Tanzanians choice

Tanzanians choice Amka mtanzania wakati ni Sasa Samia tena Mimi na wewe ndio tunaenda kuamua hatima yetu ndani ya miaka 5 ijayo 🙏🙏🇹🇿🇹🇿 sikiliza mziki mzuri kwa kutafuta Tjazz

16/06/2025

KUTOKA MAFINGA IRINGA TANZANIA
leo asubuhi wamelipokea gari lililobeba boat ya uokoaji kwa shangwe huku vijana wakilisindikiza kwa shangwe linalosikika .... Boat hiii Ni AMBULANCE YA MAJINI ambayo ilianza safari yake mtwara tar.5 June huku ikikadiliwa kutamatika safari hii baada ya siku 30 hapo jijini mwanza katika ziwa VICTORIA, Asante polisi wa mafinga kwa usimamizi mzuri kwa raia
Richa ya shamrashamra hizo lakini vijana wamebaki salama🙏 MAFINGA TUNASEMA OCTOBER TUNATIKI✔️
Ikulu Mawasiliano
Samia Suluhu Hassan
Msemaji Mkuu wa Serikali
MwanaFA
Gerson Msigwa

 Kutoka Bwawa la Nyerere, Mto Rufiji.
16/02/2025



Kutoka Bwawa la Nyerere, Mto Rufiji.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza kuhusu masuala ya matumizi ya Nishati...
16/02/2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza kuhusu masuala ya matumizi ya Nishati Safi ya kupikia kwenye Mkutano wa Kawaida wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika katika ukumbi wa Nelson Mandela uliopo Makao Makuu ya Umoja huo, Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 16 Februari, 2025.
Ikulu Mawasiliano
Samia Suluhu Hassan

Kutoka kwaMsemaji Mkuu wa SerikaliGerson MsigwaAnatupa tumaini WATANZANIA
16/02/2025

Kutoka kwaMsemaji Mkuu wa Serikali
Gerson Msigwa
Anatupa tumaini WATANZANIA

Ujenzi JNHPP Wafikia Asilimia 99, Yaleta Tabasamu kwa WatanzaniaNa Mwandishi wetu- RufijiUjenzi wa mradi wa kufua umeme ...
16/02/2025

Ujenzi JNHPP Wafikia Asilimia 99, Yaleta Tabasamu kwa Watanzania

Na Mwandishi wetu- Rufiji

Ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) wenye uwezo wa kuzalisha Megawati 2,115 za umeme umefikia asilimia 99.80 ya utekelezaji wake kufikia Februari 15, 2025, ukiwa na thamani ya fedha za Kitanzania shilingi trilioni 6.558.

Akieleza kuhusu mradi huu, wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Februari 16, 2025,uliofanyika Rufiji mkoani Pwani, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamadini, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa amesema ukubwa wa mradi huo unawafanya Watanzania watembee kifua mbele ndani ya Afrika Afrika Mashariki akisema “Hakika Watanzania Tumeweza”.

Akieleza kuhusu hali ya utekelezaji wa mradi kwa ujumla, Bw. Msigwa amebainisha kuwa hadi kufikia Februari 15, 2025 mitambo nane kati ya tisa tayari inazalisha jumla ya Megawati1880, huku mtambo namba moja ukiwa katika hatua za mwisho za usimikaji na unatarajiwa kuanza majaribio mwishoni mwa mwezi Februari 2025.

Ameeleza kuwa sehemu nyingine muhimu katika utekelezaji wa mradi wa JNHPP ni utekelezaji wa mradi wa kusafirisha umeme kutoka JNHPP hadi Chalinze – kV 400, yenye urefu wa km 160 ambao umefikia asilimia 99.5 ikilinganishwa na asilimia 44 mwaka 2021/22.

