19/07/2025
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Ernest Sungura amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mabaraza ya Habari Duniani (WAPC) na pia Makamu Mwenyekiti wa Mabaraza ya Habari ya Afrika Mashariki (EAPC).
Akitoa pongezi kufuatia uchaguzi huo, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile amesema uchaguzi huu si tu ni heshima kwa Sungura binafsi, bali ni uthibitisho wa mchango mkubwa wa Tanzania katika uendelezaji wa taaluma ya habari duniani.
“TEF inatambua juhudi na uongozi mahiri wa Sungura uliosaidia kujenga misingi ya ushirikiano wa kikanda na kimataifa kupitia jukwaa la Mtandao wa Mabaraza Huru ya Habari Afrika (NIMCA), na sasa amepanda kwenda WAPC. Tunathamini mchango wake katika kukuza mazingira wezeshi kwa uhuru wa habari, uwajibikaji na weledi katika sekta ya habari,” amesema Balile katika barua ya pongezi.
Mhariri | John Mbalamwezi