Kajenjere Media

  • Home
  • Kajenjere Media

Kajenjere Media KAJENJERE MEDIA
Digital creator
Official account of KAJE TV
News update & Trends story

Rais mteule wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kuhukumiwa leo Ijumaa asubuhi kwa saa za huko katika mahak**a ya New Yo...
10/01/2025

Rais mteule wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kuhukumiwa leo Ijumaa asubuhi kwa saa za huko katika mahak**a ya New York kwa kughushi rekodi za biashara. Mei mwaka jana alipatikana na hatia kwa makosa 34 yanayohusiana na malipo ya kutunza siri aliyolipwa nyota wa filamu za ngono Stormy Daniels.

Daniels alilipwa dola za kimarekani 130,000, ili anyamaze na asizungumzie kuhusu madai yake kwamba alifanya mapenzi na Trump. Trump amekana kuwa walifanya ngono na mwanamke huyo, na amekanusha makosa yoyote.

Hukumu hiyo inakuja baada ya jana usiku Mahak**a ya Juu kukataa ombi la Rais Mteule Donald Trump la kuchelewesha hukumu ya kesi hiyo. Jaji katika kesi hiyo, Juan Merchan, amedokeza kuwa hatampeleka Trump gerezani, na hatawekwa katika kipindi cha uangalizi wala hatopigwa faini.

Trump hatarajiwi kuhudhuria hukumu hiyo ana kwa ana na kuna uwezekano atahudhuria kupitia video. Trump ndiye rais mteule wa kwanza wa Marekani, au rais, kuhukumiwa kwa uhalifu.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali imevuka lengo la Ilani ya U...
10/01/2025

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali imevuka lengo la Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) ya 2020-2025 iliyoainisha ujenzi wa kilomita 275 za barabara. Ameeleza kuwa Serikali imeamua kuongeza idadi ya barabara zitakazojengwa kwa kiwango cha lami hadi kufikia kilomita 300 mijini na vijijini. Rais Dk Mwinyi ameyasema hayo alipoifungua Barabara ya Ukutini -Bandarini Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba leo Januari 10.

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imekipiga marufuku kituo cha televisheni cha Al Jazeera kufuatia mahojiano ...
10/01/2025

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imekipiga marufuku kituo cha televisheni cha Al Jazeera kufuatia mahojiano yake iliyofanya na kiongozi wa kundi la waasi la M23 ambalo limeteka maeneo mashariki mwa nchi. Kulingana na msemaji wa serikali ya Kongo, Patrick Muyaya, mamlaka ya nchi hiyo ilibatilisha kibali cha waandishi wa shirika hilo nchini humo na kwamba kituo cha Al Jazeera kilimuhoji mkuu wa mtandao wa ugaidi bila kuwa na kibali.

Siku ya Jumatano kituo cha televisheni cha Al Jazeera kilimuhoji Bertrand Bisimwa, Mkuu wa kundi la waasi la M23 linalopambana na jeshi mashariki mwa nchi. Katika mahojiano hayo Bisimwa, aliishutumu serikali ya Kinshasa kwa kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano mnamo mwezi Agosti na kudai kwamba kundi la M23 linaendesha vita kamili vinavyoendelea.

Muyaya aliyafananisha mahojiano hayo kuwa sawa na kuukumbatia ugaidi na kwamba hilo halikubaliki na kuwataka wanahabari kutotoa fursa kwa magaidi. Niliamua, baada ya tathmini na mashauriano na timu yangu, kuondoa vibali vilivyotolewa kwa waandishi wa habari wa AlJazeera, Muyaya aliwaambia waandishi wa habari.

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amesema maandalizi yanaendelea kwa ajili ya mkutano wake na Rais wa Urusi Vladimir ...
10/01/2025

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amesema maandalizi yanaendelea kwa ajili ya mkutano wake na Rais wa Urusi Vladimir Putin. Yuko tayari kukutana, na tunafanya maandalizi, Trump amewaambia waandishi wa habari kabla ya kukutana na magavana wa chama cha Republican katika makazi yake ya Mar-a-Lago huko Florida.

