AFYA BORA

AFYA BORA Your Health is our first priority

MAUMIVU YA KIUNO NA MGONGO NA SULUHISHO LAKEMaumivu ya mgongo ni ile hali ya kuhisi maumivu au kutojiskia vizuri/kawaida...
03/07/2024

MAUMIVU YA KIUNO NA MGONGO NA SULUHISHO LAKE

Maumivu ya mgongo ni ile hali ya kuhisi maumivu au kutojiskia vizuri/kawaida katika misuli au mifupa ya mgongo wako (eneo lililopo kati ya kiuno na shingo).
Maumivu haya yanatofautiana baina ya mtu na mtu na pia yanategemea sana wapi ilipo shida katika mgongo wako; nini kisababishi na kiungo kilichoathiriwa (kilichoumizwa/jeruhiwa).

Vivyo hivyo dalili nazo hutegemea na kisababishi na hivyo baadhi ya watu huwa na dalili zinazofanana huku wengine wakiwa na dalili za aina mbali mbali kuanzia mamivu ya mgongo, kushindwa kufanya shughuli za kawaida za kila siku kutokana na maumivu, homa na kutetemeka, kupungua uzito (hasa baada ya ajali/magonjwa ya mifupa), kupungua nguvu katika misuli ya miguu, miguu kuwaka moto/kuchomwa chomwa mithili ya sindano au miiba, ganzi kwenye miguu hadi kushindwa kumudu kuzuia haja ndogo na/au kubwa.

Aina kuu za maumivu ya mgongo:
Mara nyingi, maumivu ya mgongo hujitokeza katika aina kuu mbili ambayo ni:
(Maumivu yanayosambaa)

1. Maumivu yasiyohama (yapo katika eneo la mgongo husika hajalishi unafanya nini – localized pain). Mara nyingi maumivu ya namna hii ni yale yanayokuwa yametokana na kujeruhiwa kwa misuli/mifupa ya mgongo kwa ajali au kupigwa eneo la mgongoni. Au, ni yale yanoyotokanana mkao mbaya usiozingatia afya ya mgongo [anagalia mako mzuri katika somo “post” iliyopita –MKAO MZURI (NI UPI)?] hivyo kusababisha kuchanika kwa misuli ya ndani ya mgongo na kusababisha maumivu!!

2. Mamivu yanayosambaaa na kuangazia maeneo mengine ya mwili wako mbali na mgongo k**a vile miguu. Maumivu haya hutokana na mgandamizo katika mfumo wa fahamu/neva kutoka kwenye mifupa, uvimbe au kuumizwa kwa uti wa mgongo/neva zinazochomozea mgongoni baada ya ajali au kujeruhiwa mgongo wako kwa kupigwa/kuanguka. Mfano: shida ipo mgongoni ila unahisi ganzi kwenye m(i)guu au m(i)guu kuwaka moto).
Visababishi vya maumivu ya mgongo:
(Ubebaji wa mizigo)

Moja ya visababishi vikuu vya maumivu ya mgongo ni
▪️Aina ya kazi unayofanya.
▪️Mkao
▪️ Ubebaji wa mizigo mizito
▪️Kulalia godoro laini na lililobonyea/linalobonyea katikati wakati wa kulala.
▪️Kujeruhiwa mgongo wako kunakotokana na ajali, michezo, kuanguka, kupigwa, n.k au uvimbe (kansa) katika uti wa mgongo.
▪️Ujauzito/uzito wa kupita kiasi (kitambi)
▪️Msongo wa mawazo (stress)
▪️Magonjwa yanayoathiri mifupa (pingili) za mgongo k**a vile TB ya mifupa ya mgongo
▪️Kuvunjika au kuhama kwa mifupa ya mgogo kutoka nafasi yake.

MAUMIVU YA KIUNO:
Haya ni maumivu ya yanayotokea maeneo ya kiuno.
Maumivu haya ni moja ya mambo ambayo yanasababisha idadi kubwa ya watu katika nchi zilizoendelea kuwa waumini wazuri wa mahospitali eidha kulazwa au kuhudhuria klinik mara kwa mara. Maumivu ya mgongo yanauhusiano mkubwa sana na misuli,kano na mifupa.

