09/03/2026
JOYOUS CELEBRATION KUREJEA KWA KISHINDO MWEZI MAY
Kundi la Joyous Celebration la Afrika ya Kusini linatarajiwa kuanza kusherehekea miaka 30 tangu kuanzishwa kwake mwezi May mwaka huu kwa kufanya maonyesho ya siku 4 mfululizo kwa Mara ya kwanza.
Joyous ambao wamekuwa wakisuasua toka mkataba wake na kampuni ya simu ya MTN kumalizika miaka 5 iliyopita. Imekuwa ikiandamwa na na suala zima la uendeshaji baada ya waasisi wake Jabu na Mthunzi kuomba kujitoa katika kundi hilo mapema mwaka 2021 lakini mwenzao Dkt. Lindelani alipinga wazo hilo na kutaka kuachiwa jukumu la uendeshaji. Hata hivyo hivi karibuni Jabu alimshutumu Dkt Mkhize kwa ubadhirifu wa pesa kitu ambacho alikipinga na kutaka masuala yote ya pesa kuanzia mwanzo mpaka 2021 aulizwe Jabu kwakuwa ndiye aliyekuwa anasimamia.
Mthunzi Namba amekuwa akionekana kwenye kundi lingine la injili la Spirit of Praise ambako amekuwa akialikwa K**a mgeni maalumu.
Joyous watafanya maonyesho manne kuanzia tarehe 30/04 katika ukumbi wa Joburg theatre huku kukiwa na tetesi kwamba watatumia maonyesho hayo kurekodi album yao ya 29 maana hawajaweza kurekodi kwa miaka takribani miwili kutokana na tatizo la uendeshaji wa kundi hilo ambalo limekuwa chachu ya makundi mengi ya uimbaji barani Afrika ikiwemo Tanzania. Aidha litatangaza tarehe nyingine ya ziara zao nchini humo wiki hii