25/08/2025
Usiku wa tarehe 8 Machi 2014, ndege ya Malaysia Airlines MH370 ilipaa angani kutoka Kuala Lumpur kuelekea Beijing. Ndani ya chumba cha marubani walikuwapo watu wawili—Kapteni Zaharie Ahmad Shah, rubani mkongwe mwenye uzoefu wa miongo kadhaa na zaidi ya saa 18,000 za kurusha ndege, na Fariq Abdul Hamid, kijana mwenye ndoto kubwa, akiwa kwenye safari za mwisho za mafunzo yake ya kurusha Boeing 777.
Dakika chache baada ya kupaa, mawasiliano ya kawaida yalifanyika. Sauti ya taratibu ikasikika: “Good night, Malaysian three-seven-zero.” Ilikuwa ndiyo mara ya mwisho dunia kumsikia mmoja wa marubani hao. Baada ya hapo, ndege ikapotea kwenye rada—kama kivuli kilichomezwa na usiku wa anga.
Mpaka leo, jina la Zaharie na Fariq linatajwa kwa sauti ya mashaka na maswali yasiyo na majibu. Wao ndio walioshika usukani wa safari ya anga iliyoanza kwa kawaida, lakini ikamalizika kuwa moja ya siri kubwa zaidi katika historia ya usafiri wa ndege.
Haya yote yapo kwenye THE VAULT kwenye Dar24 Media pekee