
20/05/2025
Nimepokea taarifa rasmi Kutoka kwa Wakili Emmanuel Ukashu ambaye baada ya kupata taafifa za kuk**atwa kwa wahusika na Kuombwa na Mawakili wao tusaidie jambo hili na Msisitizo wa Ombi kutoka kwa Rais wa LSK Adv.Faith Odhiambo
Nimepokea hivi punde taarifa toka kwa Wakili Emmanuel Ukashu zikithibitisha kuwa Bwana Boniface Mwangi, mwanahabari na mtetezi wa haki za binadamu kutoka Kenya, pamoja na Bi. Agatha Atuhaire, mwanahabari na wakili kutoka Uganda, ambao walikuwa wakishikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tangu tarehe 19 Mei 2025, wamefukuzwa na kurejeshwa katika nchi zao za asili.
Inadaiwa kuwa Bwana Mwangi alik**atwa kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo kwa ajili ya kuingia nchini, ambapo aliwasili Tanzania tarehe 18 Mei 2025.
Watu hao wawili wameondolewa nchini kwa kusindikizwa rasmi na maafisa wa Idara ya Uhamiaji ya Tanzania.
K**a marafiki wa haki za binadamu, utawala wa sheria na katiba katika ukanda wa Afrika Mashariki, tunayo dhamana ya kuendelea kushirikiana na mamlaka zetu kuhakikisha kuwa mikataba ya kikanda, katiba na sheria za kitaifa na kimataifa zinazolinda haki za binadamu, wanahabari na watetezi wa haki, zinazingatiwa ipasavyo ili kuimarisha misingi ya utawala wa sheria katika ukanda wetu.
Tunasihi umuhimu wa kuheshimu misingi iliyowekwa chini ya Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu, pamoja na nyaraka nyingine zinazotambulika kimataifa ili kuimarisha uwajibikaji, uwazi na utawala bora katika eneo letu.
Wakili B.A.K. Mwabukusi.
Rais wa Chama cha Wanasheria
Tanganyika.