Wiki Books Publishers

Wiki Books Publishers A publishing house specializing in original spiritual and health books. Visit: https://wikibookspublisher.blogspot.com/?m=1

28/03/2026

Ilikuwa wazi kuwa Jonathan atarithi kiti cha baba yake Mfalme Sauli, lakini hayo hayakuwa mapenzi ya Mungu maana tayari alishaamua kuwa Daudi ndiye atakuwa Mfalme.

Vivyo hivyo, Samweli alipoenda nyumbani kwa Yese kuchagua Mfalme k**a alivyoagizwa na Mungu, Samwel, Yese na watoto wake walitegemea kuwa Eliabu mzaliwa wa kwanza ndiye atakuwa Mfalme, lakini hayo pia hayakuwa mapenzi ya Mungu maana tayari alishaamua kuwa Daudi ndiye atakuwa Mfalme.

Kila mmoja kwa wakati tofauti (Jonathani na Eliabu) waliumia sana kutoka mioyoni mwao maana kwa mtazamo wa kibinadamu ni kana kwamba walionekana hawafai mbele za Mungu kwasababu walikuwa halali kwa sifa za kibinadamu kupata nafasi hio.

Hata hivyo jambo zuri ni kuwa Jonathani na Eliabu walikubali kuwa maamuzi ya Mungu ni sahihi na hayapingwi ijapokuwa walikuwa na maumivu ya kukataliwa, hivyo wakaamua;

1. Kutunza siri ya Daudi kuwa yeye ndiye atakayekuwa Mfalme isifahamike mbele ya Sauli,
2. Walimlinda Daudi kwenye vita vikali wakati bado alikuwa hajakomaa kivita,
3. Walikubali kuwa chini ya Daudi ijapokuwa wao walikuwa
a. Wanauhalali wa sifa za kibinadamu kupata nafasi ya ufalme,
b. Wakubwa kiumri,
c. Wanauzoefu mkubwa wa kivita kuliko Daudi.

FUNZO: Mungu anapoamua nani awe nani anafahamu zaidi kusudi, hata k**a kwa namna za kibinadamu unaweza kuwa na uhalali wa nafasi hio lakini kiroho inaweza isiwe hivyo. Mungu anapoamua kuwa tofauti na unayoyatarajia kuna mawili;

i. Ukubali uwe na amani kusubiri kilicho bora zaidi au wakati mwingine ubaki hivyo hivyo.
ii. Uamue kupingana nae, ujitie mawazo, uishi kwa msongo mkubwa na mwisho uwe muasi.

JUA NAFASI YAKO

MAOMBI YA MFALME HEZEKIA - PART 1Baada ya kufa kwake Mfalme Sulemani mwana wa Daudi, mwanaye Rehoboamu akatawala juu ya ...
03/02/2026

MAOMBI YA MFALME HEZEKIA - PART 1

Baada ya kufa kwake Mfalme Sulemani mwana wa Daudi, mwanaye Rehoboamu akatawala juu ya Israeli yote, hata hivyo hakwenda katika njia sahihi mbele za Mungu kwani aliacha shauri la wazee akafuata shauri la vijana.

Mpasuko ukatokea miongoni mwa kabila 12 za Israeli, Yeroboamu mwana wa Nebati akiongoza mgogoro huo kwa kutaka makabila ya Israeli yajitenge.

Mwisho kabisa, Yeroboamu akafanikiwa kuyashawishi makabila 10 ya Israeli kumfuata na kufanya Reheboamu kubaki na makabila mawili pekee yaani Yuda na Benjamini.

Makabila 10 yakaanzisha ufalme wa kaskazini ulioitwa, Ufalme wa Israeli katika mji wa Samaria huku makabila mawili yakabaki kusini, Yerusalemu ambapo ufalme wao uliitwa Ufalme wa Yuda.

Makabila ya kaskazini yakamwasi Mungu kwa kufuata ibada za sanamu kiasi cha kutokwenda Yerusalemu kumtolea Mungu dhabihu katika sikukuu za pasaka, uasi huu uliongozwa na Yeroboamu mwenyewe. Ikawa hivyo miaka mingi kiasi cha kwamba Mungu sasa akatuma manabii kuhubiri hukumu na ya kwamba watu warudi katika njia sahihi.

Eliya mtishibi alikuwa ndiye nabii wa kwanza kuhubiri toba katika nyumba ya mfalme Ahabu na mkewe Yezebeli, hata hivyo nyumba ya Israeli walizidi kurudi nyuma na kumuasi Mungu zaidi, maanabii k**a Elisha, Amosi na Hosea nabii wa mwisho walifuatia kuendeleza kile ambacho Eliya alikianza lakini bado hali ikawa ngumu.

Mungu mwenyewe akamwambia Hosea "Efraimu amejifungamanisha na sanamu, mwache" Hos 4:17, kwahio Mungu akawaacha kabila 10 maana waliukataa wokovu.

Katika enzi hizo palikuwa na falme mbili zenye nguvu, yaani Ashuru na Misri. Mfalme wa Ashuru alikusudia kutanua mipaka yake kwa kuzivamia falme jirani, mfalme wa Ashuru akaazimia kuivamia Israeli na katika mwaka 722 akaiangusha Israeli yote na kuwa mwisho wa makabila 10 za Israeli maana kwa Ashuru kwao kuua ilikuwa k**a mchezo.
...............

Address

Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 07:00 - 22:00
Tuesday 07:00 - 22:00
Wednesday 07:00 - 22:00
Thursday 07:00 - 22:00
Friday 07:00 - 15:00
Sunday 07:00 - 12:00

Telephone

+255621142591

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Wiki Books Publishers posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Wiki Books Publishers:

Shortcuts

Share

Category