17/01/2026
Mwenyekiti wa WAWATA Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam Mama Stella Rwegasira akiongea na Mamia ya WAWATA Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam waliofika katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Shukrani ya WAWATA wa Jimbo hilo.
Misa Takatifu ya Shukrani ya WAWATA Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam. Misa imeadhimishwa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu Posta Dar es Salaam na Mhashamu Henry Mchamungu, Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam.
Sambamba na Adhimisho hilo, WAWATA Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam wametoa Matoleo yao katika kituo cha kulelea watoto wenye mazingira magumu Msimbazi Center Jimboni humo, ikiwa ni Ishara ya Shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa makuu anayowajaalia katika Utume wao.
:
:
www.jugomedia.net