13/05/2024
Chombezo- Chibonge.
Mtunzi cadotz product
Sehemu 02
"Mimi sina mke naishi peke yangu"nilimjibu.
Alikaa kmya bila kuongea chochote kisha akanyanyua mkono wake na kunishika cheni niliokua nimevaa shingoni.
"Hii cheni nzuri Sana umenunua wapi?" Aliuliza
"Aah ni mtaani tu nilikutana na teja nikampatia za unga akanipa"niliongea kumjibu.
Niliongea nae sana kisha akakubali kwenda kulala kwangu.
Nilifurahi sana kwani nilijua hapo ndio nimeshaua.
Geto kwangu nilipokua nnaishi kulikua uswahilini kidogo hivyo nilipokua napita na mtoto wa kishua vile kila mmoja alikua ananikodolea macho.
Alikua ni mtoto mzuri umbo lake la unene liliendana sawa na kimo chake hivyo kumfanya aonekane mzuri hata rangi yake na mavazi aliyokua amevaa alimpendeza sana. Hakuna mwanaume aliyeweza kuzuia shingo yake na macho yake kumsindikiza mrembo huyu alipokua anapita.
Hata ulimi nao haukuweza kuvumilia kukaa kimya bila ya kutoa neno kusifia uumbaji huu.
Hakika nilijiona kidume kupita tu mtaa na mtoto yule ambae kiumri alionekana bado hajanifikia.
Nilitamani sana muda ule iwe mchana niwe nakatiza nae mtaa halafu nikutane na Mwajuma ndala ndefu au chaus*ku mdomo kunuka nadhani wangenyooka. Kupita nae tu ilikua ni heshima kwangu bado mechi niliokua naamini nitapewa. Nilikua nimepania kweli kuzichana nyavu na Shanga kuzikata.
Muda wote huo nilikua na mrembo Lily ambae alikua kimya akishangaa mitaa tuliokua tunakatiza. Kuna wakati nilikua ninamuacha atangulie ili nimtazame kwa nyuma ama kweli yule msanii alioimba *mzigo na toroli nguo inataka pasuka hakukosea* mtoto alikua amejaliwa haswa. Mimi suala la kumweka moyoni mwangu s*kua nalo kabisa nilikua nimepanga kula tu na kuondoka.
"Hivi huku huwezi kupotea jamani wakati unarudi nyumbani" aliniuliza swali ambalo lilikata ukimya uliokua umetawala kwa muda huku mimi nikiwaza jinsi nitakavyosakata kabumbu.
Ndio nilipanga kula tunda kwani nilikua naamini hakina mwanamke aliyeweza kuvuka mlango wa geto kuingia ndani akatoka salama ilikua lazima achezee tu.
"Aah huku Hamna shida ni sababu ya ugeni wako tu ila ukikaa muda utazoea"nilimjibu huku tukiendelea kutembea.
Safari yetu hatimae ilifikia tamati baada ya kufika nyumbani. Siku ile uwani kulikua na watu tofauti na s*k nyingine wengi wakisimuliana story za hapa na pale niliangaza macho nikamwona Habiba mwanamke ambae alikula sana hela zangu bila kufanikisha ligi. Nilikua nachukua sana kitendo chake cha kunifanya mimi ATM machine. Niliwasalimia kisha nikanyoosha moja kwa moja mpaka kwenye mlango wa chumba changu huku nyuma nikiwanafuatwa na Lily
"Hamiss"ilikua sauti ya k**e iliita kisha nikageuka kumwitika mwitaji.
Nini kitatokea. Us*kose sehemu ijayo