10/12/2017
*NUKUU ZA NDG. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI, MWENYEKITI WA CCM NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWENYE MKUTANO MKUU WA 9 WA UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)*
Disemba 10, 2017.
Dodoma.
1. "Ni ukweli usiopingika kuwa, uhai na ustawi wa taifa lolote duniani ni vijana, hii inatokana na sababu moja vijana ni kundi kubwa" JPM
2. "Chama kinapokuwa na vijana wengi walio hamasika ndio usalama wa chama na taifa " JPM
3. "Napenda mfahamu ujana pekee haikufanyi uwe hazina ila ili uwe hazina inakupasa uwe mzalendo, muadilifu, nidhamu, utu, mchapakazi, mtii, mwenye kupenda kujielimisha na mwenye udhutu wakuleta fikra mpya na siyo kijana legelege".JPM
4. "Kijana ambaye ni mpenda rushwa, mwizi, fisadi, tapeli, mtumia madawa ya kulevya hana mchango wowote kwa taifa na hata kwa chama".JPM
5. "Uchaguzi huu ni muhimu sana kwa sababu Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) ni chombo muhimu sana katika chama". JPM
6. "Muelekeo wa Umoja wa Vijana tuliokuwa tunaujua, siyo muelekeo tulionao sasa".JPM
7. "Ni lazima wajumbe mlioko hapa mumtangulize Mungu mbele, na mtambue jukumu lenu kwa Vijana wote wa Tanzania".JPM
8. "Nitashangaa sana k**a leo mtaniletea Mwenyekiti aliyewahonga, kuwahonga ni kushusha thamani yenu, na ni dalili ya kuonesha hatokuwa kiongozi mzuri".JPM
9. "Mwenyekiti wa Vijana anayetakiwa ni mmoja tu, makabila ya watanzania ni zaidi ya 120 hamuwezi kuchagua kwa kabila na mkifanye hivyo hamtafanikiwa kupata kiongozi".JPM
10. "Mkachague viongozi waadilifu, wanyenyekevu, wachapakazi, wenye kuchukizwa na rushwa watawavusha. Ninyi muwaelekeze viongozi pakwenda siyo
wao wawaelekeze pakwenda".JPM
11. "Umoja wa Vijana limekuwa ni kundi la kuwazuia vijana wengine wasiingie, kila mwenye uwezo amekuwa akiwekewa vigingi vya kila aina". JPM
12. "Nawaomba Ndugu zangu vijana msitengeneze ukuta na vijana wenzenu taifa hili ni lenu wote". JPM
13. "Viongozi wakiwa wanyonge na wachini wanakuwa wanyonge zaidi, Vijana wa CCM niwaombe mjiamini mmekuwa wanyonge sana".JPM
14. "Ifike wakati viongozi wastaafu mrudi kwenye jumuia hii hata mfanye nao mikutano ya kuwahamasisha na kuwatia moyo". JPM
15. "Hii bodi ya Umoja wa Vijana iondoke bodi hii haitusaidii".JPM
16. "Viongozi mtakao wachagua na mliochaguliwa fanyeni tathimini ya mali za Umoja wa vijana ziwe kwenye daftari moja, hapo ndipo mtakuwa mnaweza kujitegemea". JPM
17. "UVCCM iwe sauti ya vijana, mtetezi wa vijana, kimbilio, chemchem ya fikra na chuo cha kuandaa vijana katika uongozi kwa chama na serikali "JPM
18."Chagueni wagombea wenye sifa na uwezo". JPM
19."Tuanzishe ukurasa upya wa Umoja wa Vijana nawapenda sana UVCCM nina wahitaji katika kuleta maendeleo ya Nchi yetu". JPM
20. "Na waahidi kila penye nafasi vijana hatutawasahau".JPM
21." Vijana muwe wenye kujenga hoja na msibweteke, anzisheni miradi tutawasaidia". JPM
22."Ukijituma watu watakuona tu".JPM
23. "Nataka Umoja wa Vijana wenye muelekeo wakushika dola".JPM
Imetolewa na,
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM).