06/09/2024
Selena Gomez sasa anaweza kuongeza kuwa bilionea kwenye orodha ndefu ya mafanikio yake.
Mwigizaji huyo mwenye umri wa miaka 32, mwimbaji, mwekezaji na mjasiriamali amefanikiwa kufikia hatua hiyo ya kifedha na hivyo kumfanya kuwa mmoja wa mabilionea wachanga zaidi nchini Marekani, kulingana na Bloomberg, ambayo imeripoti kuwa utajiri wake wa dola bilioni 1.3.
Baadhi ya utajiri wa nyota huyo unatokana na uimbaji, ushirikiano wa chapa na uigizaji, lakini wingi wa utajiri wake unatokana na biashara yake ya Rare Beauty.