17/08/2026
: Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na ACT-Wazalendo wamelaani kukamatwa kwa Wakili Peter Madeleka, huku vikitaka Jeshi la Polisi kumuachia huru bila masharti yoyote.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Agosti 13, 2026, Madeleka alikamatwa saa 9:30 Alasiri katika eneo la Mikocheni B, Wilaya ya Kinondoni, kwa tuhuma za kudharau amri ya Mahakama Kuu.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa Wakili Madeleka anatarajiwa kufikishwa mahakamani kesho Agosti 17, 2026, kuhusiana na tuhuma hizo.
Kwa nyakati tofauti, vyama hivyo vimesema mwenendo wa kutumia vyombo vya dola kuwabana watu wanaotoa maoni kuhusu masuala ya umma unaweza kujenga hofu miongoni mwa wananchi, kudhoofisha imani ya umma katika taasisi za haki na utawala wa sheria.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Rupia, Agosti 16, 2026, chama hicho kinalitaka Jeshi la Polisi kumuachia huru Madeleka mara moja bila masharti yoyote.
“Chadema inalitaka Jeshi la Polisi kumuachia huru mara moja bila masharti yoyote. Pia, tunatoa wito kwa wadau wa haki za binadamu, wanasheria, vyombo vya habari na wananchi wote kuendelea kufuatilia kwa karibu suala hili na kuhakikisha haki za Wakili Madeleka zinalindwa,” amesema Rupia katika taarifa hiyo.
Kwa taarifa zaidi ufuate (follow) ukurasa wetu mpya wa Facebook EXTRA>>>> https://www.facebook.com/share/1QMjXDHqGv/?mibextid=wwXIfr
Powered by
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M - Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
ITVTanzania
Follow