Simulizi Zetu

Simulizi Zetu Karibu kwenye Ukurasa huu uweze kusoma stori zilizoandikwa kwenye vitabu mbalimbali

22/06/2024

Shout out to my newest followers! Excited to have you onboard! Salum Viera, Adinan Creed, Iki Love, Juv Audq

I've received 200 reactions to my posts in the past 30 days. Thanks for your support. 🙏🤗🎉
13/06/2024

I've received 200 reactions to my posts in the past 30 days. Thanks for your support. 🙏🤗🎉

13/06/2024

K**a unataka mikeka ya kuweka hela kubwa njoo tucheze

Wale wanaopenda  ODDI mbili na wapo tayari kutumia makampuni ya Warusi k**a     basi njoo jiunge kwenye group langu.NIME...
06/06/2024

Wale wanaopenda ODDI mbili na wapo tayari kutumia makampuni ya Warusi k**a basi njoo jiunge kwenye group langu.
NIMESEMA ODDI MBILI sasa uje kunisumbua unataka 10.

Group ni hili .
https://chat.whatsapp.com/GNUSrDhDtbk2RSkiRpdV1b

Mabingwa njooni katika group la mikeka la ODI 1.5-3 TU huku nawataka wenye uwezo wa kucheza hela kubwa sio wa kucheza Bu...
03/06/2024

Mabingwa njooni katika group la mikeka la ODI 1.5-3 TU huku nawataka wenye uwezo wa kucheza hela kubwa sio wa kucheza Buku.
MIKEKA NI BUREEEEE

https://chat.whatsapp.com/GNUSrDhDtbk2RSkiRpdV1b

Nimesema huku ODI ni 2 sasa uje kuanza kunisumbua unataka ODi 10.

Oya wale wenzangu wa MIKEKA nataka niwambie kuwa kampuni bora ya ubashiri ya    wamejitafuta na sasa wamerudi tena.Wamer...
30/05/2024

Oya wale wenzangu wa MIKEKA nataka niwambie kuwa kampuni bora ya ubashiri ya wamejitafuta na sasa wamerudi tena.
Wamerudisha njia zote za malipo sahzi unaweka na kutoa pesa mwenyewe.
Jiunge kwenye group letu hapa Njoo tuwafirisi tena.
Group hili👇
https://chat.whatsapp.com/GNUSrDhDtbk2RSkiRpdV1b

UTANGULIZI… SIMULIZI YA“MWISHO NA MWANZO WA MAISHA YANGU”ningependa kusema nilikufa kifo cha heshima. Lakini wengine wan...
29/05/2024

UTANGULIZI… SIMULIZI YA
“MWISHO NA MWANZO WA MAISHA YANGU”

ningependa kusema nilikufa kifo cha heshima. Lakini wengine wanaweza kusema
ni upumbavu wangu mwenyewe uliopelekea kifo changu.
Ilikuwa tarehe 24 Desemba, mkesha wa Krismasi. Vipande vya theluji vikianguka
katika anga k**a upepo ukivuma kutoka kaskazini hadi kusini. Nilikuwa nikitetemeka kwa baridi kali ingawaje nilikuwa nipo ndani ya jacketi kubwa la bluu na skafu ya kijani niliojifunga shingoni nikiwa natoka Chuo na vitabu vyangu vya vikiwa mikononi,

Nikiwa nimesimama katika kituo cha kusubiri Basi, ili linipeleke sehemu ninapoishi
Ambapo ni kambi ya Watoto Yatima, nyumba ninaeishi toka nilipozaliwa hapa duniani. Mahali palipojaa njaa, njaa na… njaa zaidi watu tuliokuwa tunaishi maeneo hayo ni wa kipato cha chini sana.
Muda huo wote nilikuwa nahisi njaa sana, Labda inaweza kuwa sababu ya kunifanya nisifikirie vizuri na kupelekea kufanya maamuzi k**a yale. Siku zote nilikuwa na njaa. Nadhani kulikuwa na watoto wengi sana

Ghafla niliona lori kubwa jekundu likija likielekea upande wawa bustani ambapo msichana mdogo alikuwa akicheza, Akili yangu haikuweza kufikiria zaidi, kitu pekee nilichoweza kuwaza ni Kwenda haraka kumuokoa mshichana yule pale alipokuwa amekaa.
Nilijikuta nimegongwa na kutupwa kando ya Barabara,maumivu makali yanipata hadi ndani ya moyo

Ghafla nikajiona nimesimama kando ya barabara tena, nikitazama watu wengi waliosimama katikati ya bustani. Nilimwona msichana mdogo ambae nahisi ndie niliemuokoa akiwa katika mikono ya mama yake.

