TheAxis Plus

TheAxis Plus We are the Axis, We Are The World. Join to socialize with us

18/04/2018

Haya sasa team pesaaaaaa

Usimlaumu Baba yako kwanini hakujenga  tuu...follow
17/04/2018

Usimlaumu Baba yako kwanini hakujenga tuu...follow

Mvua ya Dar Yazua Balaa Mamba Aonekana Katikati ya Jiji akitafuta msosi Shuhudia Mwenyewe Hapa
16/04/2018

Mvua ya Dar Yazua Balaa Mamba Aonekana Katikati ya Jiji akitafuta msosi Shuhudia Mwenyewe Hapa

Sema neno uiponye roho yangu
16/04/2018

Sema neno uiponye roho yangu

GHANA: Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ametuzwa tuzo ya Uongozi Bora katika tuzo za 'Africa Prestigious Award' kwa ...
16/04/2018

GHANA: Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ametuzwa tuzo ya Uongozi Bora katika tuzo za 'Africa Prestigious Award' kwa mwaka 2017/18

> Utoaji wa tuzo hiyo ulifanyika Jumamosi, Aprili 14, 2018 jijini Accra, Ghana..

ADOLF HITLER,MBABE ALIYEITAWALA DUNIA KWA MASAA Adolf Hi**er (Braunau, Austria, 20 Aprili 1889; Berlin, Ujerumani, 30 Ap...
16/04/2018

ADOLF HITLER,MBABE ALIYEITAWALA DUNIA KWA MASAA

Adolf Hi**er (Braunau, Austria, 20 Aprili 1889; Berlin, Ujerumani, 30 Aprili 1945) alikuwa dikteta wa Ujerumani kuanzia mwaka 1933 hadi kifo chake.

Adolf Hi**er akiwa mtoto mchanga.

Alizaliwa nchini Austria mwaka 1889, akaingia shule ya sekondari mwaka 1900 lakini hakufaulu, hivyo alishindwa kuendelea na masomo.

Alijaribu tena kurejea shuleni, zamu hii katika shule ya uchoraji iliyojulikana k**a Akademia ya Usanii ya Vienna akafeli tena.

Baada ya kifo cha wazazi alikosa msaada wa familia akakaa kwa muda katika nyumba kwa ajili ya watu wasio na makazi. Tangu alipohama nyumbani aliacha kufuata dini ya mama yake, Klara, akachukia moja kwa moja Kanisa Katoliki kwa kuliona halipendelei Wajerumani.

Baada ya kujaribu maisha ya msanii na mchoraji, alikuwa mwanajeshi wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia.

Mwanajeshi 1914 - 1918

Mwaka 1913 alihamia Munich katika jimbo la Bavaria (Ujerumani). Mnamo Agosti 1914, wakati wa mwanzo wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, alijitolea kwa jeshi la Bavaria ambapo kutokana na bidii na ukak**avu wake alipanda cheo na kuwa praiveti. Mwisho wa vita mwaka 1918 alikuwa na cheo cha koplo.

Kuingia siasa

Baada ya vita alikosa kazi lakini aligundua kipawa chake cha kuhutubia watu, akajiunga na siasa na kuingia katika chama kidogo cha N**i (NSDAP) alikopanda ngazi haraka.

Jaribio la mapinduzi 1923

Adolf Hi**er pamoja na dikteta wa Italia Benito Mussolini.

Hi**er alivutwa sana na mfano wa Benito Mussolini, kiongozi wa kifashisti wa Italia, aliyefaulu mwaka 1922 kupindua serikali ya Italia kwa maandamano makubwa ya wafuasi wake kuelekea Roma.

Mwaka 1923 Hi**er alijaribu kumwiga Mussolini kwa kupindua serikali ya Bavaria - k**a utangulizi wa kupindua serikali ya kitaifa huko Berlin- lakini alik**atwa na kuhukumiwa kwa uasi huo kifungo cha miaka mitano, ingawa alitumikia miezi tisa tu. Chama chake kilipigwa marufuku.

