a tumeangalia athari zake kwa Masoko ya Tanzania,

Sidhani k**a tumeangalia athari zake kwenye Uwekezaji wa ndani,
Waliojenga Majumba Kariakoo na kwenye Masoko mengine,

Sidhani k**a tumeangalia athari zake kwenye pato la Taifa kwasababu wawekezaji toka nje watakuja kuchukua Pesa zetu na kuondoka nazo,

Sidhani k**a tumeangalia athari zake kwenye taasisi zetu za kifedha kwasababu hawa Raia wa Kigeni wana Benki zao, hawa Watanzania wanakopa kwenye Mabenki hivyo uwekezaji huu utayumbisha taasisi hizi za kifedha kwasababu Biashara kwa Watanzania itashuka, thamani ya Nyumba kwenye masoko mengine itashuka n.k

Sidhani k**a tumeangalia athari za hawa watu kujua masoko yetu ya nchi jirani k**a Congo, Zimbabwe, Zambia, Malawi, Comoro, Uganda, Burundi n.k

Asili ya hawa watu wakishayajua masoko yako huwa wanataka kwenda kuwekeza kwenye masoko yako ili wewe usipate kabisa wateja,

Vipi k**a wakienda kuwekeza moja kwa moja Congo, Zambia, Zimbabwe, Malawi, Burundi, Comoro n.k?

Sisi Watanzania tutakuwa na nini?
Tutabaki na Majengo ya Ubungo bila Biashara ama ndio tutaona umuhimu wa wawekezaji wa ndani ama tutasaini nao Mkataba wa kutofanya Biashara k**a hii kwenye nchi nyingine Barani Afrika,

Nina mashaka
Sina Imani na hawa wageni,

Ndugu wa kweli ninayemwamini ni Mtanzania mwenzangu ambaye hatoweza kuchepusha maendeleo na mafanikio sehemu nyingine tofauti na Tanzania,

Naomba sana Viongozi, Wadau na Watanzania kwa ujumla tuliangalie hili suala upya na kwa undani sana,
Lisije likatuletea balaa huko mbeleni!

Ushauri wangu ni kuwapa kipaumbele Watanzania kufanya Biashara Ubungo kwa masharti ya kuweka bei za chini mno kwa bidhaa watakazouza na kuuza kwa Idadi kubwa pekee!

Ndugu yenu
*IBRAHIM JEREMIAH*

18/02/2024

Kipaji

TOYOTA SPACIO Year of make:2002Engine Capacity: 1490ccColor: Blue Mileage:40,231kmDrive system 2WDTransmission Automatic...
08/05/2023

TOYOTA SPACIO
Year of make:2002
Engine Capacity: 1490cc
Color: Blue
Mileage:40,231km
Drive system 2WD

Transmission Automatic
Reverse Camera
Parking Sensor
New Tyres and Sportsrims
Immaculate air condition

Fuel Petrol ⛽️
Imported from Japan
Airbags
Air Condition
Full documents
Full duty paid

Free Registration
Accessories:
Jack + handle
Wheel 🔧

PRICE: 16.9M

Exchange Allowed.

Wasiliana nasi
0758 376 623 / 0623 376 623

TOYOTA ALLEXYear of make:2003Engine Capacity: 1490ccColor: silver Mileage:40,281kmDrive system 2WDTransmission Automatic...
07/05/2023

TOYOTA ALLEX
Year of make:2003
Engine Capacity: 1490cc
Color: silver
Mileage:40,281km
Drive system 2WD

Transmission Automatic
Reverse Camera
Parking Sensor
New Tyres and Sportsrims
Immaculate air condition

Fuel Petrol ⛽️
Imported from Japan
Airbags
Air Condition
Full documents
Full duty paid

Free Registration
Accessories:
Jack + handle
Wheel 🔧

Exchange Allowed

Wasiliana nasi
0758 376 623 / 0623 376 623

21/04/2023
Miaka ya 1970, North Korea waliagiza Magari ya Volvo 1,000 toka nchini Sweden, Magari yakasafirishwa na kukabidhiwa, Cha...
21/04/2023

Miaka ya 1970,
North Korea waliagiza Magari ya Volvo 1,000 toka nchini Sweden,

Magari yakasafirishwa na kukabidhiwa,

Cha kushangaza North Korea walikataa risiti za malipo ya Magari na wakakataa kulipa kabisa,

Mpaka leo North Korea wana deni la Dola Milioni mia tatu na thelathini ($330Millions) Sweden kwa ajili ya Magari hayo,
ambapo wameweka rekodi katika historia ya kufanya wizi mkubwa wa Magari kupata kuwahi kutokea Ulimwenguni!