Ni kweli nimepata ajali, au hii ni ndoto tu?
Mawazo yangu yalivurugwa na sauti za ving'ora. Inawezekana likawa ni gari la wagonjwa. Wahudumu wa afya walikuwa wakikimbia kuelekea umati mkubwa ule wa watu waliokusanyika.
nilijivuta kando ili kuwaacha, lakini sikuwa na uwezo wa kufanya hivyo kwa haraka sikuwa nanguvu zaidi za kutosha.

Ewe Mungu nisaidie, Watakuja kunigonga hawa niliona lile gari la wagonjwa likija kasi upande wangu.
Nilifunga macho yangu na kushikilia pumzi yangu, nikingojea huo mgongano unaokuja. Lakini haikutokea. Wahudumu wa afya walikuwa
tayari wameimama kwenye umati huo wenye shughuli nyingi. Nilipata hamu ya kutaka kuona watu hawa wanashangaa nini, ndipo niliposongea na kuangali ndipo nikamwona mtu aliyekuwa amelala ardhi.

Ni, Mimi...? nilijiuliza
Nimekufa? Kweli nimekufa. Sikuwa nikiota hata kidogo.
Nilitazama chini ulipo lala mwili wangu. Walikuwa wameufunika kwa shuka la kijani sikuweza kujitambua. Mwili wangu wote ulikuwa umesagika na kule kugongwa na lori. Sikutaka kujitazama nilipokuwa katika hali hii.

Badala yake, niligeuka kuwatazama wahudumu wa afya waliokuwa wakijaribu kwa
ubora wao kurudisha uhai wangu. Niliwachangamkia, nikijaribu kutamani kupata nafasi ya pili ya kuishi tena.
Nilitazama chini kwenye miguu yangu. Ndio, nilipogundua kwamba sikuwa tena kwenye ardhi. Nilikuwa nimekufa kwa hakika sasa. Hakukuwa na jinsi nilivyoweza kurudi kwenye mwili wangu.
Kipande kidogo ndani ya moyo wangu kilipiga kelele kwa majuto hata nikakumbuka

mambo ambayo sikuwa nimefanya katika kipindi kifupi cha maisha yangu.
Hapana! Sitaki kufa. Ndio bado nataka kuishi, bado, hata hivyo. Nataka kuwa na mchumba ili aweze kunibusu kwanza kabla sijakufa, Nataka kuishi Maisha mazuri baada ya kumaliza masomo yangu, niwe na pesa zangu nile chakula kizuri katika mgahawa mzuri wa kitajiri, Kubwa zaidi sitaki kufa kwasababu siwezi kumuacha mdogo wangu, Amy pekeyake bado ni mdogo sana hawezi kuishi bila mimi.

Nilifumba macho, nikihisi mwili wangu ukizunguka bila ya kujidhibiti.
Nilishusha pumzi ndefu, kisha sekunde moja baadaye, mwili wangu ulikuwa umetulia. Nikafumbua macho. Nilijikuta kwenye chumba cheupe. Kulikuwa na kitanda kimoja tu. kilikuwa cheupe sana. Kuta, sakafu, na dari pia zilikuwa nyeupe. Mwangaza wa maua hapo juu ulizidisha tu ile hali ya uweupe mule ndani.

Kwa mbele yangu nikaona Mti mdogo wa mkrismasi uliesimama kwenye kona ya chumba. Nilifarijika kidogo nilipouona. Ilinipa baadhi faraja kwamba sikuwa peke yangu katika chumba hiki chenye rangi nyeupe kila pande bila kuwa na kiumbe.

Nilikwenda kugusa jani la mti wa Mkrismasi nikapatwa na huzuni na maumivu makali moyoni, hadi machozi yakaanza kunitoka. Kumbe Mti huu ulikuwa plastiki hivyo ikaniondoa ile shauku ya kuhisi humu ndani kuwa na kiumbe hai kingine zaidi yangu.

