Bongo updates

  • Home
  • Bongo updates

Bongo updates Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Bongo updates, Digital creator, .

𝗖𝗛𝗥𝗜𝗦𝗣𝗜𝗡 𝗡𝗚𝗨𝗦𝗛𝗜🚨 ; Mshambuliaji Chrispin Ngushi atakamilisha usajili wake wa kujiunga na CoastalUnionfc  kwa mkopo akito...
13/01/2024

𝗖𝗛𝗥𝗜𝗦𝗣𝗜𝗡 𝗡𝗚𝗨𝗦𝗛𝗜

🚨 ; Mshambuliaji Chrispin Ngushi atakamilisha usajili wake wa kujiunga na CoastalUnionfc kwa mkopo akitokea Yanga SC.Makubaliano yamekamikika rasmi usiku huu na Chrispin Ngushi ataanza safari ya kwenda Coastal Union kesho kukamilisha usajili wake.

Kila la kheri Ngushi ✊

🟢🟡

Meli ya Kifahari ya abiria iliyo kubwa kuliko zote duniani ijulikanayo k**a "Icon of the Seas", imewasili kwa mara ya kw...
13/01/2024

Meli ya Kifahari ya abiria iliyo kubwa kuliko zote duniani ijulikanayo k**a "Icon of the Seas", imewasili kwa mara ya kwanza huko Miami nchini Marekani, ikitokea Finland ambako imeundwa.

Meli hiyo ilipokelewa kwa shangwe kubwa katika Bandari ya Miami na wakazi wa eneo hilo, mashabiki wa kampuni ya Meli za Royal Carribean na Wafanyakazi waliokuwa na shauku kubwa ya kushuhudia tukio hilo la kihistoria.

Pamoja na kuwa na hifadhi kubwa ya maji (waterpark) kuliko Meli zote duniani, meli hiyo ina vitu vingi vya kipekee ambavyo havikuzoeleka.

Ina urefu wa futi 154 kutokea chini, ina ghorofa 20, ndani yake kuna vitongoji nane. Ina jumla ya vyumba 2805 na inao uwezo wa kuchukua jumla ya abiria 7,600.

Meli hiyo itatoa huduma za safari za siku saba kwa watalii kwenda Mashariki au Magharibi mwa visiwa binafsi vya Karibeani.

Icon of the seas imetengenezwa katika mji wa Turku, nchini Finland, ilifanyiwa majaribio ya kwanza Juni 2023.

Meli hiyo "Icon of the Seas" inatarajiwa kuzindua rasmi safari zake Januari 27.

Kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya England Sven-Goran Eriksson (75), ameeleza baadhi ya mambo ambayo anatamani kuyafany...
13/01/2024

Kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya England Sven-Goran Eriksson (75), ameeleza baadhi ya mambo ambayo anatamani kuyafanya katika siku zake za maisha zilizobakia.

Mapema jana Kocha huyo mkongwe ameeleza kusumbuliwa na ugonjwa wa saratani ya kongosho (pancreas) iliyofikia hatua za mwisho.

Akizungumza na Sky News, Sven amesema mpango wake ni kusafiri na kuhudhuria mechi nyingi.

Aidha anayotamani zaidi awe na nafuu ya afya aweze kuiona ni kati ya kati ya England na Brazil itakayofanyika mwezi Machi huko Wembley.

"Natamani nisiwe na maumivu makali sana, ili niweze kwenda Uingereza kutizama mechi hiyo itakayochezwa Machi 23".

"Kuamka bila maumivu ni zawadi kubwa sana ambayo watu tunaichukulia kirahisi pale tunapokuwa na afya, lakini tukiugua ndio tunaelewa umuhimu wake".

Alipoulizwa ikiwa kuna nafasi kwenye soka ambayo aliwahi kuitamani bila mafanikio, alijibu,

"Kuwa Meneja wa Liverpool, sikufanikiwa, mimi bado ni shabiki wa Liverpool".

"Nakumbuka nilikuwa nikipishana sana maneno na Sir Alex Fergusson, kuna wakati tulihitaji wachezaji wengi kutoka Manchester United, hii ni kawaida, ile ilikuwa klabu bora sana"

"Mume wangu amenizawadia gari aina ya Range kwa ajili ya kuendea sokoni, ni zawadi yangu baada ya kutimiza umri wa miaka...
13/01/2024

"Mume wangu amenizawadia gari aina ya Range kwa ajili ya kuendea sokoni, ni zawadi yangu baada ya kutimiza umri wa miaka 30. Ananipenda na weusi wangu na nahisi nikijichubua nitaachika"- Joan Gray, Mwanamitindo

Afisa habari wa TP Mazembe  akiwa na afisa habari pekee mwenye medali CAF nchi hii  Hawa Mazembe ambao waliharibu kitche...
13/01/2024

Afisa habari wa TP Mazembe akiwa na afisa habari pekee mwenye medali CAF nchi hii

Hawa Mazembe ambao waliharibu kitchen party ya mwakorobo hapa kwa Mkapa, leo wamepata ushindi dhidi ya mabingwa Esperance de Tunis

Sisi tumemkanda Mazembe nje ndani watu wakasema Mazembe wamechoka wakasahau kilichowakuta. Leo Mazembe wamewakumbusha mwakarobo kuwa wao sio wabovu ila Yanga kiboko..

Address


Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Bongo updates posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

  • Address
  • Alerts
  • Claim ownership or report listing
  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share