Azam TV

Azam TV Azam Media Ltd is a Tanzanian media company owned by the Bakhresa Group.

Under the AzamTV brand | Follow our other accounts AzamTV Burudani AzamSports Sinema Zetu HD

25/11/2025

Wakati baadhi ya vijana wananufaika na elimu ya mafunzo ya ufundi stadi kupitia mpango wa wanagenzi, kundi la vijana wasiopata fursa hizo limeiomba Serikali kupanua mpango huo ili uwafikie wengi zaidi.


Mhariri | John Mbalamwezi

25/11/2025

Wavuvi katika Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma wamedai kuwa takribani mashine 50 za uvuvi zimeporwa ziwani humo kuanzia Januari hadi sasa, jambo lililofanya wavuvi hao kumuombaMkuu wa Mkoa huo, Simon Sirro kuweka doria ya Jeshi la Wananchi ili kukomesha matukio hayo.


Mhariri | John Mbalamwezi

25/11/2025

Wajasiriamali wadogo katika maeneo mbalimbali nchini wameiambia kuwa wanasubiri kwa hamu utekelezaji wa ahadi ya kurasimisha shughuli zao, wakiamini kuwa endapo hilo litatekelezwa vyema, litaboresha na kurahisisha ustawi wa biashara zao za kila siku za kujipatia kipato.

Wakati wakionesha matumaini hayo, Wizara ya Viwanda na Biashara imesema tayari ipo kwenye mchakato wa kutekeleza ahadi ya Rais Samia Suluhu Hassan ya urasimishaji wa wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo ndani ya siku 100 za kwanza ofisini.


Mhariri | John Mbalamwezi

25/11/2025

Changamoto ya ukosefu wa zahanati ya kijiji katika Kijiji cha Matale, mkoani Simiyu, uliosababisha wananchi kutembea zaidi ya kilomita sita kufuata huduma za afya, imeanza kupatiwa ufumbuzi kupitia ujenzi wa zahanati mpya unaotekelezwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA).

Mradi wa zahanati hiyo, unaotekelezwa na TAWA, umefikia asilimia 63 na unagharimu zaidi ya shilingi milioni 283. Unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.


✍Rebeca Mbembela
Mhariri | John Mbalamwezi

25/11/2025

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limezitaka mamlaka zinazohusika kwa mujibu wa sheria kushirikiana kikamilifu katika kudhibiti uchafuzi wa mazingira unaotokana na kelele na mitetemo, ili kuwalinda wananchi dhidi ya athari za kiafya.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Meneja wa Uzingatiaji wa Sheria NEMC, Hamadi Taimuru amesema uchafuzi huo wa mazingira unasababisha madhara k**a kupungua kwa usikivu, msongo wa mawazo, shinikizo la damu, matatizo ya moyo na usingizi hafifu. Amesema kwa watoto, kelele huathiri umakini na uwezo wa kujifunza.


✍Upendo Michael
Mhariri | John Mbalamwezi

25/11/2025

Baada ya kuanzishwa kwa anuani za makazi, sasa Serikali imeleta programu tumizi ya ‘National Physical Addressing’ (NaPA), ambayo inamwezesha Mtanzania kupata barua ya utambulisho kutoka serikali ya mtaa bila kulazimika kufika ofisini.

Msikilize Afisa Hesabu kutoka Wizara ya Habari na Mawasiliano, Charles Semzaba, akifafanua jinsi mfumo huo unavyofanya kazi pamoja na hatua za kujiandikisha.


✍Warda John
Mhariri | John Mbalamwezi

25/11/2025

Wakulima wa chama kikuu cha wakulima wa korosho MAMCU wilayani Masasi na Nanyumbu mkoani Mtwara wamefanikiwa kukusanya zaidi ya Shilingi Bilioni 149 baada ya kuuza korosho zao katika minada miwili iliyofanyika msimu wa kilimo wa mwaka 2025/2026.

Fedha hizo zimetokana na mauzo ya korosho kwa bei ya kilo moja iliyokuwa ikiuzwa kwa zaidi ya Shilingi 2,100.

John Kasembe ana taarifa zaidi.

Mhariri

25/11/2025

Hospitali ya Mtakatifu Elizabeth ya Arusha imeanzisha kitengo maalum cha kuhudumia watoto wwanaozaliwa kabla ya wakati wao ili kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma mahsusi kwa watoto hao.

Kitengo hicho kinatarajiwa kuhudumia zaidi ya watoto 350.

Ramadhani Mvungi ameandaa taarifa ya kina.

Mhariri

25/11/2025

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amekubali kubadilishwa kwa baadhi ya vipengele via mpango wa amani kati ya nchi yake na Urusi ili kumaliza mgogoro unaoendelea baina ya nchi hizo.

Taarifa zaidi inasimuliwa hapa.

Mhariri

25/11/2025

Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzanja (TAA) imesema imeanza maboresho ya sehemu mbalimbali za Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) ikiwemo mifumo ya ulinzi kwa lengo la kuongeza ubora wa huduma na kuvutia mashirika mengi kutumia uwanja huo.

Imeandaliwa na Sheila Mkumba.

Mhariri

25/11/2025

Wajasiriamali wadogo wanaofanya shughuli zao katika Soko Kuu la Iringa wameiomba serikali na taasisi za bima kuwafikia na kuwapa elimu ya manufaa ya kuzikatia bima biashara zao ili kukabiliana na majanga ya asili.

Muhammad Nyaulingo amezungumza nao.

Mhariri

25/11/2025

Inaelezwa kuwa, mapenzi yakipungua kati ya wenza, ni moja ya sababu za kuwepo kwa vitendo vya ukatili wa kihisia, hasa kwa wanawake, msikilize Mkurugenzi wa Taasisi ya Woman of Substance, Mariam Mlembele akieleza zaidi. Je?, unakubaliana na mtazamo huu?


✍Juliana James
Mhariri |

Address

Tazara
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Azam TV posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Azam TV:

Share