Kulikuwa hakuna kabisa tumaini la uwepo wa kiumbe kingine chenye uhai katika chumba hiki, zaidi ya mimi mwenyewe tu mawazo yangu juu ya maisha yaligeuka uchungu mkuu. Nilikuwa katika kiwango changu cha chini kabisa cha tumaini, na hakuna faraja inayoweza kupatikana katika eneo chumba hiki.

Katika maisha yangu yote nilifanya kazi kwa bidii na kusoma hata kwa ugumu zaidi Kutaka kufikia maisha bora, nilikutana na changamoto nyingi hata zikapelekea muda mwingine kupata alama za chini zaidi katika masomo yangu lakini haikuweza kunifanya niishiwe tumaini na kunyongea k**a hali ninayo hisi muda huu aktika chumba hiki.
Nikiwa na miaka kumi na nane, nilikuwa huru kuishi peke yangu,Bila msaada wa familia yoyote au marafiki, nilikuwa k**a kinda la ndege pekee lilokuwa likijifunza
jinsi ya kupiga mbawa zake na kupaa juu katika ulimwengu huu wa kikatili, ambao sasa nilikuwa nimeuacha nyuma.

Sikuwa nimefanikiwa kuishi maish mazuri, Siku zingine tuliishi kwa kikombe kimoja cha chai na Tambi chache ila tulifanikiwa kufika kesho yake tena na masiha yakasonga mbele.

Ningefanya nini? Nilikuwa tu mwanafunzi wa chuo kikuu. Angalau hatukuwa tunaishi mitaani. Lakini niliishi Pamoja na mdogo wangu Amy, ambaye nililelewa nae katika kituo cha watoto yatima…

Atakuwaje sahizi ikiwa mimi siponae tena katika dunia ile jamani. niliwaza kichwani huku machozi yakimbubujika pale nilipokumbuka akinikimbilia wakati natoka chuo.
Amy, alikuwa msichana wa miaka kumi na moja tu. niliweka ahadi kwa Mama Pamoja na Baba kwamba ikiwa kuna chochote kingetokea kwao, ningechukua jukumu la kumlea Amy, badala yao.

Mwisho wa kusikitisha ulikuja wakati nilipofikisha miaka minane, na Amy miaka miwili tu.
Wazai wangu wote wawil walihusika katika ajali ya gari, wakatuacha mimi na Amy
bila kuwa na ndugu au jamaa wa kutulea. Na sasa mimi pia nimeondoka katika dunia ile Je, itakuwaje kwa Maisha ya mdogo wangu. Niliendelea kuwaza bila kuwa na majibu katika kichumba hiki kidogo.

Nilitaka kulia, lakini machozi hayakutoka wakat huu. Nilijaribu kuyalazimisha, lakini yalikataa. Haya Macho ya laana, kwanini hayataki kutoa machozi hata kidogo? Nilijilaani mwenyewe.
Nillifunika uso wangu kwa viganja vyangu. Ilibidi nifikirie kitu, Ingawa nilikuwa nimekufa sasa, lazima kuna kitu ningeweza kufanya.
Labda nimrudia katika umbo la mzimu na kumwangalia na niendelee kumtunza mdogo wangu?
Lakini yule mtoto anachukia mizimu na anaiogopa sana, Mara ya mwisho nakumbuka tulipokuwa tunatazama katik TV alipoonekana mzimu katika muvi aliogopa sana na kuja kujibana kwangu, sasa itakuwaje k**a nitarudi katika umbo la mzimu? Mawazo mengi bila majibu, uchungu mwingi bila machozi hakika maumivu yalikuwa makali sana yasioelezeka hata kidogo. niliendelea kuwaza zaidi na zaidi.

"Lo, kumbe maisha ni magumu sana hata wakati umekufa?"Nilijisemea.

“Unaomboleza nini wewe?”
Nilishtuka. Kuna mtu aliongea mara moja tu. Nilipepesa macho huku na kule
chumbani, sikuona mtu yoyote ila mimi mwenyewe. Niligundua kuwa yalikuwa ni mawazo yangu mwenyewe.

Ee Bwana mpendwa!
Kuna mtu alizungumza tena. Nilisikia kwa sauti kubwa ya wazi wakati huu.
Nilizunguka kwenye kiti changu, mwili wangu mzima ukitetemeka k**a jani. Nikasema Mpendwa Bwana. Tafadhali nisaidie. Waache wafu wapite kwa amani. Usiruhusu waje kunisumbua hapa nilipokaa.