Hi**er akiwa kijana aliwahi kusoma vitabu vya Mwingereza Chamberlain aliyedai kwamba kuna mbari mbalimbali za watu zenye tabia na thamani tofauti sana.

Akiwa gerezani aliandika kitabu kilichoitwa "Mein Kampf" ("Mapambano Yangu") alikojaribu kueleza imani na siasa zake. Humo alieleza pia chuki dhidi ya Wayahudi na itikadi yake ya ubaguzi wa kimbari.

Katika itikadi hiyo mbari ya juu ni watu wa Ulaya ya Kaskazini aliowaita "Waaria", na wale ambao ni duni zaidi ni watu weusi. Vikundi vingine vimo katikati. Lakini watu wabaya kabisa katika itikadi hiyo ni Wayahudi ambao ni wajanja wakuu upande mmoja, lakini hawana uwezo wa kuunda kitu kwa upande mwingine. Hivyo wanajaribu kwa ujanja wao kutawala dunia kwa kuiba fikra na mafanikio ya Waaria.

Kujenga chama

Baada ya kutoka gerezani alirudia siasa. Alijitahidi kushika utawala wa chama cha NSDAP akakubaliwa kuwa kiongozi mkuu. Ndani ya chama alianzisha vikosi viwili vilivyovaa sare vikifanya mazoezi k**a wanamgambo na kuwa tayari kupigana na maadui wa kisiasa wakati wa maandamano.

Kikundi cha SA ("Sturmabteilung" - "Kikosi cha kushambulia") kilikuwa na watu wengi sana kikavuta hasa wanaume wasio na kazi waliovaa sare ya kahawia. Kikosi cha pili kilikuwa na watu wachache kikaitwa "SS" ("Schutzstaffel" - "Kikosi cha ulinzi") waliovaa sare nyeusi.

Chama chake hakikufaulu hadi 1929, wakati uchumi wa dunia pamoja na wa Ujerumani ulipoporomoka vibaya. Mamilioni waliachishwa kazi na kuona njaa. Katika hali hiyo watu walianza kupigia kura vyama vyenye itikadi kali.

Katika uchaguzi wa mwaka 1930 kura za NSDAP ziliongezeka kutoka 2.6% hadi 18.3%. Serikali za Ujerumani zilikuwa za vyama vingi na dhaifu.

Mwaka 1932 chama cha NSDAP kilipata 33% na kuwa chama chenye kura nyingi zaidi nchini na chama kikubwa katika bunge la Reichstag. Katika hali hiyo viongozi wa Dola la Ujerumani waliamua kumwingiza Hi**er katika serikali mwaka 1933.

Chansela na kiongozi wa Ujerumani

Tarehe 30 Januari 1933 Hi**er akawa Chansela wa Ujerumani. Mara moja alichukua nafasi kuwakandamiza wapinzani wake na baada ya mwaka mmoja hata wale waliomwingiza madarakani.

Baada ya mwaka mmoja utawala wake ulisimama imara kabisa ilhali wapinzani wengi walik**atwa na kupelekwa katika makambi ya KZ.

Hi**er alifuata siasa ya kujenga uchumi na kurudisha watu kazini akibahatika kwamba uchumi wa dunia ukapaa tena.

Hi**er alifuta mapatano yote ya Ujerumani yaliyodai ukubwa wa jeshi lake kuwa watu 100,000 tu akajenga jeshi kubwa, akaanzisha utawala wa kidikteta wa "Dola la Tatu" akipiga marufuku vyama vya upinzani. Alitesa wapinzani wote na watu wa mbari alizochukia, hasa Wayahudi.