VYANZO
Kwenye vertebral disc
Maumivu yanatokea pale ambapo kutakuwa na kupasuka au kulika kwa gegedu zinazounda pingili za kiuno. Misuli dhaifu na tindikali nyingi inayoingia kwenye damu pamoja na upungufu wa madini ya chokaa hali huwa mbaya zaidi.
-Kuharibika kwa misuli eneo husika.
-Mifupa na kano{ligament}
-Figo na kibofu cha mkojo.
-Matatizo ya tezi dume au kizazi kwa akina mama.
-Kula kupita kiasi au kunywa.
-Kukosa choo kwa muda mrefu.
-Misuli iliojishikiza kwenye kiuno huadhiriwa na tabia mbaya ya ulaji na uvaaji usiozingatia kanuni za afya bila kusahau magonjwa ya mifupa{arthriti}.

Mvutaji wa sigara usababisha mtu kukohoa kutokana na ni****ne. Hali hiyo husababisha mzunguko wa damu kuwa mdogo huku misuli ikipoteza ulaini elasticity na hapo ndipo maumivu huongezeka sana.
Kukosa choo kwa muda mrefu zaidi usababisha kiuno kuuma kutona na utumbo mpana kuchafuka huku gesi ikizalishwa kwa wingi.
Matatizo ya uzazi kwa jinsia zote mbili, pamoja na kuongezeka kwa lactic acid kwenye misuli.

SULUHISHO
Andika neno SULUHISHO kwenda What's App au nipigie +255756395091 nikupe mwongozo vizuri

MATATIZO YA VIUNGO(JOINT PROBLEMS),MIGUU KUWAKA MOTO,MAUMIVU YA KIUNO NA MGONGO.MATATIZO YA VIUNGO(JOINT PROBLEMS)  ya v...
10/01/2024

MATATIZO YA VIUNGO(JOINT PROBLEMS),MIGUU KUWAKA MOTO,MAUMIVU YA KIUNO NA MGONGO.

MATATIZO YA VIUNGO(JOINT PROBLEMS)
ya viungo,miguu kuwaka moto,maumivu ya kiuno na mgongo, yamekua yakiwasumbua watu wengi hasa wenye uzito mkubwa,wanaofanya mazoezi na wazee wenye umri kuanzia 55+
Hii ni kwasababu umri unavyozidi kwenda mwili unashindwa kuzalisha ute ute katika viungio vya mifupa,na hivyo kupelekea misuguano ya mifupa,ambapo husababisha maumivu makali sana na kupelekea mtu kushindwa Kukaa,Kuinuka,Kukimbia au Kutembea Kabisa!!

CHA TATIZO LA VIUNGO (JOINTS TEAR AND WEAR)

-Mara Nyingi Ugonjwa Huu Huitwa ARTHRITIS,Unasababishwa na hitilafu yoyote katika sehemu hizo za maungio ya mifupa.
Inaweza kuwa cartilage inalika,upungufu wa synovial fluid(Maji Maji Katika Maungio),maambukizi ya vijidudu katika moja ya maeneo hayo au mchanganyiko wa matatizo Mbali Mbali,Ikiwemo Uzito mkubwa.
Tabia kuu ya magonjwa haya ni maumivu kwenye maungio ya mifupa (joints) ambayo ni endelevu na ambayo hutokea eneo hilo hilo moja.

Chanzo Cha Arthritis Ni Nini...?
Ili Upate Kuelewa Vyema Chanzo cha ugonjwa huu,hebu kwanza tutazame muundo wa joint au sehemu mifupa miwili inapokutana(Maungio).
Mfano Goti ambapo mifupa miwili mmoja wa paja na mwingine wa mguu vinapokutana:

Maungio ya mifupa-Ligaments;
-Ndicho kitu kinachoshikilia mifupa hii miwili pamoja,hii ni k**a utepe wa plastiki au mpira unaonyumbuka uliozunguka eneo hilo kwa nje,ukikunja goti inanyumbuka na ukinyoosha mguu inarudi.

Cartilage;Huu ni utando unafunika eneo ambalo mifupa hugusana ili kuzuia mifupa hii isisuguane moja kwa moja,Utando huu ambao kwa kiswahili tunauita gegedu huyawezesha maungio hayo kufanya kazi kiulaini pasipo kusababisha maumivu.