“Vizuri! Kumbe unaogopa.” Sauti ikasikika tena
Niliinua kichwa changu kwa mara nyingine niliposikia hiyo sauti tena. Nahisi watakuwa wawili mana nilisikia sauti moja nzito na mwingine aliongea sauti nyembamba, Waliendelea kubishana.

Nikavuta pumzi na kukusanya nguvu za ujasiri wa kuongea. "Wewe ni nani?"

Ili kuhakikisha kwamba hayakuwa mawazo yangu tu yakinivuraga kichwani Niliangalia mazingira yangu tena, Nyuma yangu, Mbele yangu lakini hapakuwa na kitu wala mtu yoyote. Nilikuwa mimi tu katika chumba hiki cheupe.
“Huoni kwamba anastahili kutuona?” sauti nyembamba iliongea tena.
"Lakini hajafa huyu mtu." Ile sauti nzito iliongea.
"Kweli, lakini yuko hapa, sivyo, kimajukumu, yeye yupo katika wajibu wetu.”
"Sawa, jionyesha, basi." Mwenzie akamjibu.
"Hapana, jionyeshe wewe kwanza." Wa pili akamjibu pia

Nilinyamza kimya nikisikiliza namna wanayozungumza, mashaka makuu yalinipata nikahisi nitakufa tena kwa mara ya pili.Sikuelewa ni wakina nani wanaoongea, na kwanini wanasema bado sijakufa, nak**a sijafa hapa nipo wapi?
Maswali haya hayakuwa na majibu nilijikunja katika kiti kile k**a nasubiri hukumu yangu. Nikajikaza na kusema,…

“Tafadhali, acheni kubishana jionyesheni kwangu,Siwaogopi hata mmoja wenu,” niliongea kwa kujikaza ikiwa nilikuwa na hofu sana.

Ivi nilikuwa natania hapa, itakuwaje k**a atakaetokea hapa ndio mtoa hukumu ya Kwenda motoni na Kwenda peponi k**a tulivyokuwa tunafundishwa kule katika dunia ile? Atanifanya nini zaidi ya kunipeleka motoni tu kwa jeuri niliowafanyia hapa sahzi, nilihisi natamani kujikojolea ila mkojo haukutoka, niltamani kulia kwa sauti ila sauti haikutoka pia nikatulia kimya k**a sikuwepo katika chumba kile.

"Sawa, sawa," sauti ya kubwa ilisema, na kisha ndani ya sekunde niihisi k**a mwanga wa moto na moshi mweupe kisha mtu alioenekana mbele yangu akiwa amevaa vazi jeusi. Alionekana kijana kabisa, labda katikati ya miaka ishirini kwa hesabu zetu za kule duniani. Yeye alivaa kofia nyeusi pia, k**a mchinjaji, kwa hivyo sikuweza tazama macho yake. Naye alikuwa ameshika…Chinjio iliokuwa na makali pande zote mbili.

Ee Bwana wangu. Nisaidie. Nilirudi nyuma, nikijaribu kuwa nae mbali zaidi, mpaka miguu yangu ikagonga kitanda kilichopo nyuma yangu, na mimi nikaa nikiwa nimejikunyata pale.
Alishusha pumzi na kuanza kutembea kuelekea kule nilipokuwepo, upanga wake mkali uling’aa sana ulipokutana mwanga.

Hili jambo Sio nzuri hata kidogo. Kufa mara moja ilikuwa imenitosha inakuwaje sasa huyu mtu anakuja na panga kali hivi kwahiyo ndio amekuja kuniua kwa mara ya pili?
Ghafla mwanga mwingine na moshi ukatokea, na wakati huu, mtu mwingine alionekana, amevaa sawa na yule wa kwanza, akiwa na kofia ile ile nyeusi iliyofunika uso wake.

Kitu cha kwanza alichokifanya alipotokea mbele yangu ni kurudisha kofia yake nyuma na kumnyang'anya mwenzie ule upanga.
“Nilikuambia usishike kitu hicho. Inatisha watu,” alisema kwa kufoka yule mtu mwingine na kutengeneza ukuta mwembamba kimiujiza ulionitenganisha na wao ila ulikuwa k**a kioo hivyo tulikuwa tunaonana.

“Hmm.” Mwanaume mwingine aliinua bega lake na kugeukia pande nyingine, bila kujali hali hiyo.
"Na ondoa kofia yako. Sio adabu kuzungumza na mgeni wetu ikiwa umefunika uso wako.”