“Aidha, ujenzi wa kituo cha kupoza Umeme cha Chalinze ambacho ni sehemu ya mradi huo umefikia asilimia 92 ikilinganishwa na asilimia 35.9 mwaka 2021/22. Ukamilishwaji wa miundombinu hii imewezesha umeme kusafirishwa kutoka kituo cha kuzalisha umeme cha JNHPP hadi Chalinze na kuingizwa kwenye Grid ya Taifa,” amesema Msigwa

Kuhusu malipo kwa Mkandarasi Msigwa amesema thamani ya ujenzi wa mradi wa JNHPP ni shilingi trilioni 6,558,579,983,500.28 ambapo hadi kufikia mwezi Februari 2025, mkandarasi alikuwa amelipwa kiasi cha Shilingi trilioni 6,289,992,351,216.53 ambacho ni sawa na asilimia 95.90 ya malipo yote.
Msemaji Mkuu wa Serikali
Samia Suluhu Hassan
Ikulu Mawasiliano

KAZI INAENDELEA TUNAVUKA NASamia Suluhu Hassan
16/02/2025

KAZI INAENDELEA
TUNAVUKA NA
Samia Suluhu Hassan

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongoza Mkutano wa Kawaida wa 38 wa Wakuu wa Nc...
16/02/2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongoza Mkutano wa Kawaida wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) kwa niaba ya Mwenyekiti wa AU, Rais wa Angola Mhe. João Lourenço katika ukumbi wa Nelson Mandela uliopo Makao Makuu ya Umoja huo, Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 16 Februari, 2025. Aidha, Tanzania imechaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Uongozi wa Umoja wa Afrika (Bureau of the African Union Assembly) kwa mwaka 2025.
Samia Suluhu Hassan
Ikulu Mawasiliano
Msemaji Mkuu wa Serikali
Tanzanians choice

On behalf of the Government and the people of the United Republic of Tanzania, I extend my heartfelt congratulations to ...
16/02/2025

On behalf of the Government and the people of the United Republic of Tanzania, I extend my heartfelt congratulations to His Excellency Mahmoud Ali Youssouf, on being elected as the Chairperson of the African Union Commission. I look forward to working with you in our collective pursuit for a more prosperous, united and peaceful Africa.
Samia Suluhu Hassan
Ikulu Mawasiliano

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mwenyekiti wa Kamati y...
16/02/2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mwenyekiti wa Kamati ya Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (CAHOSCC), Rais wa Kenya Mhe. William Ruto kando ya Mkutano wa Kawaida wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU), Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 16 Februari, 2025.

Ikulu Mawasiliano
Msemaji Mkuu wa Serikali

RAIS DK. MWINYI APOKEWA KWA KISHINDO PEMBA-Wanachama 2,439 wa ACT wajiunga na CCM.Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt....
16/02/2025

RAIS DK. MWINYI APOKEWA KWA KISHINDO PEMBA

-Wanachama 2,439 wa ACT wajiunga na CCM.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Hussein Ali Mwinyi amezisisitiza Jumuiya za Chama Cha Mapinduzi kuwahamasisha Wanachama na Wananchi kujiandikisha na kujitokeza kwa Wingi kupiga Kura ili CCM ishinde kwa Kishindo.

Dkt. Mwinyi ambae ni Mgombea Mteule wa Urais wa Zanzibar kwa Tiketi ya CCM ameyasema hayo alipozungumza na Wanachama na Wananchi Mauwani, Kiwani Mkoa wa Kusini Pemba Katika Mkutano Maalum wa Mapokezi yake baada ya Kuteuliwa hivi Karibuni kuwa Mgombea wa Urais wa Zanzibar.

Dkt.Mwinyi amesema kumekuwa na tabia ya baadhi ya Wana CCM kutojitokeza kupiga kura wakati wa Uchaguzi jambo linaloipunguzia Kura za Ushindi Chama hicho.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi ameipongeza UWT kwa kazi nzuri walioifanya ya Uhamasishaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura na kuiagiza kuendelea na mwamko huo.