Capsule;Hiki ni kitu kinachofunika maungio haya kikizunguka pande zote,ndani ya mfuko huu wa capsule kuna synovial fluid ambayo huzalishwa na synovial membrane.
Synovial fluid ni ute ute wa kulainisha sehemu hiyo ya maungio na synovial membrane ni utando ulio kwenye kuta za ndani za capsule.

K**a nilivyoeleza hapo juu,kuwa kuna aina zaidi ya 100 za ugonjwa huu wa joints au arthritis.
Katika mada yetu ya leo tutatazama aina k**a nne hivi za ugonjwa huu,tukielezea chanzo cha kila aina....

#1. Osteoarthritis.
- Hii ni aina ya arthritis inayosumbua watu wengi zaidi kuliko aina nyingine zote...
Ugonjwa huu huwapata zaidi watu wenye umri mkubwa,Osteoarthritis hutokea pale cartilage inapopoteza uwezo wake wa kubonyea na kuwa ngumu hivyo kuharibika haraka.
- Cartilage ni kiungo cha kuhimili migandamizo ya ghafla (shock absorber),Cartilage hii inapopoteza ubora wake,tendons na ligaments huvutika na kusababisha maumivu.
Hali ya uharibifu huu wa cartilage ikiendelea,mwishowe mifupa huanza kusuguana moja kwa moja na ndipo mgonjwa atakapoanza kupata maumivu makali sana sana.
- Athari za ugonjwa huanza taratibu na kuongezeka zaidi,Mgonjwa ataanza kupata maumivu kwenye joint baada ya kufanya shuguli fulani au baada ya mapumziko ya muda mrefu. Joints zitaanza kukaza siku hadi siku,Hasa wakati wa asubuhi unapotaka kuanza shughuli zako za kawaida.
Na siku zinavyosogea ndivyo utakavyoona ni vigumu zaidi kukitumia kiungo chako,Mara nyingine utaona uvimbe kwenye joint.
Osteoarthritis hushambulia zaidi nyonga,mikono,magoti na uti wa mgongo.

#2. Rheumatoid arthritis.
- Ugonjwa huu hutokea pale mfumo wa kinga ya mwili unapopungua,viungo huanza kushambuliwa, ikiwa ni pamoja na synovial membrane (synovium) na kusababisha uvimbe na maumivu.
Hali hii isipodhibitiwa,huweza kusababisha ulemavu. Ugonjwa huu unaweza pia kushambulia macho,ngozi,mapafu,midomo,damu na mishipa ya damu. Huu ni ugonjwa ambao zaidi ni wa wanawake na huwatokea zaidi wawapo kati ya umri wa miaka 40 hadi 60.
Mgonjwa atasikia maumivu na kuona uvimbe kwenye joints za pande zote za mwili;
Yaani k**a ni magoti,yote mawili yatashambuliwa na Viungo vinavyoshambuliwa zaidi ni vidole,viwiko vya mikono na miguu.

- Athari zake huonekana zaidi asubuhi unapoamka na maumivu yanaweza kudumu kwa muda wa hadi nusu saa.
Muathirika wa ugonjwa huu hujisikia mchovu muda wote, hukosa hamu ya kula na hupungua uzito,Ugonjwa huu huweza kukua zaidi na Kusababisha matatizo katika viungo vyote vya mwili.
Matatizo yanayoweza kujitokeza ugonjwa ukikua ni k**a yafuatayo:
– Macho kuwa na ukavu,maumivu,wekundu,kutopenda mwanga na kutoona vizuri
– Midomo,Ukavu au kukauka kwa lips za midomo,maumivu na maambukizi ya fizi
– Ngozi,Vijinundu chini ya ngozi kwenye maeneo yenye mifupa
-- Mapafu,Kushindwa kupumua vizuri
– Mishipa Ya Damu,Uharibifu wa mishipa ya damu
– Damu,Upungufu wa chembechembe nyekundu za damu

#3. Infectious arthritis (septic arthritic).
- Aina hii ya arthritis inatokana na maambukizi ya bacteria kwenye synovial fluid. Maambukizi haya yanaweza kuwa pia ni ya fungus au virusi.
Wadudu kutoka sehemu nyingine ya mwili iliyo karibu na maungio ya mifupa huweza kusambaa kupitia mfumo wa damu hadi kwenye joint na kuleta maambukizi.