Rais Putin yuko tayari kukutana. Amesema hayo hadharani, ni lazima tukomeshe vita hivi, Trump aliongeza, akizungumzia vita vya Ukraine, ambavyo ameahidi kuvimaliza lakini hajaweka bayana ni njia gani hasa amepanga kuzitumia. Reuters imeripoti kuwa Trump pia hakutaja ni lini mkutano huo unaweza kufanyika.

Ikulu ya Kremlin bado haijazungumzia maneno ya Trump, lakini siku moja kabla, msemaji wa rais wa Urusi, Dmitry Peskov aliwaambia waandishi wa habari, ikiwa Trump ataendelea na nia yake ya kutaka kuzungumza na rais wa Urusi baada ya kuapishwa Januari 20, Moscow inakaribisha hilo.

Peskov alisema Alhamisi kuwa hadi sasa hakujawa na maombi ya mkutano k**a huo kutoka upande wa Marekani. Putin mwenyewe alisema kwa njia ya moja kwa moja mwezi Desemba kwamba yuko tayari kukutana na Trump.

10/01/2025

Moto wa nyika huko Los Angeles umesababisha vifo vya takribani watu 10, huku maafisa wakionya kwamba upepo mkali unaweza...
10/01/2025

Moto wa nyika huko Los Angeles umesababisha vifo vya takribani watu 10, huku maafisa wakionya kwamba upepo mkali unaweza kuzidisha moto huo. Mkuu zima moto katika eneo hilo ameiambia BBC kwa sasa hakuna "ushahidi wa uhakika" kwamba moto huo ulianzishwa kimakusudi.

Naye mkuu wa Polisi wa Kaunti ya Los Angeles, Robert Luna anasema si salama kufikia maeneo mengi yaliyoathiriwa, huku akitarajia idadi ya vifo kuongezeka. Takriban nyumba na majengo ya kibiashara 100,000 hayana umeme huko Los Angeles, kulingana na tovuti inayofuatilia kukatika kwa umeme nchini Marekani, huku zaidi ya watu 100,000 wamehamishwa katika eneo la Los Angeles

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Geita imewahimiza wafanyabiashara kutumia kipindi hiki cha mwanzo wa mwaka 2025...
10/01/2025

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Geita imewahimiza wafanyabiashara kutumia kipindi hiki cha mwanzo wa mwaka 2025 kufika Ofisi za TRA ili kufanyiwa na kukamilisha makadirio ya kodi kwa wakati. Ofisa Mkuu wa Kodi-Idara ya Elimu na Mawasiliano, Justine Katiti amesema hayo wakati akitoa semina na elimu ya mlipa kodi kwa wafanyabiashara wa eneo la Nkome, Wilaya ya Geita mkoani hapa.

Katiti amesema hatua ya kufika mapema kwenye kwa ajili ya makadirio ya kodi kutaondoa msongamano na kuongeza ufanisi wa makadirio ya kodi kwa kila mfanyabiashara ili kupunguza malalamiko yasiyo ya lazima. Amewakumbusha wafanyabiashara kutambua kuwa kodi ya mapato inalipwa kila mwaka kwa kufuata mwaka wa kalenda ambapo makadirio hufanyika kuanzia mwezi Januari hadi Machi kwa kila mwaka.

Klabu mbili za Ligi ya Premia zinavutiwa na winga Khvitcha Kvaratskhelia, Manchester United iko tayari kuchuana na Paris...
10/01/2025

Klabu mbili za Ligi ya Premia zinavutiwa na winga Khvitcha Kvaratskhelia, Manchester United iko tayari kuchuana na Paris St-Germain kumnunua mshambuliajii wa Napoli na Georgia Khvitcha Kvaratskhelia, 23.

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeendelea na kampeni yake ya nyumba kwa nyumba ya kutoa elimu kuhusu faida na matumizi...
10/01/2025

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeendelea na kampeni yake ya nyumba kwa nyumba ya kutoa elimu kuhusu faida na matumizi ya umeme pamoja na kuhamasisha wananchi kuunganisha umeme.