Halikadhalika Dkt.Mwinyi amewapongeza na kuwakaribisha Wanachama 2,439 wa Chama cha ACT Wazalendo kwa Uamuzi wa Kujiunga na CCM kwani wamefanya Uamuzi sahihi na Kuwaahidi Ushirikiano wa kiwango cha juu.

Amempongeza Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuiendesha Nchi kwa Mafanikio na Kudumisha Amani.

Mapema Asubuhi Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi walijitokeza Kumpokea Dkt. Mwinyi alipowasili Uwanja wa Ndege wa Pemba wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais Wa Zanzibar Hemed Suleimani Abdalla.

Hatimaye alizungumza na Wazee wa CCM Afisi ndogo ya Chama Cha Mapinduzi Chakechake na baadae Msafara huo ukaelekea katika Mkutano na Wanachama Mauwani Kiwani ambapo Wana CCM walijipanga barabarani kumlaki Dkt. Mwinyi.
Ikulu Mawasiliano
Ikulu habari Zanzibar
Msemaji Mkuu wa Serikali

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki mkutano wa Kamati ya Wakuu wa Nchi na ...
16/02/2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki mkutano wa Kamati ya Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (CAHOSCC) kando ya Mkutano wa Kawaida wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU), Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 16 Februari, 2025.
Ikulu Mawasiliano
Msemaji Mkuu wa Serikali
Tanzanians choice

RAIS MWINYI:BADO ZANZIBAR KUNA FURSA NYINGI ZA UWEKEZAJI Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Husse...
13/02/2025

RAIS MWINYI:BADO ZANZIBAR KUNA FURSA NYINGI ZA UWEKEZAJI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar bado ina fursa nyingi za Uwekezaji katika Sekta mbalimbali na kuwakaribisha Wawekezaji kutoka Saudi Arabia kuwekeza nchini.

Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza na Wawekezaji na Wafanyabiashara wa Saudi Arabia waliofika Ikulu kuonana naye wakiwa katika ziara maalum Tanzania ya kubaini maeneo ya Ushirikiano na Uwekezaji pamoja na Biashara.

Aidha Rais Dkt.Mwinyi amezitaja sekta nyengine ambazo zina fursa za Uwekezaji ni Kilimo, Mafuta na Gesi na Miundombinu na kuushukuru Ujumbe huo kwa kuamua kuja Zanzibar kwani Ziara hiyo itafungua ukurasa mpya wa Ushirikiano wa baina ya nchi hizo mbili na kuwasisitiza kuwa Mabalozi wazuri wa kuzitangaza fursa ziliopo nchini kwao.

Naye Rais wa Shirikisho la Jumuiya za Wafanyabiashara wa Saudi Arabia Hassan Alhuwayz amesema wana nia ya dhati ya kuimarisha Ushirikiano na Zanzibar hususani katika masuala ya Biashara na Uwekezaji kwani tayari wamebaini kuwepo kwa fursa nyingi pamoja na kuvutiwa na Maendeleo yaliyofikiwa na Zanzibar na hali ya Amani iliopo.

Wakati huo huo Rais Dkt.Mwinyi alishuhudia Utiaji wa Saini wa Mikataba baina ya Zanzibar na Saudi Arabia ikiwemo Mkataba wa Ushauri kati ya Zanzibar na Kampuni ya Saudi Arabia African Investment and Development Company na Mkataba wa Ushirikiano baina ya Jumuiya ya kitaifa ya Wafanyabiashara wa Zanzibar (ZNCC)na Shirikisho la vyama vya Wafanyabiashara wa Saudi Arabia kwa lengo la kuimarisha Uwekezaji wa kimkakati na kukuza Uchumi wa Zanzibar.
Ikulu habari Zanzibar
Ikulu Mawasiliano

Address

Dar Es Salaam

Telephone

+255679592344

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tanzanians choice posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Tanzanians choice:

Share