Mara nyingi mtu mwenye aina nyingine ya arthritis ndiye anayepata maambukizi ya namna hii,Mgonjwa ataanza kwanza kupata homa, maumivu na uvimbe kwenye joint.
Maeneo ambayo hushambuliwa zaidi na aina hii ya arthritis ni goti, mabega,kiwiko cha mkono,kiganja (wrist) na vidole na mara nyingi ni eneo moja tu ndilo litakaloshambuliwa

#4. Juvenile rheumatoid arthritis (JRA).
- Ni ugonjwa ambao huwapata zaidi vijana walio na umri ulio chini ya miaka 16 na unakuja kwa namna nyingi.
Kuna aina kuu tatu za ugonjwa huu:

I. Pauciarticular JRA.
- Huu ndiyo unaoonekana zaidi na hauna madhara makubwa ukilinganisha na aina nyingine,Mtoto atasikia maumivu kwenye joints zinazofikia nne.

II. Polyarticular JRA.
- Huu hushambulia joints nyingi zaidi, zaidi ya nne na maumivu yake ni makali zaidi.
Kadri siku zinavyoongezeka, ndivyo maumivu yatakavyozidi.

III. Systemic JRA.
- Huu huonekana kwa nadra ambapo maumivu hujitokeza kwenye maeneo mengi na madhara yake kuwa makubwa zaidi,Mtoto ataanza kusikia homa za vipindi ambapo huzidi zaidi nyakati za jioni.
Hali hii inaweza kumtokea mtoto kwa muda mfupi au kwa wengine kwa muda mrefu sana.
Mtoto atapata mauvimu kwenye maungio ya mifupa (joints),uvimbe kwenye maungio hayo na kukak**aa kwa viungo.
Mtoto huyu atakosa hamu ya kula hivyo kumfanya akonde.
Ugonjwa ukizidi, mtoto anaweza kudumaa (kushindwa kukua), ukuaji wa mifupa yake kuathirika na kupata matatizo ya macho (uveitis).

Changamoto Kubwa Ya Matatizo Ya Joints Huwapata Wana Michezo,Wanyanyua Vyuma(Body Builder),Watu Wanaofanya Kazi Ngumu,Mafundi Magari,Wabeba Mizigo Na Madereva Wa Masafa Marefu Na Wafanyakazi Wa Mahofisini Wanao Fanya Kazi Za Kukaa Zaidi.

SULUHISHO KWA MGONJWA MWENYE TATIZO LA JOINTS NA KUJIKINGA NA TATIZO LA JOINTS

Hakuna Ugonjwa usio na suluhisho k**a ukiuwahi mapema,japo pia ukichelewa ina kuwa ni mbaya zaidi ila suluhisho halikosekani kabisaa!!
Na Suluhisho pekee la Tatizo La Joints ni kutumia Virutubisho(Food Supplements) kwa mwenye tatizo na wanaofanya mazoezi ili kuongeza huo ute ute kwa lengo la kuzuia misuguano ya Joints.Tuma ujumbe neno AFYA kwenda whatsapp namba 0756395091 au piga simu usaidiwe mapema.

*INAWEZEKANA KUWA NI WEWE UNAPITIA HALI HII....**i.  Unafanya mazoezi kila siku lakini bado unapata changamoto katika te...
09/02/2023

*INAWEZEKANA KUWA NI WEWE UNAPITIA HALI HII....*

*i. Unafanya mazoezi kila siku lakini bado unapata changamoto katika tendo la ndoa.*

*ii. Unakula vizuri, matunda, mboga mboga lakini bado unapata changamoto katika tendo la ndoa.*

*iii. Huna uzito mkubwa, huna magonjwa yoyote ya mfumo wa maisha k**a vile Presha, Tezi Dume nk.*
*Lakini unapata changamoto katika tendo la ndoa.*

*iv. Huna msongo wa mawazo, huna magonjwa ya kuambukiza, huna magonjwa ya zinaa n.k.*
*Lakini bado unapata changamoto katika tendo la ndoa.*

*K**a wewe ni mmojawapo na unapitia changamoto hii, basi hii Audio ni muhimu sana kwako.*

Andika neno BORESHA kwenda What's App au nipigie 0756395091 nikupe mwongozo vizuri jinsi ya kuipata package yako na kuanza mapema safari yako ya kujiimarisha mfumo wako mzima wa uzazi kupitia kirutubisho chetu pendwa

Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when AFYA BORA posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to AFYA BORA:

Share

Category