Mtu mtata anapotaka kufanya Biashara nawe muombe alipie kabisa,

Utamdai vipi mtu Mtata mwenye Mabomu ya Nyuklia?

Utak**ataje mali zake?😅

Leo asubuhi nilitumiwa ujumbe kuwa nimetumia asilimia 75 ya kifurushi changu cha Internet, maana yake ni kuwa nimebakiwa...
18/04/2023

Leo asubuhi nilitumiwa ujumbe kuwa nimetumia asilimia 75 ya kifurushi changu cha Internet, maana yake ni kuwa nimebakiwa na asilimia 25 ya Kifurushi changu,

Nilikuwa na kifurushi cha Internet chenye Mb 490, Asilimia 25 ya Kifurushi ni sawa na Mb 123,

Cha ajabu nikaingia Kudownload Video moja yenye Mb 10, Video imekwama kudownload kwenye Mb 2.9,

Nikashtuka
Inakuwaje Kifurushi chenye Mb 123 kishindwe Kudownload Video yenye Mb 10,

Nikajiuliza sana ikanibidi niandike ili kuhoji,
Asubuhi nikajiunga kifurushi kingine ambacho kiliisha mida ya saa saba,

Saa 13:15 nilijiunga kifurushi kingine cha elfu moja chenye MB 490, Nikaingia Facebook kwa dakika chache kisha nikapigiwa Simu,

Nilipomaliza kuzungumza kwenye Simu na kuingia Online nilitumiwa ujumbe kuwa kifurushi changu cha Internet kimeisha,

Yaani nimejiunga kifurushi hiki cha Internet saa saba na robo na kimeisha kabla ya dakika 30 na sijatazama video wala kudownload kitu chochote,

Pia Applications nilizonazo kwenye Simu niliset hazijiupdate na niliondoa Auto download,

Huu ni wizi wa waziwazi tunaibiwa,

Kifurushi cha shilingi elfu moja chenye Mb 490 kinaisha hata dakika 30 hazijapita, hii ni haki jamani?

Kwa maana rahisi ni kuwa,
Itahitaji tununue kifurushi cha Internet cha elfu 48 ili tuweze kutumia ndani ya siku moja tu,

Gharama ya vifurushi vya Internet Tanzania imekuwa kubwa mno kwasasa kuliko hata gharama za vifurushi katika Mataifa makubwa k**a Marekani, China na Uingereza ambapo wao wanalipia Bili kwa mwezi,

Tunaiomba Serikali itusaidie kwenye hili ili watumiaji pia tuweze kujua matumizi yetu halali,

Haiwezekani muuzaji wa vifurushi akawa anajua matumizi wakati mnunuaji na mtumiaji hajui,

Muuzaji akisema kifurushi kimekwisha ndio kimekwisha hivyo, mtumiaji hana pakulalamika na hakuna hatua zozote zinazochukuliwa dhidi ya hii Mitandao ya Simu,

Kuna siku nyingine nilikuwa nimetoka kujiunga na kifurushi cha Internet, dakika 10 mbele nikatumiwa ujumbe kifurushi kimekwisha,

Nikasema wasinitanie
Nikawapigia Simu wakaniambia kifurushi bado kipo nizime Simu kisha niiwashe tena,

Huu ni wizi wa waziwazi kwa watumiaji wa Mitandao

Ushahidi ni huu hapa chini kwenye picha.

Share tafadhali

Ili ujumbe uzifikie mamlaka husika na Serikali ili hatua ziweze kuchukuliwa

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA Halotel Tanzania

Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when TanzaMwanga posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share