13/07/2026
Tanzania imepata heshima ya kuwa mwenyeji wa Kongamano la Kimataifa la Ukuzaji Viumbemaji Duniani (WA26T) na Kongamano la Ukuzaji Viumbemaji Afrika (AFRAQ26), baada ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jumuiya ya Wakuzaji Viumbemaji Duniani (WAS) kusaini hati ya makubaliano ya maandalizi ya kongamano hilo litakalofanyika nchini Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), kuanzia Desemba 1 hadi 4, 2026.
Makubaliano hayo yamesainiwa leo Julai 13, 2026 Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, kwa niaba ya Serikali, huku WAS ikiwakilishwa na Mwenyekiti wa Tawi la Afrika (AFRAQ), Prof. Julius Manyala.
Akizungumza baada ya utiaji saini huo, Mheshimiwa Balozi Dkt. Bashiru alisema uteuzi wa Tanzania kuwa mwenyeji wa kongamano hilo ni matokeo ya mafanikio makubwa yaliyopatikana katika sekta ya ukuzaji viumbemaji, hususan ongezeko la uzalishaji kwa zaidi ya asilimia 300 ndani ya kipindi cha miaka mitano.
Alifafanua kuwa uzalishaji wa viumbemaji umeongezeka kutoka tani 44,700 katika mwaka wa fedha 2020/2021 hadi tani 181,535.76 mwaka 2025/2026, hatua aliyoeleza kuwa imechangiwa na sera za Serikali za kuboresha mazingira ya uwekezaji, kuimarisha tafiti, kuendeleza matumizi ya teknolojia na kuongeza ushiriki wa sekta binafsi.
"WAS imeionesha Tanzania imani kubwa kwa kuipa fursa ya kuwa mwenyeji wa kongamano hili, na hii ni nafasi muhimu ya kuitangaza nchi yetu na kuonesha mafanikio tuliyoyapata katika sekta ya ukuzaji viumbemaji na Uchumi wa Buluu," alisema.
Alisema kongamano hilo linatarajiwa kushirikisha zaidi ya wajumbe 2,000 kutoka zaidi ya mataifa 100, wakiwemo watafiti, wawekezaji, watunga sera, wabunifu wa teknolojia na washirika wa maendeleo.
Kwa mujibu wa Waziri huyo, mkutano huo utafungua fursa za kuvutia uwekezaji, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, kubadilishana teknolojia na kuongeza masoko ya bidhaa za sekta ya uvuvi na ukuzaji viumbemaji.
Aliwataka wadau wote, wakiwemo vyuo vikuu, taasisi za utafiti, sekta binafsi, taasisi za fedha na mamlaka za serikali za mitaa, kushiriki kikamilifu katika maandalizi ya kongamano hilo ili kuhak