“Acha kunitawala,” yule mwingine akaongea na akarudi nyuma.
Yule ambaye alikuwa ameondoa kofia yake kwanza alinyakua kofia
ya yule mwingine na kumng'oa. Wote wawili walinigeukia mimi, ambapo sasa ilinipa mtazamo kamili wa nyuso zao. Na kitu pekee nilichofanya wakati huo ni kuvuta pumzi yangu.

Mungu wangu! Hawa ni mapacha wanaofanana nini, walionekana kuwa wazuri sana.
haikumaanisha uzuri k**a wale wavulana niliokuwa nawaona chuoni katika dunia ile. Hawa ni akina nani? Je, ndio malaika? Au Mapepo wabaya? nilijiuliza maswali mengi sana bila majibu
Nilikuwa nimesahau kabisa kuwa nimekufa na nilikuwa naangalia watoke mbele ya kope zangu.

Nani hangefanya hivyo? Unapojitenga na jamii, k**a ilivyokuwa, kwa maisha yako yote.

“Samahani,” niliwakatiza kipndi wao wanaendelea kubishana
"Tafadhali unaweza kuniambia mahali hapa ni wapi?"
Ghafla walifahamu uwepo wangu tena.

"Oh samahani. Hebu tuone sasa, Hiyo listi iko wapi?" mmoja alisema.
Yule mwingine akatoa kifaa k**a simu mfukoni na kumpatia mwenzie.

“Hebu tuone,” yule mwenzie aliyekuwa ameshika kile kifaa alisema.
Baada ya kuchunguza katika kile kifaa chenye muundo wa simu, alianza kusoma.

“Bibi Tami Green, Umri wako miaka kumi na tisa. una mdogo wako anayeitwa Amy
Green ambaye ana umri wa miaka kumi na moja. Wazazi wako walikufa katika ajali ya gari. Ulichukuliwa Kwenda kulelewa katika kituo cha watoto yatima ukiwa na umri wa miaka minane, pamoja na mdogo wako akiwa na umri wa miaka miwili. Mliishi huko hadi ulipofikisha miaka kumi na nane mwaka mmoja uliopita.

Ulimaliza secondari na ukajiunga Chuo Kikuu, ukisomea fani ya sayansi ya afya. Je ni wewe?”

“Ndiyo. Huyo ni mimi,” nilijibu.
"Jina langu ni Mvunaji," mtu huyo alisema, akiweka kifaa chake kwenye mfuko wa vazi lake. Akampa ishara mtu aliyekuwa kando yake. “Na huyu hapa ni kaka yangu.” Anaitwa “Grim”

“Mvunaji?” nilisema, nikiwa nimepigwa na butwaa, nikiwatazama kutoka kwa ndugu mmoja na mwingine. “kwahiyo mpo wawili tu?” niliuliza.
"Ndio," Mvunaji alijibu. "Sote wawili tuko kazini leo."mara zote tupo wawili.
Unafikiri tungeweza kuwa na uwezo wa kusafirisha roho zote za watu kwa haki k**a angekuwa moja tu.”

Watu wanakufa kila dakika. nisingeweza kukimbia kuzunguka dunia nzima kuwasafirisha watu waliokufa Kwenda mbinguni au kuzimu.
Mungu anatufanya tufanye kazi k**a tumechanganyikiwa, unajua” Mvunaji
alisema.
"Na hata hatupati malipo ya kutosha," Grim aliongezea.
"Acha utani wako," Mvunaji alimnong'oneza.
“Sifanyi mzaha. Sijafurahi hatupati malipo ya kutosha tunapaswa kuzungumza na Mungu kuhusu hili,” Grim alinung'unika tena.

“Sahau kuhusu malipo yetu kwa sasa. Tuna mambo ya muhimu sana ya kushughulikia. Lazima tumsafirishe Tami,” Mvunaji alimwambia kaka yake.

“Unanisafirisha? Wapi?" Niliuliza kwa hofu niliposikia mazungumzo yao ya faragha.
Nilijua nimekufa. Na hawa wanasema wanataka kunisafirisha nikawa ninahofu sana wananipeleka wapi tena na ni nani kati yao atakaenisafirisha.
Kungekuwa na njia ningerudi duniani k**a mtu aliepotea ili nikamtunze mdogo wangu Amy.

