TIC MEDIA

TIC MEDIA Ni chombo cha Habari cha Jumuiya ya Shia Ithna'ashariyyah Tanzania-TIC, Mtaa wa Kigogo,Plot na. 186

6. Uongozi wa Idara ya Ustawi wa Jamii inatoa wito kwa kila Mtanzania Shia Ithna’ashariyyah anayetaka Kitambulisho cha T...
24/04/2025

6. Uongozi wa Idara ya Ustawi wa Jamii inatoa wito kwa kila Mtanzania Shia Ithna’ashariyyah anayetaka Kitambulisho cha TIC anaweza kutuma Taarifa zake kwa Naibu Katibu Mkuu Ustawi wa Jamii TIC Taifa kwa Namba 0765851747, *Hakuna Gharama*, Taarifa zitawasilishwa kwa Ngazi husika, *Gharama zitakuwa kwa ngazi ya Mkoa au Ngazi husika*.

 -es-salaamUongozi  wa Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnaashariyyah  Tanzania  (TIC) Ukiongozwa na Sheikh Mkuu wa  Jumuiya h...
22/01/2024

-es-salaam

Uongozi wa Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnaashariyyah Tanzania (TIC) Ukiongozwa na Sheikh Mkuu wa Jumuiya hiyo MAULANA SHEIKH HEMEDI JALALA MWAKINDENGE Umefanya Ziara maalumu Leo 22 /1/2024 katika Ofisi za Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Dar Es Salaam MHE. ASKOFU JUDE THADDEUS S. RUWA'ICH Zilizopo katika kanisa la Sant Joseph Bandarini - Dar Es Salaam.

Sheikh Jalala amesema lengo la Msafara huo ni kutambuana na kujuliana hali k**a viongozi wa dini.

" Baba Askofu
Tumekuja kukujulia hali kwa sababu tunaamini sisi wote lengo letu ni moja ambalo ni kumlingania mwanaadamu ili kumuweka katika njia ilio nyooka njia ya mwenyezimungu SWT"

Katika msafara huo Sheikh Jalala aliongozana Makamo Mwenyekiti (TIC) Ndugu Abdulkarim Shamte Wakiambatana na Mataalamu wa maswala ya Uhusiano wa Kijamii kutoka Uingereza Sir. Mur'tadhwa.



  es salaam Waislamu wa madhehebu ya Shia wamefanya Matembezi ya Amani kwaajili ya kumbukumbu ya kifo cha Mtume Muhammad...
14/09/2023

es salaam

Waislamu wa madhehebu ya Shia wamefanya Matembezi ya Amani kwaajili ya kumbukumbu ya kifo cha Mtume Muhammad s.a.w.w kilichotokea mwezi 28 swafar siku k**a ya leo.

Ambapo sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Ithna'ashariyyah Tanzania Sheikh Hemedi Jalala Mwakindenge Amesema.
MTUME MUHAMMAD alikuwa ni mwenye Huruma na Upendo kwa watu na siku hii ya leo mwezi 28 swafar ni siku ambayo tunakumbuka huruma ya Mtume jinsi gani alivyokuwa akiwaonea huruma wanawake na watoto na alikuwa ni mwenye kuhitajia maadili mema katika Jamii.




 Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Ithnaasharia Tanzania Maulana Sheikh Hemedi Jalala Mwakindenge Amewataka waislam Kushik*...
20/08/2023



Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Ithnaasharia Tanzania Maulana Sheikh Hemedi Jalala Mwakindenge Amewataka waislam Kushik**ana na kuwa kitu kimoja kwasababu waumini wote ni ndugu.

Ametoa wito huo wakati akizungumza katika hafla ya Mauld ya Mtume Muhammad s.a.w.w katika kijiji cha kalole kata ya Kisiju Wilaya ya Mkuranga Pwani.

Halafa hiyo imehudhuriwa na Masheikh Mbalimbali wa baraza kuu la Waislamu Tanzania BAKWATA na Mgeni Rasmi akiwa Sheikh Hamid Masoud Jongo Mjumbe wa baraza la ulamaa BAKWATA.

Salaam za rambirambi kutoka mkoa wa Tanga
19/06/2023

Salaam za rambirambi kutoka mkoa wa Tanga

⚫```Matukio Mbalimbali ya Kuusindikiza``` *Mwili wa Marehemu Dokta Mohammed Saleh Kanju.*Masheikh na Waumini mbalimbali ...
19/06/2023

⚫```Matukio Mbalimbali ya Kuusindikiza``` *Mwili wa Marehemu Dokta Mohammed Saleh Kanju.*

Masheikh na Waumini mbalimbali wa Kiislamu Wamejitokeza kumsomea dua ya Khitma na kuswalia Marehemu Dokta Kanju

⚫Na Kusindikiza Jeneza lake

*Kwa ajili ya kuelekea kwenye Mazishi.*

```🕌Masjidul Ghadir.
TIC Makao Makuu

DARESALAM-TANZANIA.```

18/06/2023

Salam Alaykum
Idara ya wanawake TIC Taifa inatoa pole kwa shkh mkuu wa tic kwa msiba mzito wa aliyekuwa mwenye kiti mstaafu wa bodi ya wadhamin TIC Dr Mohammad s.kanju .
Idara yetu imepokea msiba huu kwa masikitiko makubwa.
Mungu amkutanishe mlezi wetu kiongozi wetu Dr kanju na maimam watukufu.
Na awape subra ndugu marafiki wanajumiaia na mashia wote Tz
Innalillah wa Inna ilahi Rajiuun🙏🙏😭😭

17/06/2023

TIC mkoani Lindi tawi la Mnang'ole leo baada ya dhuhrain waumini walifanya kisomo kifupi kwa ajili ya Marhum Alhaj Dr Muhamed Kanju,Mwenyekiti mstaafu wa Bodi ya Wadhamini TIC Taifa aliyefariki leo huku Kibaha katika Hospitali ya Mloganzila.

17/06/2023

Ofisi ya sheikh wa T. I. C Mkoa wa Morogoro kwa niaba ya Wanajumuiya wa T. I. C Morogoro tunatoka mkono wa pole kwa wafiwa wote kwa msiba mkubwa wa kiongozi wetu Mlezi wetu Dkt Kanju M. Mungu ailaze Roho yake mahala pema.

17/06/2023

Asalam Alaykum Uongozi wa TIC Mkoa wa Kilimanjaro umepokea taarifa ya msiba wa Dr kanju kwa masikitiko makubwa Allah aiweke Roho yake peponi Hakika pengo la Dr kanju ni kubwa

Rambi rambi zinaendelea kutolewa kwa kifo Cha mwenyekiti mtaafu wa bodi ya wadhamini ya Jumuiya ya Shia Tanzania-T.I.C
17/06/2023

Rambi rambi zinaendelea kutolewa kwa kifo Cha mwenyekiti mtaafu wa bodi ya wadhamini ya Jumuiya ya Shia Tanzania-T.I.C

17/06/2023

ASSALAAAMU ALAYKUM .
Uongozi wa TIC MKOA KIGOMA unatoa salamu za pole kwa viongozi wa TIC Taifa pamoja na familia kutokana na kifo cha ndugu yetu mzee wetu Mohammed Kanju Mkoa umepokea kwa masikitiko makubwa Taarifa hiyo. Allah amuweke mahala pema peponi pamoja na Maasumiina .
Amiina.

Address

Dar Es Salaam
114000

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when TIC MEDIA posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share