17/01/2026
Polisi katika mji mkuu wa Uganda, Kampala, wametumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wakipinga matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais. Waandamanaji hao pia walikuwa wamewasha moto barabarani, hatua iliyolazimu polisi kuzima mioto hiyo.
Tume ya Uchaguzi ya Uganda imetangaza matokeo ya awali yanayomuonesha Rais Yoweri Museveni ambaye amekuwa madarakani tangu 1986 akiongoza kwa zaidi ya asilimia 70 ya kura. Uchaguzi huo umechafuliwa na changamoto mbalimbali, ikiwemo kuzimwa kwa intaneti nchini kote, ucheleweshaji wa upigaji kura katika baadhi ya vituo, pamoja na madai ya upinzani ya kujazwa kwa masanduku ya kura.
Cc