"Sawa, inategemea wewe unataka Kwenda wapi." Grim akageuza kichwa chake kwangu.
"Juu yangu?" Niliuliza huku nikiingiwa na hofu ya hali hiyo.
Ninaenda wapi? Je, ninaenda mbinguni au kuzimu? Au nitaendelea
kukwama katika hali hii ya mshangao, nikiwa sijielewi kwamba mimi ni mwanadamu au mzimu,

"Ndiyo," Mvunaji alisema. "Kwa sasa sio wakati wako wa kufa, Muda wako wa kufa bado haujafika.”

“Basi sawa. ila kwa nini nilikufa?” niliuliza huku nikiwa nimechanganyikiwa zaidi.
“Vema, tuseme tu kwamba Mungu alikuwekea mtego katika njia ya maisha,” Mvunaji alieleza.
“Kwa nini aliniwekea mtego? Je, nilikuwa sijafanya maombi ya kutosha? Ndio maana nilikufa?" maswali yalikuwa yananitoka kwa haraka bila kujijua yanatoka wapi.

"Alikuwa anajaribu kupima imani yako tu" Nilimsikia Grim akinong'ona kwa Mvunaji.
"Umesema nini?" Nilimuuliza kwa haraka.

“Hapana, hapana. Hakuna kitu,” Mvunaji alijibu kwa harakaharaka.
"Grim anajaribu kusema ni kwamba utapewa mwili mwingine na utarudi kwako. Kwa sababu Mungu alitwaa maisha yako kimakosa, atakupa mwili mwingine urudi nao tena.”

"Lakini vipi kuhusu mwili wangu wa zamani? Na vipi kuhusu mdogo wangu, Amy?”
Masuala ambayo hayajatatuliwa kuhusu mdogo wangu yalinitia wasiwasi sana
Hakika nilikuwa nimekufa, Sikukuwepo tena kwenye dunia ile ya kawaida, lakini bado sikuweza kuacha kuwa na wasiwasi juu ya ndugu yangu.

“Sawa, kuhusu mdogo wako, nina uhakika kuna baadhi ya njia ya kutatua hilo,” Mvunaji alisema. "Na kuhusu mwili wako umeharibika sana pale ulipogongwa yaani umekuwa vipande vipande haufai tena kuangaliwa na watu”

Tuanaangalia mwili wa mtu ambae amekufa kweli ili tukurudishe kwa kutumia mwili huo.

"Unasema nini?" Nilimuuliza kwa mshangao, linawezekanaje hilo?
"Kwa kweli, Tami, mwili wako umevunjwavunjwa kabisa,"nielewe,
Grim alijibu kwa sauti yake ya upole.
"Yaani umekuwa k**a mwanasesere aliyevunjika," ilibidi Mvunaji aongeze juu.

“Nyinyi wawili hamwezi kunirekebisha?” Niliuliza huku nikiwatazama.
Nilikuwa na hakika wangeweza kufanya jambo Fulani kuhusu mwili wangu wa awali.

"Tami, tuangalie," Mvunaji alisema, akiinua pindo la kofia yake nyeusi kufunua tumbo lake. "Sisi ni ngozi na mifupa tu.
Unafikiri tuna uwezo wa kubadilisha hatima yako?
Haiwezekani, sisi tunachoweza ni kukupatia mwili mpya?"

"Yule mpuuzi dereva," nilikasirika kwelikweli. "Aliendesha gari lake kwenye mwili wangu. Natumai ataenda kuzimu kwa hilo." Nilijisema.

"Ndio, hiyo ni mada nyingine ya kujadili, Ila kwasasa tujadili kuhusu hii mada yetu iliokuwa mbele yetu. Je, utakubali tukupatie mwili mwingine?” Grim aliuliza.

Sikumjibu zaidi ya kutafakari wazo hilo kichwani mwangu.
“Njoo, Tami, Angalia upande huu mzuri. Ukiingia mwili huu mpya, utaweza kumpata mdogo wako. Je! Hilo si ndio hitaji lako? Mwili mpya pia Maisha yatakuwa mapya,” Mvunaji aliingiza mawazo chanya ndani ya kichwa changu.

“Sawa,” nilitafakari huku nikitafuna mdomo wangu. Mvunaji ameongea kitu cha maana. Katika mwili wangu mpya, ninaweza kumtafuta mdogo wangu pia na nikaishi nae hata k**a sura yangu haitakuwa k**a ile alieizoea ila roho yangu itabaki kuwa ileile.