Siasa dhidi ya Wayahudi

Chuki dhidi ya Wayahudi aliionyesha kwa sheria mbalimbali zilizokuwa kali zaidi na zaidi. Idadi ya Wayahudi katika Ujerumani ilikuwa ndogo, takriban nusu milioni kati ya wakazi milioni 62. Kila Mjerumani akitaka kuajiriwa na serikali au kupata nafasi ya masomo alitakiwa kuorodhesha wazazi na mababu hadi kizazi cha pili. Kwa njia hiyo Hi**er alipanga Wajerumani wote katika vikundi vya "Waaria" (ambao hawana Wayahudi katika familia), "Wayahudi" (watu wenye asili ya Kiyahudi, hata k**a wameshakuwa Wakristo tangu vizazi kadhaa au hawakufuata dini), "Wayahudi nusu" k**a mzazi mmoja alikuwa Myahudi, "Wayahudi robo" k**a mmoja kati ya mababu na mabibi wanne alikuwa Myahudi. Wayahudi na Wayahudi nusu walifukuzwa katika ajira ya serikali na walikataliwa kufanya kazi mbalimbali.

Sheria kuhusu "Aibu wa mbari" ilikataza ndoa kati ya "Waaria" na "Wayahudi"; "Wayahudi" waliondolewa uraia kamili.

Tokeo moja la siasa hiyo lilikuwa kuondoka kwa Wayahudi wengi kidogo katika Ujerumani; baada ya mashambulizi makali na mauaji mwaka 1938 mwelekeo huo uliongezeka.

Siasa yake mwaka 1939 ilisababisha Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

Behewa lililojaa maiti nje ya tanuri ya kambi la Buchenwald (Aprili 1945).

Hi**er alifuata siasa ya kukusanya Wajerumani wote wa Ulaya katika Dola la Ujerumani.

Mwaka 1938 alifaulu kuteka Austria na maeneo ya Wajerumani katika Ucheki bila upingamizi wa kimataifa.

Lakini aliposhambulia Poland tarehe 1 Septemba 1939 tendo hili lilikuwa mwanzo wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia kwa sababu Uingereza na Ufaransa walisimama imara kwa mikataba ya kusaidiana na Poland.

Wakati wa vita Hi**er alichukua mwenyewe uongozi mkuu wa jeshi. Mwanzoni alifaulu hata dhidi ya ushauri ya majenerali wake, hasa wakati wa vita dhidi ya Poland na Ufaransa. Lakini maazimio yake ya 1941 ya kushambulia Urusi na kutangaza hali ya vita dhidi ya Marekani yalikuwa mwanzo wa mwisho wake. Nguvu ya kiuchumi wa Ujerumani haikutosha kushindana na dunia yote.

Wakati wa vita aliamuru uuaji wa Wayahudi wote wa Ulaya, na inakadiriwa alifaulu kuwaua takriban milioni sita (2/3 ya Wayahudi wote wa Ulaya) pamoja na watu vya mbari mbalimbali k**a Wasinti (kati ya 200,000 na 1,500,000).

Hasa alipoona ya kwamba vita dhidi ya Urusi haikufaulu haraka jinsi alivyotegemea aliamua kumaliza jambo lililosababisha chuki yake hasa. Azimio la "usuluhisho wa mwisho wa suala la Kiyahudi" lilichukuliwa mwisho wa mwaka 1941 na kutangazwa mbele ya viongozi wachache mnamo Januari 1942 katika Mkutano wa Wannsee.

Baadaye siasa ya kuwatenda Wayahudi vibaya na kuwaua katika maeneo fulani ilibadilishwa kulenga Wayahudi wote katika nchi zote zilizokuwa chini ya athira ya Ujerumani au kutekwa na jeshi lake. Hadi mwisho wa vita Wayahudi walikusanywa kutoka kote Ulaya na kupelekwa kwa reli hadi makambi ya mauti.

Mwisho wa vita na kifo
Gazeti la Marekani "Stars and Stripes" la tarehe 2 Mei 1945 latangaza kifo cha Hi**er.

