15/05/2024
Wakati mmoja Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Alphabet (kampuni mama ya Google , YouTube nk) Sundar Pichai aliwahi kunukuliwa akitoa risala fupi ya sekunde sitini akisema;
"K**a maisha yangechukuliwa mfano wa mtu anayerusha matufe matano hewani,manne yaliyoundwa kwa udongo na moja lililotengenezwa kwa mpira ,kiasi cha kwamba anatakiwa ajitahidi matufe hayo yasianguke yakagusa ardhini,na ikiwa matufe hayo yakaandikwa na kupewa majina "Kazi,Afya,Familia,Nafsi,Uhusiano na ndugu", basi isingemchukua mtu muda kutambua kuwa tufe lililotengenezwa kwa mpira ni kazi ,kwasababu kwa ikiwa kwa bahati mbaya likitua ardhini litadunda na kurudi tena hewani kwakuwa ni rahisi kubadilisha kazi lakini yale matufe mengine yakitua ardhini kwa namna yoyote yataharibika ama kuvunjika na hayawezi kuundwa kurudi k**a zamani ,ndivyo ilivyo juu ya afya ,familia ,nafsi na uhusiano na ndugu. Hivyo basi lazima tuwe makini na yale tunayoyatafuta ama kuhangaikia"
Afya ni kiungo muhimu katika maisha, hakuna jambo lolote linaloweza kukamilishwa na mtu hapa duniani k**a afya yake ni mbovu. Lakini njia sahihi ipo, nayo ni ipi ? Ni hii hapa
Yeremia 6:16
"BWANA asema hivi, Simameni katika njia kuu, mkaone, mkaulize habari za mapito ya zamani, I wapi njia iliyo njema? Mkaende katika njia hiyo, nanyi mtajipatia raha katika nafsi zenu. Lakini walisema, Hatutaki kwenda katika njia hiyo."
Mungu aliweka kanuni na utaratibu mzuri wa kuishi tangu zamani wa kuhakikisha ya kuwa mwanadamu anakuwa na ustawi mzuri wa afya ya kiroho, kimwili na kiakili ili aweze kuishi maisha yenye furaha.
Kanuni hizi ni rahisi kuzitumia kila siku zinajumuisha:
1. Kuvuta hewa safi,
2. Kupata mwanga wa jua,
3. Kuwa na kiasi,
4. Kufanya mazoezi,
5. Kunywa maji safi na salama,
6. Kupumzika,
7. Kula mlo kamili,
8. Kufanya ibada.
Kitabu hiki kimeweka bayana kanuni 8 pamoja na njia za kuzitumia hizi kanuni ili tuweze kuishi tukiwa na afya njema maishani mwetu.
ANGALIZO : Kitabu hiki hakikusudiwi kuchukua nafasi ya ushauri wa kimatibabu kutoka kwa madaktari. Msomaji anapaswa kushauriana na daktari mara kwa mara kuhusu mambo yanayohusiana na afya yake na hasa kuhusu dalili zozote zinazoweza kuhitaji uchunguzi au utunzaji wa kimatibabu.
Jina la kitabu : KANUNI 8 ZA AFYA,
https://wa.me/p/7795664330485517/255621142591
Mwandishi : WIKLIF PHINUS TUARIRA,
Bei : Tsh 4000/-,
Wachapishaji : Wiki e-Books Publishers,
Aina ya Kitabu : Nakala laini,
Mawasiliano: 0621 142591,
Barua pepe: [email protected],
Kwa huduma za uchapishaji: [email protected],
Jipatie nakala yako sasa.
"Mimi Danieli, kwa kuvisoma vitabu, nalifahamu hesabu ya miaka" Danieli 9:2.