"Angalia, lango linakaribia kufunguliwa," Grim alinisihi. “Unataka kuingia
huu mwili mpya au hutaki?”

"Sawa, sina chaguo?" Nilimtazama Grim.
Alikuwa Mvunaji mwenye huruma ambaye alishika mikono yangu na kwa upole
alisema, kana kwamba ananisikitikia hali yangu, tofauti na kaka yake Grim ambaye alinidhihaki tu.

"Una chaguo. Unaweza kwenda mbinguni na usimuone tena mdogo wako, au unaweza kuingia kwenye mwili huu mpya na kumtafuta mdogo wako. Na ukamsaidie kwa njia yoyote utakayoweza.”
"Kisha mimi nikachagua kuingia katika mwili huu mpya." Niliitikia kwa kichwa kwa uchangamfu.
"Nitafanya chochote ili nikamuone mdogo wangu Amy.”

Grim kwa namna fulani aliweza kuonesha tabasamu kidogo. Niliitikia kwa kichwa
na kusema niko tayari.

Wakati Grim alikuwa karibu kufungua mlango ambao ungeniongoza kwenye mwili wangu huu mpya, nilimzuia kuomba neema chache.

“Kabla sijaingia katika mwili huu mpya, je! Naweza kuwaomba mambo machache?”
“Ni nini?” Grim alionekana kukasirishwa na kuingiliwa majukumu yake.
"Labda unaweza kuniweka kwenye mwili ambao ni mrefu kiasi Fulani k**a wa futi sita hivi?
K**a unavyoona, Mimi ni mfupi sana. Siwezi hata kufikia vikombe vikiwa kabatini.

Zaidi ya hayo, nahitaji kuwa tajiri. Sitaki tena kushinda na njaa katika mwili huu mpya. Na k**a unaweza, nataka kuwa na mpenzi wangu ambae atanipa busu langu la kwanza kabisa toka nizaliwe, Pia nizungukwe na familia yenye upendo.”

"Aaahh, unamaombi mengi sana wewe," Grim alisema kwa hasira.
"Tutafanya tuwezavyo yote unayoyataka utayapata,"Mvunaji alitabasamu na kunipungia mkono.
Ghafla, nilitupwa kwenye handaki linalozunguka, kana kwamba kimbunga kilikuwa kimenichukua kutoka kwenye chumba cheupe na kunipeleka mahali pengine. Nilifumba macho, nikisikia upepo mkali sana ukichapa nywele zangu. Nilihisi k**a napoteza ufahamu kwa ule mwendo wa upepo makli sana ambao sijawai kuuona katika Maisha yangu yote ya duniani. Mara nikakumbuka kuwa nilikuwa nimesahau kuomba jambo moja muhimu zaidi,

Daah! ningewambia waniandalie na mtu moja ambae angenipenda sana awe mume wangu 😍😍😍😍😍💑🏻🌹
Itaendelea sehemu ya Kwanza…………………………….

Imeletwa kwenu na
0787842220. WhatsApp only

Love is beautiful❣️❣️❣️❣️💃
19/05/2024

Love is beautiful❣️❣️❣️❣️💃

Ukweli kuhusu Mwanawake,“mwanawake humpenda mwanaume polepole zaidi kuliko wanaume. Mwanawake anahitaji si chini ya siku...
08/05/2024

Ukweli kuhusu Mwanawake,
“mwanawake humpenda mwanaume polepole zaidi kuliko wanaume.
Mwanawake anahitaji si chini ya siku 15 ili aanze kumpenda mwanaume wakati huo wanaume wanahitaji sekunde 8 tu kumpenda mwanamke.

Mwanamke humpenda mwanaume kwa kuzingatia vitu tofauti tofauti, Pia wanawake huvutiwa na wanaume ingwaje hawajui k**a wanavutiwa nao kwa kiasi gani”

Endelea kujiunga na Chimbo jipya la betting
Jisajili kwa link hii 👇
https://x7.lv/aroon
Promocode weka: M4C
Pia unaweza jiunga na Group langu hili kwa mikeka ya Uhakika
https://chat.whatsapp.com/CRJSbivOyGFJ3JwBblkwFY

Address

Dar Es Salaam
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Simulizi Zetu posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Simulizi Zetu:

Share