Maafisa wa jeshi ya Ujerumani walipanga mara kadhaa kumwua Hi**er. Tarehe 20 Julai 1944 alijeruhiwa na bomu ya Stauffenberg lakini hakuuawa.

Mwishoni mwa vita Hi**er alikaa Berlin hadi jeshi la Kirusi lilipokuwa limeshaingia mjini.

Tarehe 30 Aprili alijiua kwa sumu pamoja na mpenzi wake Eva Braun (alimwoa masaa tu kabla ya kujiua) na mbwa wake mpendwa "Blondi". Maiti zilichomwa kwa petroli lakini zilitambuliwa na Warusi kutokana na meno

Lori la mafuta lililoiangukia gari ya DED wa Kongwa, Mhandisi Ngusa Izengo limefanikiwa kuondolewa. Lakini mwili wa Izen...
16/04/2018

Lori la mafuta lililoiangukia gari ya DED wa Kongwa, Mhandisi Ngusa Izengo limefanikiwa kuondolewa.

Lakini mwili wa Izengo umeshindwa kunasuliwa kwenye gari yake kutokana na kuungana na kugandia kwenye vyuma.

Gari hiyo imepelekwa mjini Dodoma ambapo utaalamu zaidi utatumika kuinasua maiti iliyopo.!

Hali ilivyo eneo la TAZARA inapojengwa barabara ya juu(Flyover). Pamoja na ujenzi wa mtaro mkubwa wa maji bado haujaondo...
16/04/2018

Hali ilivyo eneo la TAZARA inapojengwa barabara ya juu(Flyover). Pamoja na ujenzi wa mtaro mkubwa wa maji bado haujaondoa tatizo.

> Hali ya miundombinu ya eneo lako ikoje? Unafikiri nini inaweza kuwa suluhisho la maji kujaa wakati wa mvua?

K**a upo mzma mpaka hivi sasa bac ucpite bila kuacha neno. Na ucsahau   maana hujui kesho yako zaidi ya mwenyewe
15/04/2018

K**a upo mzma mpaka hivi sasa bac ucpite bila kuacha neno. Na ucsahau maana hujui kesho yako zaidi ya mwenyewe

AKUTWA PORINI AKIFANYA MAPENZI NA BIBI WA MIAKA 68Kijana wa miaka 20 huko Ruvuma amekutwa porini akifanya mpenzi na bibi...
15/04/2018

AKUTWA PORINI AKIFANYA MAPENZI NA BIBI WA MIAKA 68

Kijana wa miaka 20 huko Ruvuma amekutwa porini akifanya mpenzi na bibi wa miaka 68.

Kijana alipoulizwa kwanini anafanya kitendo hicho, kasema bibi ndiye aliyemlazimisha.

15/04/2018
MASWALI MUHIMU KATIKA SHAMBULIO LA MAREKANI NCHINI SYRIA.1.Kuna maana gani kwa Marekani kupiga vituo vya kemikali Syria ...
15/04/2018

MASWALI MUHIMU KATIKA SHAMBULIO LA MAREKANI NCHINI SYRIA.

1.Kuna maana gani kwa Marekani kupiga vituo vya kemikali Syria na kumwacha Assad akiendelea kuwa Rais?

2.Kwa nini Marekani na washirika wake walikataa kusubiri ripoti ya wakaguzi na wachunguzi kwanza kuhusu madai ya kutumika silaha za kemikali?

Wakati walikuwa tayari wamewasili kufanya uchunguzi.

3.K**a kulikuwa na silaha za kemikali Katika maghala hayo baada ya kulipuliwa kwa maghala si sumu hiyo ingesambaa na kuua maelfu ya raia wa Syria?

Silaha za kemikali zinaathiri hewa na kungekuwa na silaha hizo na baada ya maghala kulipuliwa ingekuwa ni janga maana kemikali hizo zingesambaa na kuua mamia kwa maelfu ya wananchi.