Akizungumza wakati wa kampeni hiyo kwa Mkoa wa Tabora, Ofisa Maendeleo ya Jamii kutoka REA, Jaina Msuya amesema kuwa kampeni hiyo ni muendelezo wa juhudi zinazofanywa na Wakala huo kuhakikisha kila mwananchi aliyepo ndani ya wigo wa mradi umeme vijijini anaunganisha umeme.

Nia ya Serikali ni kuwaletea maendeleo wananchi wote pamoja na wa vijijini ndo maana imekuwa ikitekeleza miradi mbalimbali kwa gharama kubwa ukiwemo mradi huu wa kusambaza umeme vijijini.

Katika hatua nyingine, Msuya amesema baadhi ya wananchi wamekuwa na changamoto za kifedha na hivyo kushindwa kumudu gharama za kutandaza nyaya ndani ya nyumba zao ‘wiring’ ili kupokea umeme na hivyo wanawaelimisha kuhusu matumizi ya kifaa cha Umeme Tayari (UMETA) ambacho ni mbadala wa wiring.

Rais wa Rwanda Paul Kagame amesisitiza kuwa wapiganaji wa Kundi la M23 wanaozua ghasia nchini DR Congo hawafadhiliwi na ...
10/01/2025

Rais wa Rwanda Paul Kagame amesisitiza kuwa wapiganaji wa Kundi la M23 wanaozua ghasia nchini DR Congo hawafadhiliwi na serikali yake k**a inavyodaiwa. Rais Kagame alieleza kuwa vita katika eneo la mashariki mwa Kongo vimekuwa vikiendelea kwa miaka mingi, na kuuliza 'Je watu hapa hawajui jinsi vita hivi vilivyoanza? Vita hivi vilianza miaka mingi iliyopita na haikutokana na Rwanda’.

Aliongeza kuwa Hata sina cha kusema kwani vita hivi vilianzishwa na makundi yalikuwepo Kongo na labda baadhi yao wana asili ya Rwanda lakini walikuwa wamehamia Kongo tangu enzi za ukoloni. Rais Kagame amesema kuwa ingawa viongozi wa Kongo wameonekana kukiri kuwa waasi hao ni Wakongo na cha kushangaza ni kuwa wanadai kuwa vita hivi vinaungwa mkono na Rwanda.

Hata hivyo amesisitiza kuwa wapiganaji hao hawakutoka Rwanda, bali ni historia ya makundi ya zamani ambayo yana mizizi yake tangu wakati wa ukoloni. Kauli ya rais Kagame inajiri baada ya kuchukua udhibiti wa mji wa Masisi siku tatu zilizopita kundi la M23 huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Wakosoaji wa Rwanda wanaishutumu, kwa kuitumia M23 kupora madini kutoka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, k**a vile dhahabu, cobalt na tantalum, ambayo hutumiwa kutengeneza simu za mkononi na betri za magari yanayotumia umeme.

10/01/2025

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu amesema ana sifa na uwezo wa kuongoza nafa...
10/01/2025

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu amesema ana sifa na uwezo wa kuongoza nafasi ya uenyekiti kwa weledi. Lissu alisema kutokana na weledi wake kwenye uongozi, ndio maana Chadema ilimuona anafaa kugombea Urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Alisema anashangazwa na maneno ya baadhi ya viongozi na wanachama wa Chadema wanaosema hafai kuongoza nafasi hiyo ya uenyekiti. Alisema hatishiki na maeno waliyombatiza baada ya kuingia kwenye mchuano wa kugombea uenyekiti kwa sababu anafahamu maneno hayo ni ya kiuchaguzi tu.

Alisema katika majina anayoyakubali kati ya ma jina yote aliyobatizwa ni kuitwa mwanaharakati kwa sababu anaamini mwanaharakati ni mtu anayetetea maslahi ya wananchi kwa kiasi kikubwa, ambaye pia anaaminiwa na wananchi wanaomzunguka. Alisema lengo la kugombea nafasi hiyo ni kutaka Mbowe astaafu kwa heshima kwa sababu tangu ashike nafasi hiyo miaka 21 iliyopita, amekijenga chama hicho vizuri.

Address


Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kajenjere Media posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Kajenjere Media:

Shortcuts

  • Address
  • Alerts
  • Contact The Business
  • Claim ownership or report listing
  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share