4.Tangu lini silaha za kemikali zinaangamizwa kwa makombora?

Siku zote silaha za kemikali huaangamizwa kwa njia za kikemikali na hili ni zoezi linalohitaji eneo maalumu na hufanyika kwa ustadi mkubwa kabisa.

Ukilipua ama kutoboa kemikali ilipo basi utakuwa umeleta janga la kuangamiza watu.

5. Kulikuwa na sababu gani kwa Assad kutumia silaha za kemikali kuwashambulia waasi ambao tayari amewashinda vita?

Hili ni swali muhimu pia maana kwa kawaida mtu anaweza tu kutumia silaha hizi anapihisi amezidiwa kabisa na hana namna ya kujiokoa ama kushinda vita.

Yaani waasi umewazingira na umewazidi then ubebe silaha za kemikali. K**a ni kweli basi huu ni wendawazimu wa Assad.

K**a ni waasi basi walikuwa sahihi ili kutafuta msaada k**a huu wa Marekani.

6. Uhakika wa kwamba ile sumu imetumiwa na serikali Katika like shambulio ulitoka wapi?

maana inaweza kuwa ni waasi kwa upande mwingine.

Karibu kujadili.

HINTS ZA SHAMBULIO LA JANA.

Vituo vitatu vya utafiti wa silaha za kemikali vya Syria viliharibiwa vibaya jana kwa makombora na mabomu yaliyorushwa na Marekani, Uingereza na Ufaransa kuvilenga.

Mapema jeshi la Urusi lilitoa taarifa kuwa jumla ya mabomu na makombora 103 yalifyatuliwa, na kati ya hayo jumla ya makombora na mabomu 71 yaliangushwa kwa kutumia mitambo ya kizamani ya ulinzi ya Syria toka Usoviet.

Jeshi la Urusi halikutumia mtambo wake wa S400 uliopo Syria katika kuyadhibiti makombora hayo kwa kuwa hayakulenga maeneo ambayo mtambo huo unalinda.

Baadae jeshi la Marekani lilitoa taarifa pia likisema idadi ya mabomu na makombora iliyosemwa na Urusi ilikuwa sahihi(accurate) japokuwa walifyatua jumla ya mabomu na makombora 105.

Lakini jeshi la Marekani limekanusha kuwa baadhi ya makombora yalitunguliwa.

Jeshi lilisema hakuna kombora lililoangushwa kwa kuwa mitambo ya ulinzi ya Syria haitumii makombora ya kujiongoza na si rahisi kulenga kombora la kujiongoza(guided missiles ). Labda k**a wangefyatua guided missiles ili kulenga hayo makombora.

Kimsingi mashambulizi ya Marekani yalikuwa ya Mara moja tu na hayakuwa ya kuendelea na wala hayakuwa na lengo la kumwodoa Assad na hili limefanyika ili kutoufanya mgogoro wa Syria kuwa mkubwa zaidi kwa sababu ya Urusi.

Malengo ya mashambulizi haya yalikuwa kumzuia Assad kutumia silaha za kemikali kwa watu wake.

Kwa mujibu wa jenerali wa jeshi la Marekani, wao hawakuwa na nia ya kuingia vita ama mgogoro na jeshi la Urusi ndio maana walikuwa makini kuhakikisha hawashambuliani na jeshi la Urusi ambalo lipo nchini Syria na walilazimika kutoa taarifa mapema Katika jeshi la Urusi ni wapi watashambulia ili kuepuka uwezekano wa wao kushambuliana na Urusi.

Taarifa za Marekani kutoa taarifa Katika jeshi la Urusi mapema kabla ya mashambulizi zimetolewa pia na Balozi wa Marekani nchini Urusi kwamba walihakikisha wameipa taarifa Urusi mapema ili kuondoa uwezekano wa wao kushambuliana.

Mshinga JN

Address

Ilala
Dar Es Salaam
1

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when TheAxis Plus posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category